Tunamkumbuka Bikira Maria Mtakatifu huko Loreto mlinzi wa wanaanga
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Tarehe 10 Desemba 2023 ambapo mama Kanisa anakumbuka Siku Kuu ya Bikira Maria wa Loreto, Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Kardinali Robert Francis Prevost, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu, ilikuwa ni moja ya nyakati muhimu za maadhimisho ya kumbukumbu hiyo ya Bikira Maria, wa Loteto ambayo kwa karne nyingi imekuwa na utamaduni mkuu wa ibada kwa Mama Maria katika Nyumba ya Nazareth.
Tarehe 9 Desemba 2023 katika Kanisa Kuu la Kipapa urekebishwaji kwa upya wa kihistoria wa Tafsiri ya Nyumba Takatifu ulifanyika kwa kutoa hata baraka ya moto katika uwanja ulio mbele ya Madhabahu Takatifu. Kwa hafla hiyo, wamini walialikwa kuwasha mshumaa kwenye dirisha lao kwa kusali sala ya Salamu Maria au Litania ya Bikira Maria wa Loreto, na hivyo kuungana na kuwasha moto wa utamaduni vijijini ambao tangu karne ya 17 wamekumbuka njia ya safari ya Nyumba ya Maria katika kilima cha Loreto, ambacho ilifika usiku kati ya tarehe 9 na 10 Desemba 1294 kutoka huko Nazareti, Nchi Takatifu.
Tarehe ya Siku kuu hiyo, 10 Desemba 2023 kutakuwa na maandamano na picha ya Maria wa Loreto yakiungwa mkono Jeshi la Anga, kwa ajili ya maombi na baraka za jiji na dunia. Jumatatu, tarehe 11 Desemba 2023, kwa hiyo miaka mia moja ya Jeshi la Anga itaadhimishwa kwa Ibada ya Misa Takatifu itakayoongozwa na Monsinyo Santo Marciano, Mkuu wa Kikanisa cha Kijeshi cha Italia na akiwa pamoja na Mjumbe wa Kipapa Monsinyo Fabio Dal Cin. Baadaye itafuata Sala ya Malaika wa Bwana na baraka ambaoo helikopta ya HH-139 ya Mrengo wa 15 wa Jeshi la Anga ambayo itaruka juu ya Basilica kama ishara ya heshima kwa Mlinzi wa Mbinguni yenye rangi tatu itafuata kutoka kwenye uwanja wa Basilika hio Basilica.