Maaskofu wa Congo DRC:mkataba uliotiwa saini huko Luanda wa kusitisha mapigano lazima utumike
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mkataba wa kusitisha mapigano unapaswa kutumika kikamilifu. Nivyo wanaomba Baraza la Maaskofu la Kitaifa la Congo (CENCO) kwa serikali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda. Hayo yamo katika taarifa iliyochapishwa tarehe 7 Agosti 2024 na Baraza la CENCO ambapo likiwapongeza kila mtu kwa maendeleo hayo madogo, CENCO bado linakumbusha kuwa “huu sio mkataba wa kwanza kutiwa saini kati ya serikali za Rwanda na DRC.” Maaskofu wa Congo wamesisitiza kwamba: “makubaliano yote ya awali yamekiukwa na hata kama ripoti mbalimbali kuhusiana na suala hili hazikusababisha vikwazo. Makubaliano ambayo CENCO inarejea yalitangazwa jioni ya tarehe 30 Julai 2024 na serikali ya Angola iliyokuwa imepatanisha katika mji mkuu wa Angola kati ya Congo na Rwanda.
Ghasia bado zinaendelea
Kwa mujibu wa uraisi wa Angola ulitangaza kuwa:“Kikao cha pili cha mawaziri kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Rwanda, kilichofanyika hapa Luanda chini ya upatanishi wa Jamhuri ya Angola, kilipelekea kumalizika kwa usitishaji vita ambao utaanza kutekelezwa usiku wa manane tarehe 4 Agosti 2024. Kwa njia hiyo Kinshasa inaishutumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao wameteka maeneo kadhaa ya jimbo la mashariki la Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo kwa silaha na wanajeshi wake. Serikali ya Rwanda inakanusha shutuma za Congo lakini imejitolea kuhakikisha makubaliano ya amani na waasi wa M23. Walakini, usitishaji wa mapigano hauonekani kushikilia. M23 inaendelea kusonga mbele hadi tarehe 7 Agosti 2023, iliudhibiti mji wa Nyakakoma kwenye Ziwa Eduardo baada ya kuuteka mji wa Ishasha, mpakani na Uganda. Kwa sababu hiyo Maaskofu wa Congo waliingilia kati kuwakumbusha waliotia saini kuheshimu mikataba hiyo.
Mapigano ya M23
Kati ya 2022 na Julai 2024, Baraza la Maaskofu Nchini Congo DRC(CENCO) lilifanya karibu misheni kumi y uhamasishaji nje ya nchi, kwa lengo la kuwashirikisha washirika wa kimataifa katika mzozo wa Congo na kuwahimiza kuhusika zaidi. Katika taarifa yake, hata hivyo, Baraza hilo CENCO linabainisha kuwa "washirika wa kimataifa hawajazingatia vita vya mashariki mwa DRC kuwa kipaumbele sawa na vita vya Ukraine au hali ya Mashariki ya Kati.” Vita vya mashariki mwa DRC vina athari za kikanda ambazo hazihusishi Rwanda tu (pamoja na iliyokuwa Congo ya Ubelgiji bila shaka) lakini pia nchi nyingine, kuanzia Uganda. Kulingana na ripoti iliyochapishwa tarehe 6 Agosti 2024 na Kikundi cha Utafiti cha Congo cha Chuo Kikuu cha New York, kuanza tena kwa mapigano ya M23 mnamo 2021, miaka 8 baada ya kusikilizwa mnamo 2013, inahusiana na mikataba ya kiuchumi iliyotiwa saini kati ya DRC na Uganda, ambayo ilihatarisha, ukiondoa Rwanda katika biashara ya kikanda. Kuanzishwa tena kwa M23 kungeonekana na Kigali kama njia ya kuonesha ushawishi dhidi ya jirani yake wa kaskazini, Uganda kulingana na watafiti wa Marekani. Hata hivyo, wanabainisha kuwa tangu Aprili 2022, Rwanda na Uganda zimeanza taratibu kuunga mkono kwa pamoja M23, katika kubadilisha hali dhidi ya Wakongo.