Shule ya Msingi  Robb Elementary huko  Uvalde, Texas Shule ya Msingi Robb Elementary huko Uvalde, Texas 

Papa Francisko kwa mauaji ya Texas:kila ubaya unashindwa kwa wema!

Papa Francisko ana uchungu na sala kwa ajili ya watoto na walimu waliokufa huko Texas.Ameonesha tena katika telegram aliyomtumia Askofu Mkuu wa jimbo hilo,mara baada ya kutoa wito wake wa nguvu wakati wa kuhitimisha Katekesi yake Jumatano 25 Mei 2022.Papa alisema:“moyo wangu umevunjika.Tujitahidi wote ili janga hili lisitokee tena”.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu katika telegramu yake iliyotiwa saini na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, anaelezea uchungu wake wa kina kufuatia na mauaji yaliyotokea huko, katika shule ya Msingi Robb, Uvalde, Texas, na anawakabidhi watoto na walimu waliokufa kwa kufyatuliwa risasi kwa huruma ya mwenyezi Mungu. Katika telegramu hiyo aliyomwandikia Askofu Mkuu Gustavo Garcia-Siller, wa Mtakatifu Antoni, Papa amebainisha: “Kila ubaya utashindwa kwa wema”,  na hivyo anaomba faraja kwa walijeruhiwa na kusali ili wale ambao wamejaribiwa na vurugu kinyume chake wachukue njia ya mshikamano na wa upendo.”

Misalaba yenye majina ya watoto waliokufa
Misalaba yenye majina ya watoto waliokufa

Ununuzi wa silaha kiholela ukome

Hata hivyo maneno yake yanatoa mwangwi na yale ambayo Papa alisema mara baada ya katekesi yake 25 Mei 2022, kwa waamini na mahujaji waliokuwa wameunganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican kwenye katekesi yake. Papa alisema: “Ni wakati wa kusema basi inatosha ununuzi wa silaha kiholela. Tujitahidi wote ili janga hili lisitokee tena”. Ufyatuaji wa risasi ulitokea katika Shule ya Msingi ya Robb, Uvalde ambayo kijana mwenye umri wa miaka 18 aliwaua watoto 18 na walimu watu wazima watatu. Hata hivyo kijana huyo aliuawa na polisi, lakini kwanza alimjeruhi bibi yake aliyekuwa anatafuta kumkataza hasitenda jambo hilo.

Misalaba yenye majina ya watoto waliokufa
Misalaba yenye majina ya watoto waliokufa

Sisi ni Jumuiya ndogo tunaomba maombi yenu

Shughuli zote katika eneo hilo zisitishwa, kwa mujibu wa polisi wakati wanaendelea kufanya uchunguzi wa mauaji hayo yaliyofanyika siku mbili kabla ya kufunga mwaka wa shule. Gavana Greg Abbott alisema watu wazima wawili waliouawa walikuwa mwalimu. Msimamizi wa wilaya mahali ambapo shule hiyo ipo, na ambayo walio wengi asili yao ni kutoka Amerika ya Kusni amesema “Sisi ni jumuiya ndogo na tutahitaji maombi yenu ili kupitia wakati huu.” Shambulio hilo pia lilikuja siku kumi tu baada ya shambulio jingine la ubaguzi wa rangi katika duka kuu la Buffalo, jijini New York, ambalo liliongeza mfululizo wa mauaji ya watu wengi makanisani, shuleni na madukani. Na matarajio ya mageuzi ya kanuni za silaha nchini ni dhaifu kuliko yale yaliyotokea baada ya vifo vya Sandy Hook miaka kumi iliyopita. Shule hiyo ina wanafunzi karibu 600.

Muuaji aliuawa na polisi

Kulingana na Seneta Roland Gutierrez, mhusika wa mauaji hayo alidokeza kwenye mtandao wa kijamii kwamba shambulio linaweza kutokea. Shambulio lililoanza mnamo 5:30 asubuhi, wakati mtu mwenye bunduki alipoangusha gari lake nje ya shule na kuingia ndani ya jengo hilo, kulingana na Travis, Msemaji wa Idara ya Usalama wa Umma ya Texas. Ajenti wa Doria ya Mpakani ambaye alikuwa akifanya kazi karibu wakati ufyatuaji risasi ulipoanza alikimbia mara hadi shuleni bila kungoja waongezewe nguvu na kumpiga risasi na kumuua mtu mwenye bunduki, ambaye alikuwa nyuma ya kizuizi fulani.

26 May 2022, 16:07