Tafuta

Papa Francisko asikitishwa na Janga la milipuko wa moto katika Kituo cha Mafuta cha Matanzas nchini Cuba, uliotokea tarehe 7 Agosti 2022. Papa Francisko asikitishwa na Janga la milipuko wa moto katika Kituo cha Mafuta cha Matanzas nchini Cuba, uliotokea tarehe 7 Agosti 2022. 

Mshikamano wa Papa Francisko Na Familia ya Mungu Nchini Cuba!

Papa Francisko asikitishwa na janga la milipuko wa moto katika Kituo cha Mafuta cha Matanzas nchini Cuba, uliotokea tarehe 7 Agosti 2022. Janga hili limesababisha mtu mmoja kufariki dunia, watu 121 kujeruhiwa vibaya na watu 17 wengi wao wakiwa ni Askari wa Kikosi cha Zima Moto kutojulikana mahali waliko! Baba Mtakatifu anapenda kuonesha uwepo na ukaribu wake kwa Cuba.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake kuhusu Maana na Thamani ya Uzee, Jumatano tarehe, 10 Agosti 2022, ametumia fursa hii kutuma salam zake za rambirambi kwa mahujaji kutoka Hispania, Chile na Mexico waliokuwa kwenye Katekesi yake kutokana na janga la milipuko wa moto katika Kituo cha Mafuta cha Matanzas nchini Cuba, uliotokea tarehe 7 Agosti 2022. Janga hili limesababisha mtu mmoja kufariki dunia, watu 121 kujeruhiwa vibaya na watu 17 wengi wao wakiwa ni Askari wa Kikosi cha Zima Moto kutojulikana mahali waliko! Baba Mtakatifu anapenda kuonesha uwepo na ukaribu wake kwa wale wote walioguswa na kutikiswa na janga hili la moto huko nchini Cuba. Anamwomba, Bikira Maria, Malkia wa Mbingu awaangalie wahanga wa ajali hii pamoja na familia zao. Anawaomba waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutambua jinsi ya kutoa ushuhuda wa imani na matumaini katika “Ulimwengu ujao.”

Papa Francisko asikitishwa na janga la moto nchini Cuba.
Papa Francisko asikitishwa na janga la moto nchini Cuba.

Itakumbukwa kwamba, Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, hivi karibuni, kwa niaba ya Baba Mtakatifu amemtumia salam za rambirambi, Askofu Emilio Aranguren Echeverría, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Cuba, kuwahakikishia watu wa Mungu nchini Cuba, uwepo na ukaribu wa Baba Mtakatifu Francisko katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Ana waombea ili Mwenyezi Mungu aweze kuwakirimia nguvu ya kubeba msiba huu pamoja na kuwatia shime wale wote wanaoendelea na jitihada za uokoaji. Akiwa na tumaini kwa Kristo Mfufuka, mwishoni, Baba Mtakatifu amewapatia baraka zake za kitume, ili ziwe kwao ni faraja katika kipindi hiki kigumu.

Papa Cuba

 

10 August 2022, 15:20