Baba Mtakatifu katika hotuba yake kwa Maafisa wa Mambo yandani ya Italia amekazia changamoto kuu tatu zinazowakabili Maafisa hawa: Ulinzi na Usalama; Mabadiliko ya Tabianchi na Wakimbizi Baba Mtakatifu katika hotuba yake kwa Maafisa wa Mambo yandani ya Italia amekazia changamoto kuu tatu zinazowakabili Maafisa hawa: Ulinzi na Usalama; Mabadiliko ya Tabianchi na Wakimbizi  (Vatican Media)

Maafisa wa Mambo ya Ndani ya Nchi Italia: Ulinzi, Mabadiliko ya Tabianchi na Wakimbizi

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwa Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani amekazia changamoto kuu tatu zinazowakabili Maafisa hawa: Ulinzi na Usalama; Athari za Mabadiliko ya Tabinchi pamoja na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji. Ulinzi wa raia na mali zao ni kati ya vipaumbele vya maisha na utume wao; kwa kuhakikisha kwamba, utawala wa sheria unalindwa na kuheshimiwa na wale wanaovunja sheria za nchi wanapata haki yao.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 11 Desemba 2023 amekutana na kuzungumza na Maafisa wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Italia. Hawa wana majukumu makubwa katika kusimamia: Ulinzi na usalama waraia na mali zao; sanjari utendakazi mzuri wa taasisi za Serikali kuu pamoja na Serikali za mitaa. Mtakatifu Ambrose, Askofu na Mwalimu wa Kanisa ndiye Mwombezi na Msimamizi wao kwani kabla ya kuteuliwa kuwa ni Mchungaji mkuu wa watu wa Mungu alikuwa ni Afisa wa Serikali. Alifahamika sana kwa maneno yake yasemayo “Ishi vizuri na utabadilisha nyakati.” Hapa mkazo ni kuishi vyema kwa kutekeleza dhamana na majukumu ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao; ili watu waonje na kuhisi uwepo wa Serikali na ukaribu wake kwa watu wake; kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali za ulinzi na usalama bila kusahau huduma mbalimbali wanazotoa kwa raia. Baba Mtakatifu katika hotuba yake amekazia changamoto kuu tatu zinazowakabili Maafisa hawa: Ulinzi na Usalama; Athari za Mabadiliko ya Tabinchi pamoja na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji. Ulinzi na usalama wa raia na mali zao ni kati ya vipaumbele vya maisha na utume wao; kwa kuhakikisha kwamba, utawala wa sheria unalindwa na kuheshimiwa na wale wanaovunja sheria za nchi wanapata haki yao. Huu ni uwajibikaji mkubwa, kwa kutambua pia hatari wanazokumbana nazo wanajeshi wa vikosi vya ulinzi na usalama. Wananchi wanapaswa kukumbuka ule usemi usemao: “serva ordinem et ordo servabit te; "keep order and the order will keep you" yaani “Tii Sheria na Sheria itakutunza wewe.”

Maafisa wa Mambo ya Ndani ya Italia: Usalama, Wakimbizi na Mazingira
Maafisa wa Mambo ya Ndani ya Italia: Usalama, Wakimbizi na Mazingira

Kumbe, ulinzi na usalama wa raia na mali zao unahitaji usalama wa maisha ya mtu sanjari na utulivu wa ndani. Hii ni dhamana inayotekelezwa kwa ari na moyo mkuu; kwa sadaka na majitoleo makubwa; ni kazi inayopaswa kushukuriwa. Maafisa hawa wanatekeleza dhamana na wajibu wao katika uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi kama yale yaliyoikumba mikoa ya Emilia Romagna, Toscana na Sicilia; jambo la kushangaza ni kuona umoja na mshikamano wa watu wa Mungu nchini Italia katika kukabiliana na hali kama hii. Maafisa hawa kazi yao kubwa ilikuwa ni kuratibu vyema rasilimali iliyokuwepo! Ni kitendo cha dharura kwa sasa kuratibu kikamilifu shughuli za serikali na zile zinazotekelezwa na watu binafsi, ili kulinda na kutunza mazingira nyumba ya wote. Baba Mtakatifu amegusia pia changamoto ya wimbi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji, ambao wanateseka kwa kudhulumiwa na kunyanyaswa na wakati mwingine hadi kuuwawa kikatili.

Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao ni muhimu sana
Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao ni muhimu sana

Baba Mtakatifu Francisko anasema, sera na mbinu mkakati wa Kanisa Katoliki katika huduma kwa wakimbizi na wahamiaji inajikita katika mambo makuu manne yaani: “Kuwapokea, kuwalinda, kuwaendeleza na kuwahusisha wakimbizi na wahamiaji” katika maisha ya jamii inayowapokea na kuwapatia hifadhi na usalama wa maisha! Maafisa hawa wamepewa dhamana na wajibu wa kuratibu mapokezi ya wageni na wahamiaji hawa na kuhakikisha kwamba, wanalinda na kudumisha ulinzi na usalama. Wakimbizi na wahamiaji ni amana na rasilimali kubwa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, ikiwa kama wanapokelewa vyema. Kuna changamoto kubwa ya watoto wanaozaliwa nchini Italia na idadi kubwa ya wazee. Baba Mtakatifu amehitimisha hotoba yake kwa kuwashukuru kwa kumtembelea pamoja na wajibu wao wa kulinda na kudumisha ustawi, maendeleo na mafao ya wengi; Ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Italia ina utajiri mkubwa wa umoja na mshikamano; Ukarimu na Mshikamano. Amewatakia maandalizi na hatimaye, maadhimisho mema ya Sherhe ya Noeli. Mwenyezi Mungu aliyefanyika Mwili na kukaa kati ya waja wake, awabariki.

Maafisa wa Mambo ya Ndani

 

11 December 2023, 15:30