2023.12.21 Papa alitembelea na kukutana na Mapadre wa Sekta XXVII  ya Jimbo la Roma, Kusini mwa Mji. 2023.12.21 Papa alitembelea na kukutana na Mapadre wa Sekta XXVII ya Jimbo la Roma, Kusini mwa Mji.  (Vatican Media)

Papa akutana na mapadre 30 katika Parokia ya Mt.George

Papa anaendelea na ziara yake nje kidogo ya mji mkuu,alasiri 21 Desemba 2023 alikwenda kwenye Jimbo la Roma,Sekta ya XXVII kwa ajili ya mazungumzo na mapadre wa Sekta ya Kusini mwa mji katika Kituo cha Kichungaji cha Mtakatifu Gianna Beretta Molla.Kinajihusisha na shughuli za upendo na kulikuwa na maswali na majibu yaliyochukua takriban saa mbili.Papa aliwasalimu pia watu wa kujitolea.

Vatican News

Alasiri  tarehe 21 Disemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko alirejea kutembelea parokia nje kidogo ya Roma, ya Mtakatifu George wa  Acilia, Parokia iliyopewa jina la mfiadini wa Kapadokia na pamoja na ya kisasa ambalo ilnasimama upande wa kusini mwa Mji wa Roma. Kitongoji kilichoundwa na makazi ya umma na mazingira ya kijiji cha zamani ambacho bado kinakumbuka ziara ya 1971 ya Papa Paulo VI, ambaye alitaka kwenda kukutana na wenyeji wa kitongoji hicho kipya" kwa sababu - kama alivyosema, wao walikuwa kwenye vibanda, katika hali ya wasiwasi, katika mateso, na kwa hiyo akwa nao ndani ya moyo wake, kwa sababu ya utume wake, ambao ni ule wa Kristo. Baada ya zaidi ya miaka hamsini, Papa amerudi katika eneo hili  la kusini mwa mji mkuu wa Roma. Akiwa na na gari lake dogo, Papa Francisko , baada ya kusafiri kama dakika hamsini  hivi kutoka Mtakatitifu  Marta, alifika karibu saa 10.30 jioni katika Kituo cha Kichungaji cha Mtakatifu Gianna Beretta Molla, mahali padogo pa ibada ya parokia. Hapo alikaribishwa na jumuiya ya Wana wa Upendo-Canossian ambao wanajihusisha na parokia na Kituo baadaye mapadre wa jimbo la Roma Sekta ya  XXVII na wakuu wa parokia ya sekta ya Kusini ya Jimbo. Mapadre wote wapatao thelathini, wakisindikizwa na Askofu wa sekta hiyo, Dario Gervasi, na Paroko wa Parokia Antonio Romeo Vettorato na Padre  Angelo Compagnoni, paroko wa Mtakatifu Timoteo.

Maswali na majibu kwa mapadre na Papa

Pamoja na wote, Papa, akiwa ameketi kwenye meza ndogo yenye kitambaa chekundu juu yake, alitumia muda wa saa mbili katika maswali na majibu katika Kituo cha Kichungaji - mara baada ya maombi ya awali kwa Roho Mtakatifu. “Mkutano mzuri na wa kusisimua katika mazingira ya ukarimu sana, ya kibinadamu na ya upendo na juu ya mazungumzo ya kirafiki" na makasisi. Tulijisikia kama watoto walio karibu na baba na kutiwa moyo na yeye. Kulikuwa na nafasi ya maswali na tuliondoka tukiwa na furaha. Miongoni mwa mada zilizoguswa, uzoefu wa mapadre, ukaribisho, ukaribu na watu, sinodi na mchakato wa sinodi ambayo ndiyo njia ambayo Kanisa linaelekea katika siku zijazo,” alisema hayo Askofu Gervasi mara baada ya mkutano huo kwa Vatican News.

Baba Mtakatifu akizungumza na mapadre 30 kusini mwa mji wa Roma
Baba Mtakatifu akizungumza na mapadre 30 kusini mwa mji wa Roma

Baada ya kuzungumza na mapadre, Papa Francisko aliwasalimia watu waliojitolea wa jengo hilo. Kituo ambacho mkutano ulifanyika, kwa ajili ya Mtakatifu Gianna Beretta Molla, kilichojengwa na dada wa marehemu, Virginia, ambaye alifanya kazi huko Acilia, kiukweli ni kamili ya shughuli za upendo na mshikamano. Kila asubuhi tunaanza na ugawaji wa mkate, jioni kikundi cha watu wa kujitolea huzungusha mikate katika eneo hilo ambao hutupatia mikate na pizza ambayo haijauzwa, na asubuhi iliyofuata tunasambaza kile tulichokusanya kwa wale wanaohitaji.

Mpango wa Mama

Mbali na hayo kuna "Mpango wa Mama," ambao unasaidia akina mama na watoto kuanzia  mimba hadi umri wa miaka 3: kwa sasa kuna karibu wanawake mia moja wanaoungwa mkono na kukaribishwa ambao wana shida ya kifedha, karibu wote bila kuolewa na karibu wote ni wa kigeni,” alisema Padre Vettorato. “Mara mbili kwa juma wanaweza kukusanya chakula, nguo, mahitaji ya msingi, lakini pia tunaona kama wanahitaji kuungwa mkono kwa ajili ya ziara za kitaalam au kitu kingine chochote, alifafanua Paroko huyo.

Papa akizungumza na Mapadre 30 huko kituo cha Mtakati Gianna Molla, Kusini mwa Mji wa Roma
Papa akizungumza na Mapadre 30 huko kituo cha Mtakati Gianna Molla, Kusini mwa Mji wa Roma

Ili kusaidia Mpango wa Mama. Nafasi ya Mama pia iliundwa mwaka huu, 2023 ambapo watu wengine wa kujitolea husaidia wanawake mbalimbali wanaohudhuria katika Kituo hicho kuingiliana na kufahamiana. Na tena, katika muundo huo kuna Caritas ya parokia iliyo na kituo cha kusikiliza, mapokezi na usambazaji wa vifurushi vya chakula, ambayo hufuata karibu familia 300 na "boutique ya nguo", ambayo nguo hukusanywa: Tunazifua tunazipanga na ziweze kupatikana kwa ajili ya watu wenye uhitaji, shukrani kwa kikundi cha watu wanaojitolea,” alisema Padre Romeo.

Uwepo wa ukaribu wa wahitaji 

Paroko huyo, kabla ya Baba Mtakatifu  Francisko  kuondoka muda mfupi baada ya saa 12:30 kurejea  Mtakatifu  Marta, alionesha Altare  mbayo Papa alisimama katika sala kabla ya Sakramenti Takatifu na pia Pango la  kuzaliwa kwa Kristo ilililowekwa kwa ajili ya Noeli. Kwa mzunguko huu wa ziara, Papa anaendelea - kwa namna tofauti - uteuzi katika parokia mbalimbali za Roma na eneo jirani ambalo lilikuwa na sifa ya miaka ya kwanza ya upapa wake, kisha kuingiliwa na janga la Uviko-19 na udhaifu wa kimwili wa Papa. Hata hivyo, Papa Fransisko alitaka kurejesha nyakati hizi za uwepo na ukaribu na kufanya hivyo kupitia mapadre wa parokia za majimbo mbalimbali ambao anawaachia nafasi ya kutosha kwa ajili ya kusikiliza na kujadiliana kuhusu matatizo, mahitaji.

Ziara ya kichungaji

Ziara ya kwanza kati ya hizi, kama ilivyotajwa, ilikuwa ya Septemba 28 iliyopita katika parokia ya Mtakatifu Maria wa Afya, katika Eneo la Primavalle, inayojulikana katika habari kwa mauaji ya wanawake wawili: Michelle Caruso kijana na muuguzi Rossella Nappini. Alasiri hiyo Papa alibaki kuzungumza na mapadre 35 kuhusu changamoto za kichungaji na matatizo ya eneo hilo, yenye sifa, pamoja na mambo mengine, na ugumu wa maisha ya vijana na kutengwa na jamii. Matatizo sawa na yale yaliyojitokeza katika kitongoji cha Due Torri-Villa Verde, ambapo parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa makaribisho ipo.

Kujibu maswali na majibu ya Papa kwa mapadre 30 aliokutana nao
Kujibu maswali na majibu ya Papa kwa mapadre 30 aliokutana nao

Papa Francisko alitaka kwenda huko Novemba 16 iliyopita kukutana na mapadre karibu arobaini kutoka mikoa wa 17 ambao wanashughulikia maeneo ya Tor Bella Monaca, Torre Angela, Torre Gaia na vitongoji vingine vya jirani. Maeneo ya makazi ya umma na umaskini mkubwa, pia maeneo ya mapokezi kwa wale wanaohitaji na wageni kama inavyoonyeshwa na parokia ambayo inakaribisha katika eneo lake tata ya vyumba kumi na mbili ambapo familia katika dharura ya makazi huishi, Waitaliano au wakimbizi kutoka nchi nyingine. Papa Francisko aliweza kukutana na kuwasalimia mwishoni mwa ziara yake, akiwakumbatia na kuwapa mkono.

22 December 2023, 10:58