Tafuta

Kadinali GEORGE ALENCHERRY. Kadinali GEORGE ALENCHERRY. 

Papa ametuma barua kwa Kard.Alencherry:Mchungaji wa umoja katika Kanisa

Askofu mkuu wa Ernakulam-Angamaly wa Kanisa la Syro-Malabar amehitimisha muda wake katikati ya migogoro ya ndani,ambayo msimamizi wa kitume ameteuliwa.Papa ametuma barua kumshukuru kwa bidii na ukarimu wake.Tayari 2022 alikuwa aondoke katika hali ya migawanyiko na maandamano,lakini Sinodi ya Maaskofu wa Syro-Malabar ilisema haukuwa wakati mwafaka.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Alhamis tarehe 7 Desemba 2023, Baba Mtakatifu  Francisko amekubali kujiuzulu kwa Kardinali George Alencherry, Askofu mkuu mkuu wa Ernakulam-Angamaly wa Syro-Malabars, Jimbo kuu nchini India ambapo Papa alitoa hata ujumbe kwa  njia ya video kuwataka kuondokana na migawanyiko inayotokana na mzozo juu ya mwelekeo ambao Misa inaadhimishwa na makuhani. Kardinali aliwasilisha kwa Papa barua ya kujiuzulu kwake kutoka katika utawala wa kichungaji akiwa na umri wa miaka 78;  Na alikuwa ameongoza jimbo kuu la Ernakulam-Angamaly tangu  mwaka 2011. Habari za kujiuzulu zilitolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, ambayo ilifahamisha kwamba, “kwa mujibu wa sheria, hadi kuchaguliwa kwa Askofu mkuu mpya, msimamizi wa Kanisa la Siria-Malabar atakuwa ni  Askofu Sebastian Vaniyapurackal, mwenye makao huko Troina, Katika mutadha huo Baba Mtakatifu Francisko amemtumia Barua yake Kardinali George Alencherry, Askofu Mkuu wa Ernakulam-Angamaly  ya Kanisa la  Siro-Malabar.

Katika barua hiyo Papa anaandika kuwa“Uliposherehekea mwaka jana kumbukumbu yako ya miaka hamsini ya kuwekwa wakfu na kuadhimisha miaka ishirini na tano kama Askofu, nilifurahi kuungana nawe kumshukuru Bwana, nikionesha pia shukrani zangu huduma yake uliyooneshwa katika kipindi cha miaka hiyo na juhudi na mipango mingi ya kichungaji na kielimu. Hasa, tangu 2011, mwaka wa kuchaguliwa kwako kama Baba, Mkuu wa Kanisa Kuu la Maaskofu wa  Ernakulam-Angamaly, ishara za bidii na ukarimu wako zilikuwa nyingi, kwani ulifanya bidii bila kukoma kwa mafanikio ya hatua mbali mbali muhimu katika maisha ya Kanisa hili Maalum.” Baba Mtakatifu Francisko alibainishakuwa katika suala hilo, amefikiri juu ya utambuzi wa mamlaka ya India Yote, uanzishwaji wa ofisi za Msimamizi huko Roma na uundaji wa Upatriaki  huko Australia, Canada na Uingereza.

Inatia moyo pia kwamba masharti mbalimbali ya uchungaji wa waamini katika Bara la Kiarabu unazingatiwa kwa uzito. Hayo yote wameyazingatia bila ya kudharau njia ya kawaida ya Kanisa, kwa kuzingatia pamoja na Sinodi, huduma ya kichungaji katika katekesi na liturujia, malezi ya wakleri na kwa vijana hasa waishio ughaibuni, bila kusahau kuwajali na kuwahudumia maskini na wale wanaohitaji sana. Mnamo mwaka wa 2022  Papa Francisko alibainisha kuwa yeye alishuhudia tukio lingine muhimu katika maisha ya Wakristo wa Mtakatifu Thomas na pia katika Kanisa la ulimwengu: kumbukumbu ya miaka 1,950 ya kifo cha kishahidi cha Mtume ambaye, kulingana na mapokeo, alileta tangazo la Injili nchini India. Hapo, kama mfiadini, alijifananisha kikamilifu na Bwana na Mungu wake (rej. Yh 20:28) kupitia sadaka  kuu ya maisha yake. Kwa kuongozwa na mfano huu wa Mtakatifu Thomas, na kwa sababu ya kumpenda Bwana mfufuka na Kanisa lake, mnamo mwaka wa 2019, alijitolea kujiondoa katika utawala wa kichungaji wa Kanisa pendwa la Syro-Malabar alipokabiliwa na migawanyiko na maandamano. Hata hivyo, wakati huo, Vatican ilikubali ushauri wa Sinodi ya Maaskofu ya Syro-Malabar, ambayo iliona kuwa wakati huo ulikuwa siyo muafaka. Sinodi, hata hivyo, haikukosa kutambua katika ombi lake moyo wa Mchungaji aliyeweka umoja na utume wa Kanisa juu ya kila kitu kingine.

Kwa kuwa  sasa amefikia Jubilei mbili muhimu na kutimiza malengo ya kichungaji yaliyowekwa kwa ajili ya kundi lililokabidhiwa uangalizi wake, Papa amefikiria kujiuzulu kwake sio kama hitimisho, bali ni utimilifu wa huduma yake. Hakika, hatua hii inawakilisha ushuhuda zaidi wa uaminifu kwa Injili na njia mpya ya kulitumikia Kanisa, zaidi ya yote kupitia maombi ya kutafakari na ya maombezi, pamoja na kuendelea kutoa ushauri wake kwa mabaraza ya Kipapa ta Curia Romana anaye yeye ni mshiriki.  Kwa kuzingatia mazingatio haya, pamoja na kutokea kwa miaka mia moja ya uongozi wa serikali ya Syro-Malabar, na daima Papa akikumbuka wema na umoja wa Watu wa Mwenyezi Mungu, ameamua kukubali kujiuzulu kwake kama ishara ya uwazi na unyenyekevu wako Roho Mtakatifu. Baba Mtakatfiu anaomba kwa maombezi ya Mtakatifu Thomas Mtume na kuwahakikishia maombi yake,  na anatoa baraka zake  kwao na kwa Kanisa zima  Uaskofu Mkuu wa Ernakulam-Angamaly.

11 December 2023, 12:18