Papa arudia kuwa vita ni mbaya na tusishau Palestina,Israel na Ukraine
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kuna maumivu kwa ajili ya Nchi Takatifu na kwa ajili ya Ukraine inayoteswa, na vile vile wasiwasi kwa ajili ya watoto katika vita, lakini pia kulikuwa na ukaribu na familia za waathriwa wa tetemeko la ardhi kaskazini-mashariki mwa China na mlipuko huko Conakry nchini Guinea, ambapo katika hayo amewatiamoyo kwa shirika lisilo la kiserikali la Mediterranean Saving Humans ambalo linafanya kazi nzuri kuokoa maisha ya watu wengi baharini.. Hayo yote ndiyo yalikuwa katika salamu za Papa Francisko, kwa lugha mbali mbali mara baada ya katekesi yake, Jumatano tarehe 20 Desemba 2023, kwa waamini na mahujaji waliofika katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akiwa anazungumza na wakati watu na makundi mbali mbali yaliyokuwamo kwenye ukumbi wa Pailo VI wakimpigia makofi na kwa sauti yenye kupumua kwa shida, lakini amejitahidi kwa sauti ya taadhima, amerudia kuvinyanyapalia vita na kila aina ya vita vinavyoumiza ulimwengu na vinavyozidi katika sherehe ya Noeli inayokaribia. “Tusiwasahau watu na watu wanaoteseka kwa ubaya wa vita. Vita siku zote ni kushindwa, tusisahau hili. Kushindwa…”
Wazo kwa watu walio vitani
Papa, kama katika matukio mengine mengi pia alikumbusha kuwa watu pekee wanaofaidika kutokana na migogoro ni watengenezaji wa silaha. Na baadaye aliita kwa majina nchi hizo tatu ambazo katika saa hizi, kwa miezi kama ilivyo Nchi Takatifu, kwa miaka sasa huko Ukraine, vita vimekuwa vikiharibu matumaini yote ya siku zijazo. “Tafadhali, hebu tufikirie kuhusu Palestina, kuhusu Israeli. Hebu tufikirie kuhusu Ukraine, balozi yupo hapa (Andrii Yurash). Ukraine inayoteswa, ambayo inateseka sana…”
Kuombea amani mbele ya tukio la kuzaliwa
Pia wazo la watoto vitani, likifuatiwa na mwaliko wa kwenda mbele katika Pango la kuzaliwa kuwa: "Tumwombe Yesu amani, yeye ni mkuu wa amani. Katika siku hizi, tutamwona Mungu akiwa amelala horini: ni ujumbe mzito wa Amani kwa ajili ya maisha ya kila mmoja wetu na kwa ulimwengu wa leo”, Papa alisema muda mfupi kabla katika salamu zake kwa mahujaji wa Ureno.
Kutia moyo kwa kazi ya Mediterranea Kuokoa Wanadamu
Katika salamu zake kwa lugha ya Kiitaliano, Papa Francisko aliwasalimia Umoja wa Kichungaji wa Fermo-Centro, na askofu Mkuu Rocco Pennacchio; waamini wa Alvito na wa Riardo; Uwakilishi wa Wilaya ya Bolsena, na kuwashukuru kwa zawadi ya kiutamaduni. Salamu zake kwa wazee, wagonjwa na wenye ndia wapya na vijana kwa namna ya pekee wanafunzi wa Mtakatifu Benedetto wa Tronto na wa Roccarainola-Tufino.
Amewasalimia kikosi cha kutoa msaada cha “ Mediterranea Saving Humans, ambacho ni chama cha kijamii kilichoundwa kushuhudia na kukemea kile kinachotokea katika bahari ya Mediterania na kinachofanya kazi katika Mare Nostrum- Bahari yetu kwa ajili ya kuwaokoa wahamiaji baharini. Papa alisema “ Hawa wako hapa na wanakwenda baharini kuwaokoa watu masikini wanaotoroka utumwani huko Afrika. Wanafanya kazi nzuri, wanaokoa watu wengi. Watu wengi.”Kundi hilo linliambatana na Padre Mattia Ferrari.
Tetemeko China
Ukaribu na familia za wahanga wa tetemeko la ardhi nchini China na mlipuko nchini Guinea. Baba Mtakatifu mtazamo wake umegeukua huko China ambapo Jumatatu tarehe 18 Desemba 2023, tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha 6.2 lilipiga majimbo ya Gansu na Quinghai, kaskazini-mashariki mwa nchi. Wakati idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka, tayari kuna karibu waathirwa 200 na karibu 500 waliojeruhiwa. Papa Francisko ameonesha “Ukaribu na upendo na sala kwa watu wanaoteseka: “Ninahimiza huduma za uokoaji na kuomba baraka za Mwenyezi kwa kila mtu kuleta faraja na utulivu katika maumivu.”
Mlipuko wa mafuta huko Guinea
Askofu wa Roma na Ulimwengu mzima hakuishia hapo kwani wasi wasi wake pia umeonesha ukaribu kwa familia za wahanga na majeruhi katika mlipuko uliotokea huko Conakry, mji mkuu wa Guinea, ambapo watu wanane walifariki na 84 kujeruhiwa alfajiri ya Jumatatu 18 Desemba 2023 kutokana na mlipuko huo, wa kituo kikuu cha mafuta cha Afrika Magharibi amesema “Ninaelezea ukaribu wangu kwa familia za marehemu na majeruhi. Mungu awaunge mkono na kuwapa matumaini”,
Baraka ya mpango wa Caritas nchini Poland
Na kwa kuhitimisha, aliwasalimu Wapoland, akikumbuka mpango wa Caritas unaoendelea nchini humo unaoitwa: “Msaada kwa watoto katika mkesha wa Noeli.” Ni Mpango wa upendo unaona mishumaa ya Caritas ikiwashwa kwenye meza za familia maskini zaidi na kwamba: “Ni kielelezo cha mshikamano na watoto wenye mahitaji nchini Poland na katika nchi zilizoathiriwa na umaskini” na kuongeza kuwa: “Ninawabariki kutoka ndani ya moyo wangu na ninabariki mishumaa ya Caritas!”