Papa:Leo hii kiukweli kuna hatari kubwa ya kupoteza kilicho muhimu katika maisha
Na Angella Rwezaula - Vatican
Baba Mtakatifu Francisko katika mwendelezo wake wa kateekesi kwa waamini na mauhuaji waliofika katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, Jumatano tarehe 20 Desemba 2023 ameanza kusema kuwa miaka 800 iliyopitia , mnamo Noeli ya 1223 , Mtakatifu Francis alitengeneza huko Greccio Pango hai. Wakati katika nyumba na sehemu mbali mbali wanajiandaa au wanamalizia kutengeneza pango, inakuwa vema kugundua asili yake. Je ilianzishwa namna gani pango ? Mtakatifu Francisko alikuwa na nia gani? Alikuwa anasema hivi: “Ninataka kuwakilisha Mtoto aliyezaliwa huko Betlehemu na kwa namna moja kuonja kwa macho ya mwili ugumu ambao alijikuta kwa sababu ya ukosefu wa mambo ya lazima ya mtoto, kama alivyokuwa kwenye zizi na kama alivyokuwa amelazwa juu ya majani kati ya ng’ombe na punda” (Rej.maisha ya Francis na Thomas wa Celano XXX, 84: FF 468).
Baba Mtakatifuu Francisko amesema “Nilisisitiza neno moja “mshangao.” Na hii ni muhimu. Ikiwa sisi Wakristo tunatazama tukio la kuzaliwa kwa Yesu kama kitu kizuri, kama kitu cha kihistoria, hata cha kidini, na tukaomba, hiyo haitoshi. Mbele ya kukabiliwa na Fumba la Neno Kufanyika Mwili, mbele ya kuzaliwa kwa Yesu, mtazamo huo wa kidini wa mshangao unahitajika. Ikiwa mbele ya mafumbo hayo sitafikia mshangao, imani yangu ni ya juujuu tu; imani ya kiwango cha teknolojia ya habari." "Msisahau hili.” Papa amekazia. Francis hakutaka kutengeneza kazi nzuri ya kisanaa, lakini kuibua, kupitia pango, mshangao wa unyenyekevu wa hali ya juu wa Bwana, na ugumu ambao aliteseka, kwa sababu ya upendo wetu, katika umasikini wa groto ya Bethlehemu. Kiukweli katika wasifu wa Mtakatifu wa Assisi unabainisha kuwa “Katika eneo la kushangaza liliangaza urahisi wa kiinjili, alisifu umaskini, alihimiza unyenyekevu. Yesu umekuwa kama Betlehemu ndogo”(rej 85:FF 469).
Na tabia ya Pango ilizaliwa kama shule ya kiasi cha mahitaji. Na hii ina kitu kikubwa cha kusema kwetu. Baba Mtakatifu amesema kuwa: Leo hii kiukweli, hatari ya kupoteza kile kilicho muhimu katika maisha ni kubwa na zaidi inaongezeka zaidi chini ya kivuli cha siku kuu ya Noeli: tunabadilisha mawazo ya Noeli kwa kuzama katika ulaji ambao unaharibu maana yake. Utumiaji wa Noeli. Ni kweli kwamba tunataka kutoa zawadi, ni sawa, ni njia moja, lakini shauku hiyo ya kwenda kufanya manunuzi, ambayo yanavutia watu wakati mahali pengine hakuna utulivu wa Noeli.” Baba Mtakatifu ameeleza kuwa “Tunaangalia Pango la kuzaliwa kwa Yesu kwa mshangao huo mbele ya tukio la kuzaliwa. Wakati mwingine hakuna nafasi ya ndani ya mshangao, lakini kwa kuandaa maandalizi ya siku kuu ili kufanya siku kuu. Na Pango la kuzaliwa liliundwa ili kuturudisha kwenye mambo muhimu: kwa Mungu anayekuja kuishi kati yetu. Hii ndiyo sababu ni muhimu kutazama Pango la kuzaliwa kwa Yesu, kwa sababu linatusaidia kuelewa ni nini kilicho muhimu na pia mahusiano ya kijamii ya Yesu wakati huo, familia, Yosefu na Maria, wapendwa na wachungaji.
Kwa hiyo ni Watu kabla ya mambo. Na mara nyingi tunaweka vitu mbele zaidi ya watu. Hii haifanyi kazi,” Papa ameonya. Lakini Pango la kuzaliwa la Greccio, pamoja na unyofu unaooneshwa, pia huzungumzia furaha, kwa sababu furaha ni kitu tofauti na kujifurahisha. Lakini kuwa na furaha si jambo baya ikiwa inafanywa kwenye njia nzuri; Si jambo baya, ni jambo la kibinadamu. Lakini furaha ni ya kina zaidi, zaidi ya kibinadamu. Na wakati mwingine kuna jaribu la kujifurahisha bila kuwa na furaha; kufurahiya kupiga kelele. Kidogo ni kama sura ya mcheshi, ambaye anacheka cheka na hukufanya ucheke, lwakati yeye moyo wake una huzuni. Furaha ni mzizi wa furaha nzuri wakati wa Noeli. Na juu ya furaha, habari za wakati huo zinasema: “Na siku ya furaha ilifika, wakati wa furaha! […] Francis […] aling’ara […].
Watu walikuja na kushangilia katika shangwe ambayo hawakuwahi kuionja kabla […]. Kila mmoja alirudi nyumbani kwake akiwa amejawa na furaha isiyoelezeka” (Maisha ya kwanza, XXX, 85-86: FF 469-470). Papa Francisko ameongeza kusema: “Utulivu na mshangao, huleta furaha, furaha ya kweli, na sio furaha ya bandia.” Noeli ilitoka wapi? Bila shaka, si kwa sababu ya kuleta zawadi nyumbani au kwa kuwa na sherehe za fahari zenye uzoefu. Hapana, ilikuwa ni furaha inayofurika kutoka moyoni ilipogusa kwa mikono yao wenyewe ukaribu wa Yesu, huruma ya Mungu, ambaye hakuachi peke yako, bali anakufariji. Ukaribu, upole na huruma, ndizo tabia tatu za Mungu. Na tukitazama eneo la kuzaliwa kwa Yesu, tukiomba mbele ya Pango la kuzaliwa, tutaweza kuhisi mambo haya ya Bwana ambayo yanatusaidia katika maisha ya kila siku.
Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa “tukio la kuzaliwa kwa Yesu ni kama kisima kidogo ambacho unaweza kuchota ukaribu wa Mungu, chanzo cha tumaini na furaha. Pango la kuzaliwa kwa Yesu ni kama Injili iliyo hai, Injili ya nyumbani. Ni kama kisima katika Biblia, ni mahali pa kukutania, ambapo unaweza kumletea Yesu matarajio na mahangaiko ya maisha kama wachungaji wa Bethlehemu na watu wa Greccio walivyofanya, kwa kumpelekea matarajio na mahangaiko ya maisha kwa Yesu. Ikiwa mbele Pango la kuzaliwa kwa Yesu tunamkabidhi Yesu kile ambacho kipo moyoni mwetu, sisi pia tutapata furaha kuu (Mt 2:10), furaha inayokuja hasa kutokana na kutafakari, kutoka katika roho ya mshangao ambayo ninakwenda kutafakari mafumbo hayo. Twende mbele ya Pango la kuzaliwa. Kila mtu atazame na kuruhusu moyo uhisi kitu.” Amehitimisha.