Tafuta

2023.12.23 Kardinali Thomas Stafford Williams, Askofu Mstaafu wa  Wellington, New Zealand. 2023.12.23 Kardinali Thomas Stafford Williams, Askofu Mstaafu wa Wellington, New Zealand. 

Papa amkumbuka Kardinali Williams kwa mchango mkubwa kwa Kanisa la New Zealand

Askofu mkuu mstaafu wa Wellington,aliaga dunia tarehe 22 Desemba akiwa na umri wa miaka 93.Katika telegramu,Baba Mtakatifu Francisko anatoa shukrani kwa huduma yake kwa Kanisa huko New Zealand.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu ameonesha uchungu na kutoa rambi rambi kufuatia na  na kifo cha Kardinali Thomas Stafford Williams, aliyekuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa Wellington, New Zealand, kilichotolea tarehe 22 Desemba 2023. Hisia hizo zimeonesha kwenye telegramu aliyomwandikia Askofu Mkuu  Paul Martin, wa Jimbo Kuu la Wellington, ambapo Baba Mtakatifu anatuma salamu za rambirambi kwa mapadre wote, watawa na waamini walei, akikumbuka kwa shukrani nyingi miaka mingi ya huduma ya kikuhani na kiaskofu ya marehemu Kardinali, kati ya kundi la Kristo huko New Zealand na mchango wake kwa Kanisa lote la bara la Bahari. Kwa njia  hiyo  Baba Mtakatifu Francisko anampongeza Kardinali kwa upendo na huruma ya Mungu, na  ametoa baraka zake kwa wale wote wanaoomboleza kwa kifo cha Kardinali Williams.

Kardinali alikuwa na miaka 93

Kardinali Williams alifariki alfajiri ya tarehe 22 Desemba 2023 huko Waikanae, katika nyumba ya kustaafu iitwayo Charles Fleming, alikokuwa akiishi. Hali yake ya afya ilikuwa mbaya zaidi katika siku za hivi karibuni. Alikuwa na umri wa miaka 93. Alizaliwa tarehe 20 Machi 1930 huko Wellington, aliipewa daraja la Upadre mnamo  tarehe 20 Desemba 1959. Aliteuliwa kuwa Askofu  wa Wellington tarehe 30 Oktoba 1979, na kuwekwa wakfu wa kiaskofu tarehe 20 Desemba mwaka huo huo. Kuanzia 1 Juni 1995 hadi 1 Aprili 2005 pia alikuwa pia Msimamizi wa Shirika la Kijeshi la Kawaida la New Zealand. Alichaguliwa katika Baraza la Makardinali mnamo tarege  2 Februari 1983 na kupewa Kanisa la Gesù Divin Maestro huko Pineta Sacchetti Roma. Tarehe 21 Machi 2005 alihitimisha muda wake wa kichungaji wa jimbo kuu kufuatia na umri

Maisha yake ya kujitolea, kwa mtindo wa kiasi, kwa uchungaji huko Wellington, kwanza kama Padre na baadaye kama Askofu na Kardinali, na muda kama mmisionari wa fidei donum huko Samoa. Wasifu wa Kardinali ambaye, mwaka 1998, pia alikuwa ametekeleza jukumu nyeti la kuwa Mjumbe Maalum wa Sinodi ya Maaskofu, wa  bara  la visiwa vya Australia ambalo alikuwa na maono yenye uwezo wa kuelewa mambo yote tofauti katika uhalisia kikanisa na ushirika. Alikuwa ameomba kukumbukwa kama mtumishi aliyejitolea na kwamba sifa yake ipunguzwe hadi maneno manane tu: “Alikuwa mwenye dhambi. Tafadhali mwombee."

Papa atuma rambi rambi kwa kifo cha Kardinali Thomas Stafford Williams
23 December 2023, 17:40