Papa:Familia Takatifu ni mtaalamu wa mateso,inayotueleza mko pamoja nasi katika shida
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika Dominika ya Kwanza baada ya Noeli, tarehe 31 Desemba 2023 Mama Kanisa alikuwa anaadhimisha Siku kuu ya Familia Takatifu. Kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu Francisko alitoa tafakari yake. Akianza alisema: “Leo tunaadhimisha siku kuu ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu. Injili inatuonesha Hekalu la Yerusalemu, kwa kuwakilisha Mtoto kwa Bwana, (Lk 2,22-40). Na familia ilifika katika hekalu na hali yake katika kupeleka zawadi ya kutoa nyenyekevu na rahisi kati ya zile zilizotarajiwa kwa kushuhudia umasikini wake. Ni Maskini.” Baba Mtakatifu aliendelea kufafanua kuwa”: Hatimaye, Maria alipokea unabii kwamba: “Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako.”(Lk 2,45). Walifika katika umaskini na wanarudi wakiwa na mzigo wa mateso. Kile ambacho kinashangaza: kama Familia ya Yesu ni moja ya famili katika historia ambayo inaweza kujivunia kwake uwepo wa Mungu wa nyama na mfupa, na badala ya kuwa tajiri ni masikini. Badala ya kuwezeshwa, inaonekana kuzuiwa! Badala ya kuwa huru kutokana na uchovu, inatumbukizwa katika maumivu makali.”
Baba Mtakatifu Francisko ameuliza, “Je, hii inazungumzia nini kwa familia zetu, kwa njia hii ya kuishi historia ya Familia Takatifu, maskini, iliyozuiliwa, kwa maumivu makali? Jimbi : “Jambo zuri sana, inatuambia jambo zuri sana: Mungu, ambaye mara nyingi tunafikiri kwamba hana matatizo, amekuja kukaa maishani mwetu na matatizo yake. Alituokoa hivi (taz Yn 1:14): hakuja akiwa mtu mzima, lakini akiwa mtoto mdogo sana aliishi katika familia, mtoto wa mama na baba; alitumia muda mwingi huko, kukua, kujifunza, katika maisha ya kila siku, kujificha na kimya.” Baba Mtakatifu ameongeza kusema: “ Na hakuzuia shida, badala yake kwa kuchagua familia yaani familia moja “mtaalamu wa mateso” anaelezea familia zetu kuwa: “Ikiwa unajikuta katika shida, ninajua uzoefu mnaofanya, maana mimi, mama na baba yangu tulijaribiwa kwa kuweza kuwambia kuwa hata familia zenu, ninyi hampo peke yenu!” Papa amesisitiza kuwa: Yosefu na Maria “walishangazwa na mambo yaliyosemwa juu ya Yesu” (taz. Luka 2:33 ), kwa sababu hawakufikiri kwamba mzee Simeoni na nabii Ana wanegweza kusema mambo hayo na walishangaa.”
Kwa njia hiyo Papa ametaka kusisitiza hilo juu ya “uwezo wa mshangao.” Kwamba Uwezo wa mshangao ni siri ya kusonga mbele vizuri katika familia. Kutozoea kawaida ya mambo, kwanza kujua jinsi ya kushangazwa na Mungu, ambaye anatusindikiza. Na kisha, kwa kushangaa katika familia. Papa amefikiria kuwa ni vyema kwa wanandoa kuwa katika ndoa, kwanza kwa kujua jinsi ya kushangazwa na mwenzi wako, kwa mfano kwa kumshika mkono na kumwangalia machoni mwake kwa dakika chache jioni, kwa huruma: mshangao hukuongoza katika upole, daima”. Kwa hiyo “ Upole katika ndoa, katika wanandoa? ni mzuri.” Na kisha kushanga muujiza wa maisha, wa watoto, na kupata wakati wa kucheza nao na kuwasikiliza. Papa ameuliza swali “Ninakuuliza, baba na mama: unapata muda wa kucheza na watoto wako? Kuwapeleka katika matembezi? Jana nilizungumza na mtu kwenye simu na nikamuuliza je: “Uko wapi?” – akajibu “Eh, niko uwanjani, niliwapeleka watoto wangu matembezini”.
Kwa kuongezea Baba Mtakatifu amesisitiza: “Huu ndio ubaba na umama mzuri. Na kisha, kushangaa kwa hekima ya babu na bibi: mara nyingi, tunawaondoa babu na babi zetu kutoka katika maisha yao. Na kumbe hapana: babu na bibi ni vyanzo vya hekima. Tujifunze kushangazwa na busara za babu na bibi zetu, na kwa historia zao. Babu na bibi huturudishia maisha muhimu. Na kushangazwa, hatimaye,na historia yetu ya upendo - kila mmoja wetu ana yake mwenyewe na Bwana alitufanya tutembee kwa upendo: kwa kushangazwa na hili. Na pia, maisha yetu hakika yana mambo mabaya, lakini pia tunashangazwa na wema wa Mungu katika kutembea nasi, hata kama hatuna uzoefu. Maria, Malkia wa familia, utusaidie kustaajabu: leo tuombe neema ya mshangao; Mama Yetu atusaidie kushangazwa kila siku na mema na kujua jinsi ya kuwafundisha wengine uzuri wa mshangao.” Papa amehihitimisha.