2023.12.18 Papa akutana na wawakilishi wa Hospitali "Miulli" ya Acquaviva delle Fonti (Bari),Italia. 2023.12.18 Papa akutana na wawakilishi wa Hospitali "Miulli" ya Acquaviva delle Fonti (Bari),Italia.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa,Hospitali Miulli:Kumweka mtu katikati na kukuza utafiti wa kisayansi

Kumweka mtu katikati na kukuza utafiti wa kisayansi ni vipengele viwili ambavyo Papa amefafanua kwa wawakilishi wa Hospitali ya Francesco Miulli wa Bari Nchini Italia aliokutana nao tarehe 18 Desemba 2023.“Uhamiaji ni tatizo linalofanya maeneo kuwa maskini na tunafahamu kwa hakika,inawezekana kuhimiza wataalamu wengine wa ngazi ya juu kuja na kufanya kazi nchini Italia,katika kubadilishana ujuzi juu ya upeo mpana.”

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko,Jumatatu tarehe 18 Desemba 2023, amekutana na wawakilishi wa Hospitali ya “Francesco Miulli” ya huko  Acquaviva delle Fonti, Bari nchini Italia,  ambapo katika hotuba yake amewashukuru kumtembelea na kwamba wamememrusu kukutana na Jumuiya hiyo.  Ni Muhimi li wa Kikanisa, na hiyo inatia changamoto zaidi wajibu wetu kama Kanisa. Kwa hakika, ni mahali panapochanganya msukumo wa Kikristo na taaluma na uvumbuzi wa kimatibabu na kiteknolojia.  Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko amependa kuzingatia vipengele viwili muhimu vya kazi yao. Cha kwanza kabisa ni kumweka mtu katikati na kukuza utafiti wa kisayansi.  Akianza na na kumweka mtu katikati.  Baba Mtakatifu amebainisha kuwa Hospitali yao “ni ya kale iliyoanzishwa karne tisa zilizopita, kama hospitali ya wagonjwa maskini, yaani, kama mahali pa kukaribisha na salama ambapo wale wanaoteseka wanaweza kupata kimbilio na msaada. Na pia wanajaribu kuwa waaminifu kwa dhamira ya wale waliowatangulia, wakiendelea kuwaweka maskini wagonjwa katikati ya kazi yao, na ndani yao Yesu, ambaye alituambia kuwa: “Kila kitu mlichomtendea  mmoja tu wa watu  hawa Ndugu zangu, mlinitendea mimi” (taz. Mt 25:40).

Wawakilishi wa Hospitali F. Miulli ya Acquaviba delle Fonti wakutana na Papa
Wawakilishi wa Hospitali F. Miulli ya Acquaviba delle Fonti wakutana na Papa

Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa hiyo imewafanya kuwa ukweli unaoendelea na wanaoendelea kukua, kama walivyothibitishwa na jinsi wanavyosasisha mara kwa mara matibabu na miundo, ili kutoa huduma kamili zaidi kwa wagonjwa. Kiukweli, eneo jipya la hospitali linawawezesha kutoa wagonjwa zaidi ya vitanda 600, na vyumba vya uendeshaji na vitengo vya matibabu, ambapo wafanyakazi zaidi ya elfu hufanya kazi kwa taaluma na kujitolea. Baba Mtakatifu amefurahishwa na  ufunguzi, ndani ya muundo, wa kliniki ya wahamiaji -iliyoundwa kwa ushirikiano na Caritas kijimbo - ambayo inatumia huduma za hiari za wafanyakazi wote wa matibabu na wauguzi. Hii ni nzuri sana, na inashuhudia roho ambayo wanatekeleza huduma yao. Pamoja na haya yote, inaweza kusemwa kwamba “Miulli” ni rasilimali ya thamani kwa eneo lake na pia katika ngazi ya kitaifa.

Wawakilishi wa Hopitali F.Miulli
Wawakilishi wa Hopitali F.Miulli

Papa ameendelea  kufafanua katika hatua ya pili ambayo ni kukuza utafiti wa kisayansi alisema tayari wao wamejishughulisha na hilo kwa miongo kadhaa, kwa ushirikiano na vyuo vikuu vingi vya Italia. Kwa miaka miwili, hata hivyo, kwa idhini ya Wizara ya Vyuo Vikuu na Utafiti, “Miulli” imekuwa Chuo Kikuu cha Matibabu na kimewezesha Kozi ya Shahada ya Uzamili ya Mzunguko Mmoja katika Tiba na Upasuaji. Hili ni dhumuni la thamani kubwa, ambalo kwa upande mmoja huruhusu wafanyakazi wa afya waliopo kutekeleza huduma inayotambulika katika nyanja za kitaaluma na afya katika eneo lao, na kwa upande mwingine pia huwapa akili bora zaidi ya eneo hilo fursa ya hama: Uhamiaji ni tatizo linalofanya maeneo kuwa maskini, na tunafahamu; kwa hakika, inawezekana kuhimiza wataalamu wengine wa ngazi ya juu kuja na kufanya kazi nchini Italia, katika kubadilishana ujuzi juu ya upeo mpana. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa Hospitali ya “Francesco Miulli” inaweza kukuza mzunguko mzuri kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa ajili ya manufaa ya jamii na wagonjwa, wakati huo huo kujali ubora wa huduma na tahadhari kwa watu. Amewashukuru kwa kile wanachofanya na kuwahimiza waendelee na njia hiyo kwa shauku. Amewabariki kwa moyo wote wao na kazi yao na kuwatakia Noeli njema! Na ikiwapendeza wasisahau kumuombea, Baba Mtakatifu amehitimisha.

Hotuba ya Papa kwa Wawakilishi wa Hospitali FR Miulli
18 December 2023, 15:44