Papa:Jeshi la anga ni mlinzi wa maisha,haki na amani
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Wakati ambapo migogoro ya kutisha inatesa ubinadamu, kulinda ni hakikisho la dhamira ya jeshi ambalo daima linalenga kutetea uhai, haki na amani. Baba MtakatifuFrancisko, amesema hayo Jumamosi tarehe 9 Desemba 2023, wakati wa kukutana na Kikundi cha Wanaeshi Anga wa Italia wakifuatana na Mkuu wa Majeshi na Mapadre watoa huduma kwenye vikanisa vyao. Katika hotuba yake Papa Francisko ameakisi jukumu muhimu la huduma ya Jeshi la Anga, katika fursa ya maadhimisho ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo, ambapo alisema ni historia inayoweza kusomwa kutoka katika mitazamo tofauti, kwa kuanzia na ile ya maendeleo ya kisayansi ambayo, pamoja na mageuzi yake, imeashiria ulimwengu wa kuruka na kwamba hakuna mgeni katika shida na mitego.
Utafiti, uvumbuzi na teknolojia mpya Papa amekazia kusema hazipaswi kamwe kuwa chini ya maslahi ya mamlaka au matumizi mabaya, lakini ni lazima na daima zielekezwe kwenye manufaa fungamani ya mwanadamu, yaani kwa ajili ya maendeleo ya watu wote, na haki zaidi. Katika njia hii yao ni na itabaki kuwa huduma ya thamani kwa ajili ya amani, alisisitiza Baba Mtakatifu. Na kwa hiyo Mageuzi hayo, alibainisha, pia kuwa yameashiria huduma ya kijeshi, ambayo ilionekana kuwa muhimu zaidi ya yote wakati wa kutisha wa vita hadi kuwa muhimu leo hii katika mazingira mengine mengi, kuanzia na usalama wa ndege hadi uokoaji, ushirikiano na mashirika ya kimataifa ya utume wa misaada ya kibinadamu na amani hasi kufikia usimamizi wa majanga makubwa ya asili na pia kwa ajili ya nchi zisizo na vifaa na idadi ya watu wasiojiweza.
Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake alisema: “Ninafikiria pia mchango wenu katika dharura za kiafya, kama vile janga la Uviko-19, ambalo limewafanya wajitolee kufanya kazi katika hospitali, ili kusaidia kampeni ya chanjo na kuhakikisha usafiri wa anga wa wagonjwa.” Mbali na ile ya Uviko -19 na dharura zingine za kiafya, alifikiria mwenendo wa kiraia katika hali ngumu, nje ya nchi au mamlaka, kuwa ni ahadi ambayo tunaelewa kwa kina cha huduma yao kwa nchi, iliyopanuliwa kwa ajili ya wanadamu ambao ni familia. Na kwa hakika ile ya kibinadamu ndio mtazamo wa mwisho ambao Baba Mtakatifu Fransisko alizungumzia kuwa askari wanaotetea, wanaokaribisha, kusaidia na kuwahudumia watu pia shukrani kwa msaada wa mapadre. Wakati huo huo, wanatoa mafunzo, wadumisha utambulisho wa watumishi wa Serikali na wananchi.
Kwa kuhitimisha Papa Francisko aliwasifu kwa shauku, ya kujitolea, ujasiri na motisha, na uwezo wa kuwa tayari kulipa gharama wao binafsi ya maisha kama ilivyokuwa, kwa mfano, kwa askari kumi na tatu wa Italia waliouawa Kindu, nchini Congo, wakiwa wanasafiri kutoa misaada ya kibinadamu chini ya Kofia ya Umoja wa Mataifa. “Katika wakati huu, ambapo ubinadamu unateswa na migogoro ya kutisha, ulinzi wa utajiri huu wa kibinadamu unawakilisha dhamana bora ya ukweli kwamba kujitolea kwenu daima kunaelekezwa kwenye ulinzi wa maisha, haki na amani. Kwa haya yote ninawakabidhi ninyi, familia zenu na huduma yenu kwa Mlinzi wa mbinguni, Maria wa Loreto, ambaye kumbukumbu yake ya kiliturujia itafanyika kesho.”