Basilika ya Bikira Maria wa Machozi aliyetokea miaka 70 iliyopita huko Siracusa,kusini mwa Italia. Basilika ya Bikira Maria wa Machozi aliyetokea miaka 70 iliyopita huko Siracusa,kusini mwa Italia. 

Papa kwa kanisa la Siracausa:Je wanadamu wataelewa lugha ya ajabu ya machozi hayo?

Papa alituma barua kwa Askofu Mkuu wa Siracusa katika maandhimisho ya Miaka 70 ya tokeo la Mama wa machozi.Katika ujumbe:Machozi yalitokea katika mazingira hatarishi ya Vita vya II vya Kidunia,katika nyumba ya kawaida ya kijiji.Mchanganyiko wa hali hizi unakumbusha upendo wa upendeleo wa Bwana,mpenda maisha,maskini na wahitaji.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 7 Desemba 2023 katika mkesha wa Masifu ya Kwanza ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, alimtumia Barua Askofu Mkuu Francesco Lomanto wa Jimbo Kuu Katoliki la Siracusa Italia, katika fursa ya Miaka 70 ya Mama Yetu wa Machozi huko Siracusa. Katika Barua hiyo Baba Mtakatifu anabanisha kwamba, “Miaka sabini imepita tangu machozi ya Mama yalipomwagika kwa upole kwenye ardhi ya Siracusa: kati ya 29 Agosti na 1 Septemba 1953, kutoka katika macho ya Bikira, aliyooneshwa na Moyo Safi kwenye mchoro uliowekwa kando ya kitanda cha wenza wa ndoa yalitiririka kiukweli machozi ya binadamu. Tangu wakati huo Kanisa la Siracusa limelinda kwa uangalifu na kwa utauwa machozi haya, ambayo mara nyingi huwafikia wagonjwa, wazee, wanaoteseka na jumuiya za kikanisa katika sehemu mbalimbali za dunia, ikiwa ni ishara ya uwepo wa karibu na wa dhati wa Mama wa Mungu na  mama yetu. 

Maria yanonesha ushiriki wa upendo wa huruma wa Bwana

Machozi ya Maria yanaonesha kushiriki kwake katika upendo wa huruma wa Bwana, anayeteseka kwa ajili yetu sisi watoto wake; ambaye anatumaini kwa bidii uongofu wetu; ambaye anatungoja, kama Baba mwenye huruma, atusamehe kila kitu na siku zote. Kwetu sisi, hata hivyo, swali la Mtumishi wa Mungu Papa Pio XII linafanywa upya: "Je, wanadamu wataelewa lugha ya ajabu ya machozi hayo?” (Ujumbe wa radio, 14 Oktoba 1954). Ili kukaribisha wito wake wa kinabii, Kanisa la Sirausa linaadhimisha Mwaka wa Maria: Kwa njia hiyo Papa ameongeza kusema kuwa: “Ninapenda kuelezea ukaribu wangu kwa jumuiya ya jimbo, nikiungana kiroho na kutoa salamu za dhati kwako, kwa Mapadre, kwa watu waliowekwa wakfu na waaminifu wote.”

Tukio la ajabu lilitokea katika faragha

Machozi yalitokea, katika mazingira hatarishi ya Vita vya Kidunia vya pili, katika nyumba ya kawaida ya kijiji ambapo familia ya wanyenyekevu, ya Angelo Iannuso na Antonina Giusto waliishi, wakitarajia mtoto wao wa kwanza. Mchanganyiko wa hali hizi unakumbuka upendo wa upendeleo wa Bwana, mpenda maisha, kwa maskini na wahitaji: Kanisa, ambalo ni Bibi-arusi wake, haliwezi kujizuia kukubaliana na upendeleo huu. Zaidi ya hayo, tukio la kustaajabisha, lililotokea katika faragha ya nyumba, linatualika kufikiria uzuri wa ajabu wa makao ya nyumbani, kituo cha upendo na maisha,na kuunga mkono familia iliyoanzishwa juu ya ndoa, ikionesha thamani yake ya ndani kama kiini msingi wa jamii na wa Kanisa.

Machozi ya Mama kama hayo hata leo hii inaendelea kumwagika

Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa hata hivyo machozi ya Mama huyo yanaendelea kumwagika wakati walio dhaifu zaidi wanabaguliwa na vurugu na vita vinapoenea, kushindwa kunakodai waathiriwa wasio na hatia. Kwa kukabiliwa na majaribu ya maisha na historia, hasa katika hali ya vita vya siku hizi vinavyotia wasiwasi, tusichoke kuomba maombezi ya Maria, Malkia wa Amani na Mama wa faraja. Wasiwasi wake wa kimama uwahimize waamini kujenga na kufuata njia za amani na msamaha na kuwa karibu na wagonjwa wa mwili na roho na wale walio peke yao na walioachwa. Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema inafariji kujua kwamba Mama wa Mungu, aliyeitwa kwa jina la "Mama yetu wa Machozi", amewapa neema nyingi wale waliomgeukia.”

Maadhimisho yaidhinishe neema kuu katika Kanisa la Siracusa

Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa maadhimisho haya muhimu yaidhinishe neema kuu katika Kanisa zima la Siracusa, nia ya kufananisha maisha ya mtu zaidi na Yule ambaye Maria anatuonesha, Bwana Yesu Kristo, ili imani ihuishwe, upendo utekelezwe, imani ishuhudie na kuamsha matumaini. Mama yetu awaunge mkono, na  ambaye pamoja nanyi ninamsihi: Ee Bikira Maria, Sindikiza njia ya Kanisa na zawadi ya machozi yako matakatifu, ulete amani ulimwenguni pote na uwalinde watoto wako kwa ulinzi wako wa uzazi. Utusaidie katika uaminifu kwa Mungu, katika huduma kwa Kanisa na kwa upendo kwa ndugu zetu wote. Amina.” Kwa kuhimitimisha Papa ameandika kuwa “Wakati ninawaomba mniombee, kwa moyo wote naintuma Baraka yangu, ninayowapatia wale watakaoshiriki katika sherehe hizo kuu za ukumbusho.”

Barua ya Papa kwa waamini wa Siracusa wakiadhimisha Miaka 70 ya kutokea kwa machozi
11 December 2023, 11:29