Tafuta

2023.12.21  Matashi mema ya Heri za Noeili kwa Curia Romana. 2023.12.21 Matashi mema ya Heri za Noeili kwa Curia Romana.  (Vatican Media)

Noeli 2023,Papa kwa Sekretarieti Kuu ya Vatican:kusikiliza,kutambua na utembea

Kusikiliza kama Maria kwa magoti,kufanya utambuzi kama Yohane Mbatizaji na kuacha nafasi kwa Mungu zaidi ya hukumu na kutembea kama Mamajusi bila kupotea kwenye mawimbi ya ugumu na unyenyekevu.Ndiyo kiini cha hotuba ya Papa wakati wa kukutana na Makardinali,Maaskofu pamoja na Familia ya Sekretarieti kuu ya Vatican kutakiana heri za kiutamaduni za Noeli 2023.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Awali ya yote ninataka kumshukuru Kardinali Re kwa maneno yake na  hata nguvu alizo nazo kwa miaka 90 na endelea mbele kwa neema,  Asante. Fumbo la Noeli huamsha mioyo yetu kwa mshangao, neno muhimu, mshangao wa tangazo lisilotarajiwa: Mungu anakuja, Mungu yuko hapa kati yetu na nuru yake imepenya giza la ulimwengu milele. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 21 Desemba 2023 ameanza kusema katika hotuba yake wakati wa kukutana na Makardinali, Maaskofu pamoja na Familia ya Sekretarieti kuu ya Vatican, kama sehemu ya utamaduni wa kutakiana heri na baraka za Sherehe za Noeli kwa mwaka 2023. Baba Mtakatifu katika hotuba yake, amesema kuwa  tunahitaji kusikiliza na kupokea tangazo hili kila wakati, hasa katika wakati ambao bado unaoneshwa kwa majonzi na vurugu za vita, na hatari za milele ambazo tunaoneshwa kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi, umaskini, mateso, njaa  na kukazia kuwa kuna njaa ulimwenguni   na kwa majeraha mengine ambayo hukaa katika historia yetu. Inafariji kugundua kwamba hata katika "mahali" ambapo uchungu huu upo  kama vile katika nafasi zote za ubinadamu wetu dhaifu, Mungu anajifanya kuwepo katika utoto huu, katika hori ambalo leo hii anachagua kuzaliwa na kuleta upendo wa Baba kwa kila mtu; na anaufanya kwa mtindo wa Mungu: ukaribu, huruma, na upole. Huu ndio mtindo wa Mungu: wa ukaribu, huruma na upole, Papa amekazi tena.

Hotuba ya Papa kwa Curia Romana
Hotuba ya Papa kwa Curia Romana

Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa, tunahitaji kusikiliza tangazo la Mungu ajaye, kuzitambua ishara za uwepo wake na kuamua Neno lake kwa kutembea nyuma  yake. Kusikiliza, kutambua, kutembea: ndiyo maneno matatu kwa ajili ya safari yetu ya imani na kwa huduma tunayofanya hapa Curia. Kutokana na hiyo Papa Francisko amependa kufafanua kupitia baadhi ya wahusika wakuu wa Noeli Takatifu. Kwanza kabisa Maria, ambaye anatukumbusha kusikiliza. Msichana wa Nazareti, aliyekuja kuukumbatia ulimwengu ni Bikira wa kusikiliza kwa sababu alisikiliza tangazo la Malaika na kuufungua moyo wake kwa mpango wa Mungu. Anatukumbusha kuwa amri kuu ya kwanza ni: “Sikiliza Israeli” (Kum 6:4), kwa sababu kabla ya agizo lolote ni muhimu kuingia katika uhusiano na Mungu, tukiikaribisha zawadi ya upendo wake inayokuja kwetu. Kusikiliza, kiukweli, ni neno la  kibiblia ambalo sio tu linarejea kusikia, lakini linamaanisha kuhusika wa moyo na kwa hivyo maisha yenyewe. Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa Mtakatifu Benedikto alianza Kanuni yake:  kuwa “Sikiliza kwa makini, oh mwanangu [...] (Kanuni, Dibaji, 1). Kusikiliza kwa moyo wako ni zaidi ya kusikia ujumbe au kubadilishana habari; ni usikilizaji wa ndani wenye uwezo wa kukatiza matamanio na mahitaji ya wengine, uhusiano ambao hutualika sisi kushinda mifumo na kushinda chuki ambayo wakati mwingine tunaingilia maisha ya wale wanaotuzunguka.

Kusikiliza daima ni mwanzo wa safari. Bwana anawaomba watu wake usikivu huu wa moyo, uhusiano naye, ambaye ni Mungu aliye hai. Na hii ni kumsikiliza Bikira Maria, ambaye anapokea tangazo la Malaika kwa uwazi, uwazi kabisa, na kwa sababu hiyo hafichi usumbufu na maswali ambayo yanayoletwa ndani yake; lakini anajihusisha kwa hiari katika uhusiano na Mungu ambaye amemchagua, akiukaribisha mpango wake. Kuna mazungumzo na kuna utii. Maria alielewa kwamba yeye ndiye mpokeaji wa zawadi isiyo na thamani na, kwa kupiga magoti yake, yaani, kwa unyenyekevu na mshangao, alisikiliza. Baba Mtakatifu amekazia kuwa “Kusikiliza kwa kupiga magoti ni njia bora ya kusikiliza kweli, kwa sababu ina maana kwamba sisi si juu  ya mwingine katika nafasi ya mtu ambaye anadhani kuwa tayari kujua kila kitu, ya mtu ambaye tayari kutafsiri mambo kabla hata kusikiliza, ya mtu anayetazama chini kutokea juu lakini, kinyume chake, tunajifungua kwa fumbo la mwingine, tayari kupokea kwa unyenyekevu chochote anachotaka kutupatia. Kwa njia hiyo Papa amesisitiza kuwa: “Na tusisahau kwamba katika tukio moja tu linaruhusiwa  kumtazama mtu kwa juu hadi chini  hasa ni  kwa kuinama kumsaidia,  ndiyo tukio pekee ambalo unarusiwa kutamza mtu kunzia chini hadi juu.

Papa akutana na Curia Romana katika heri za Noeli 2023
Papa akutana na Curia Romana katika heri za Noeli 2023

 

Baba Mtakatifu ametoa onyo kuwa “Wakati mwingine, hata katika mawasiliano kati yetu, tunahatarisha kuwa kama mbwa mwitu wawindaji: mara moja tunajaribu kumeza maneno ya mtu mwingine, bila kuwasikiliza kabisa, na mara moja tunamwaga maoni yetu na hukumu zetu juu yao. Badala yake, kusikiliza kila mmoja kunahitaji ukimya wa ndani, lakini pia kutoa nafasi ya ukimya kati ya kusikiliza na kujibu. Sio mchezo wa ping pong,  bali kutoa nafasi ya kusikiliza, kuelewa, kati ya kusikiliza na kujibu.” Kwa kukazia zaidi Papa amesema: “Kwanza tunasikiliza, kisha kwa ukimya tunakaribisha, tunatafakari, tunatafsiri na baadaye tu, tunaweza kutoa jibu. Tunajifunza haya yote kupitia maombi, kwa sababu yanapanua moyo, yanafanya ushuke ubinafsi wetu kutoka kwenye msingi wake, hutufundisha kuwasikiliza wengine na kuzalisha ndani mwetu ule ukimya wa kutafakari. Tunajifunza kutafakari kupitia  maombi, kwa kupiga magoti mbele ya Bwana, lakini si tu kwa miguu yetu, bali  kupiga magoti kwa mioyo yetu! Hata katika kazi yetu kama Curia, “tunahitaji kusihi kila siku, kuomba neema yake kufungua mioyo yetu baridi na kutikisa maisha yetu vuguvugu na ya kijuujuu. […] Ni haraka kurejesha roho ya kutafakari, ambayo huturuhusu kugundua tena kila siku kwamba sisi ni walinzi wa wema ambao unafanya ubinadamu, ambao hutusaidia kuishi maisha mapya. Hakuna kitu kilicho bora kuwapitishia wengine" (Evangelii gaudium, 264).

Katika hotuba hiyo Baba Mtakatifu ameendelea kukazia kuwa kkwa Sekretarieti ya Vatican kuwa  kuna haja ya kujifunza ustadi wa kusikiliza. Kabla ya majukumu yetu ya kila siku na shughuli zetu, hasa kabla ya majukumu tunayojikita nayo, tunahitaji kugundua tena thamani ya mahusiano, na kujaribu kuyavua taratibu, ili kuyahuisha kwa roho ya kiinjili zaidi ya yote kwa kusikilizana. Kwa moyo wangu na kwa magoti yangu. Tusikilizane zaidi, bila chuki, kwa uwazi na kiasi,  huku moyo wangu ukiwa umepiga magoti. Hebu tusikilize kila mmoja, akijaribu kuelewa vizuri kile ambacho ndugu  anasema, kufahamu mahitaji yake na kwa namna fulani maisha yake mwenyewe, ambayo yanajificha nyuma ya maneno hayo, bila kuhukumu. Kama vile Mtakatifu Ignatius anavyoshauri kwa hekima: “Lazima ichukuliwe kwamba Mkristo mwema lazima awe na mwelekeo wa kutetea badala ya kulaani uthibitisho wa mwingine.” Ikiwa huwezi kutetea, jaribu kufafanua ni kwa maana gani mtu mwingine anaelewa; ikiwa anaelewa vibaya, mrekebishe kwa upole; kama hii haitoshi, tumia njia zote zinazofaa kuielewa kwa usahihi na hivyo kujiokoa” (Mazoezi ya Kiroho, 22). Yote ni kazi kuelewa mwingine vizuri. Na ninarudia: kusikiliza ni tofauti na kusikia. Kutembea katika mitaa ya miji yetu tunaweza kusikia sauti na kelele nyingi, lakini kwa ujumla hatuzisikilizi, hatuziweka ndani na hazibaki ndani yetu. Jambo moja  la kusikiliza kwa urahisi, ni jambo lingine kusikia, ambalo pia linamaanisha "kukaribisha ndani.”

Viongozi wa Curia Romana wakisikiliza hotuba ya Papa
Viongozi wa Curia Romana wakisikiliza hotuba ya Papa

Kusikiliza pamoja hutusaidia kupata utambuzi kama njia ya utendaji wetu. Na hapa tunaweza kurejea Yohane Mbatizaji. Kwanza Madonna anayesikiliza, sasa ni Yohane ambaye anafanya utambuzi. Tunajua ukuu wa nabii huyo, ukali na unyeti wa mahubiri yake. Hata hivyo, Yesu anapofika na kuanza huduma yake, Yohane alipitia msukosuko mkubwa wa imani; alikuwa ametangaza ujio wa Bwana unaokaribia kama ule wa Mungu mwenye nguvu, ambaye hatimaye angewahukumu wenye dhambi kwa kutupa kila mti usiozaa matunda katika moto na kuchoma majani kwa moto usiozimika Taz. Mt 3:10-12).  Lakini sura hii ya Masiha inasambaratika mbele ya ishara, maneno na mtindo wa Yesu, mbele ya huruma na rehema anazoonyesha kwa kila mtu. Ndipo Mbatizaji alihisi hana budi kufanya utambuzi ili kupokea mweleke mapya. Kiukweli, Injili inatuambia hivi: “Yohane, aliyekuwa gerezani, aliposikia juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kwa wanafunzi wake kumwambia: Je! wewe ndiwe yule ajaye, au tumngoje mwingine? ( Taz. Mt 11,2-3). Kwa ufupi, Yesu hakuwa kama alivyotarajiwa na kwa hiyo hata Mtangulizi lazima aongoke kwa upya wa Ufalme, na lazima awe na unyenyekevu na ujasiri wa kufanya utambuzi.

Baba Mtakatifu Francisko amesema  kuwa “utambuzi ni muhimu kwa sisi sote, sanaa hii ya maisha ya kiroho ambayo inatuvua madai ya kujua kila kitu tayari, hatari ya kufikiria kuwa inatosha kutumia sheria, jaribu la kuendelea, hata katika maisha ya Curia Romana, kwa kurudia tu mifumo , bila kuzingatia kwamba Fumbo la Mungu daima linatuzidi na kwamba maisha ya watu na ukweli unaotuzunguka ni na daima unabaki bora kuliko mawazo na nadharia. Maisha ni bora kuliko mawazo, daima. Tunahitaji kujizoeza utambuzi wa kiroho, kuchunguza mapenzi ya Mungu, kuhoji mienendo ya ndani ya moyo wetu, na kisha kutathmini maamuzi yanayopaswa kufanywa na chaguzi zinazopaswa kufanywa. Kardinali Martini aliandika hivi: “Utambuzi ni tofauti sana na uangalifu wa kina wa wale wanaoishi katika usahaulifu wa kisheria au kwa kisingizio cha ukamilifu. Ni mlipuko wa upendo ambao huweka tofauti kati ya mema na bora, kati ya yenye manufaa yenyewe na yenye manufaa sasa, kati ya kile kinachoweza kuwa kizuri kwa ujumla na kile kinachopaswa kukuzwa sasa.” Na akaongeza: “Ukosefu wa mvutano wa kupambanua kilicho bora mara nyingi hufanya maisha ya kichungaji kuwa ya kufurahisha, ya kujirudia: vitendo vya kidini huongezeka, ishara za kitamaduni hurudiwa bila kuona maana yake” (Injili ya Maria, Milano 2008, 21), hii ni nukuu nyingine kutoka kwake.  Kwa hiyo utambuzi lazima utusaidie, hata katika kazi ya Curia, kuwa watiifu kwa Roho Mtakatifu, kuweza kuchagua mielekeo na kufanya maamuzi si kwa msingi wa vigezo vya kidunia, au kwa kutumia kanuni tu, bali kulingana na Injili. “Sikiliza, Maria, kutambua, Mbatizaji na sasa neno la tatu, bi kutembea.” Papa alisisitiza.

Viongozi wa Curia Romano na Papa
Viongozi wa Curia Romano na Papa

Na mawazo yetu kwa kawaida yanakwenda kwa Mamajusi. Hao wanatukumbusha umuhimu wa kutembea. Tunapoikaribisha Furaha ya Injili,  kiukweli, huchochea mwendo wa kufuata ndani yetu, na kusababisha msafara wa kweli kutoka kwetu na kutuweka kwenye njia kuelekea kukutana na Bwana na kuelekea utimilifu wa maisha. Kuhama kutoka kwetu. Mtazamo wa maisha yetu ya kiroho ambao lazima tuuchunguze kila wakati. Imani ya Kikristo - hebu tukumbuke hili - haitaki kuthibitisha hakika zetu, kutufanya tuwe na hakika za kidini rahisi, au kutupa majibu ya haraka kwa matatizo magumu ya maisha. Kinyume chake, Mungu anapoita daima huvuvia njia, kama ilivyokuwa kwa Ibrahimu, Musa na kwa manabii na kwa wanafunzi wote wa Bwana. Yeye hutuweka katika safari, hututoa nje ya maeneo yetu ya usalama, anahoji juu ya upatikanaji wetu na kwa usahihi kwa njia hii, hutuweka huru, hutubadilisha, huangaza macho ya mioyo yetu ili kutufanya tuelewe ni tumaini gani ambalo ametuitia (rej. Waefeso 1:18). Kama Michel de Certeau anavyosema, "yeye ambaye hawezi kuacha njia ni fumbo. […] Tamaa huleta ziada. Inazidi, inapita na kupoteza mahali. Inakufanya uende mbali zaidi, mahali pengine

Baba Mtakatifu amesema kuwa “Hata katika huduma hapa katika Curia ni muhimu kukaa kwenye njia, si kuacha kutafuta na kuzama katika ukweli, kushinda jaribu la kubaki kimya kwenye "labyrinth" njia isiyo toka  na kubaki ndani ya ua wetu na hofu zetu. Hofu, ugumu, marudio ya mifumo huzalisha utulivu, ambau na faida dhahiri ya kutoleta shida lakini  kutulia hakina kusonga mbele na, hutuongoza kuzunguka katika njia zetu zisizo na kutoka, tukiadhibu huduma ambayo tumeitwa kutoa kwa Kanisa na kwa dunia nzima. Na tuwe makini dhidi ya uthabiti wa itikadi  na  tuwe waangalifu: uthabiti wa itikadi  ambayo mara nyingi, chini ya kivuli cha nia njema, hututenganisha na ukweli na kutuzuia kusonga mbele.” Badala yake tunaitwa kusafiri na kutembea, kama Mamajusi walivyofanya, kufuata Nuru ambayo daima inataka kutuongoza zaidi na ambayo wakati mwingine hutufanya kutafuta njia ambazo hazijachunguzwa na kutufanya tusafiri njia mpya. Na tusisahau kwamba safari ya Mamajusi - kama kila safari ambayo Biblia inatuambia - daima huanza “kutoka juu” kwa ajili ya wito kutoka kwa Bwana, kwa ishara itokayo mbinguni au kwa sababu Mungu mwenyewe anakuwa kiongozi anayeangazia hatua za watoto wake. Kwa hiyo, wakati huduma tunayoifanya ina hatari kuwa isiyo na upenyo wa kutoka,  katika ugumu  au wastani, tunapojikuta tumechanganyikiwa katika mitandao ya urasimu na “kupitia”, tukumbuke kutazama juu, kuanza tena kutoka kwa Mungu; kujiruhusu kuangazwa na Neno lake, kupata daima ujasiri wa kuanza tena.” Papa aongeza: “ Na tusisahau kwamba njia pekee ya  kutoka nje nje njia isyo na upenuo ni “kutokea juu.” Inahitaji ujasiri wa kutembea, kwenda mbali zaidi. Ni suala la utashi. Inahitaji ujasiri wa kupenda.”

Papa na Curia Romana kwa Heri za Noeli 2023
Papa na Curia Romana kwa Heri za Noeli 2023

Papa amependa  kukumbuka tafakari ya Padre mwenye bidii juu ya fundisho hilo, ambalo linaweza pia kuwasaidia katika kazi yao kama Curia. Alisema kuwa “ni vigumu kuwasha tena makaa chini ya majivu ya Kanisa. Mapambano ya leo ni kufikisha shauku kwa wale ambao tayari wameipoteza zamani. Miaka 60 baada ya Mtaguso, bado kuna mjadala juu ya mgawanyiko kati ya "progressives" na "conservatives", yaani (muktadh wa maendeleo  kwa kuzingatia sera ya mageuzi na upya na wale ambao wanalinda na kutunza bila kutotaka kubadilika kwa wakati) na  kuwa hii sio tofauti,  kwani tofauti kuu ya kweli ni kati ya "kupendeza na "kuzoea". Hii ndiyo tofauti. Ni wale tu wanaopenda wanaweza kutembea.” Papa amekazia. Baba Mtakatifu amerudia kuwashukuru kwa kazi yao  na kujitolea kwao. “Katika kazi yetu, tunasitawisha kusikiliza kwa moyo, hivyo kujiweka katika utumishi wa Bwana kwa kujifunza kukaribishana, kusikilizana; tujizoeze kupambanua, kuwa Kanisa linalotaka kufasiri ishara za historia kwa Nuru ya Injili, kutafuta masuluhisho yanayopitisha upendo wa Baba; na tubaki daima katika safari, kwa unyenyekevu na mshangao, ili tusianguke katika dhana ya kujisikia kuwa tumefika na ili hamu ya Mungu isifie ndani yetu. Amewashukuru sana na zaidi ya yote kwa kazi yao wanayofanya kwa kimya kimya. Wasisahau “kusikiliza, kutambua, na kutembea. Maria, Yohane Mbatizaji na Mamajusi.” Bwana Yesu, Neno aliyefanyika mwili, atupatie  neema ya furaha katika utumishi wa unyenyekevu na ukarimu. Na tafadhaliwasipoteze  hisia zetu za ucheshi, hii ni afya. Heri ya Noeli, pia kwa wapendwa wao! Na, mbele ya Pango la kuzaliwa kwa Yesu, Mniombee.”

Vitabu ambavyo Baba Mtakatifu amewazawadia Curia Romana
Vitabu ambavyo Baba Mtakatifu amewazawadia Curia Romana

Mara baada ya hotuba yake, Baba Mtakatifu amewasalimia mmoja mmoja wa Sekretarieti ya Curia Roma na kuwazawadia vitabu kwa ajili ya Noeli Kwa maana hiyo Vitabu vilivyotolewa zawadi ni vitatu vyenye kichwa: “Noeli, mahubiri na mazungumzo yaliyochaguliwa” vilivyotolewa na OssiApp. AidhaKitabu cha tatu, kimechapishwa na LEV chenye kichwa: “Noeli 10 pamoja - Matashi mema kwa Sekretarieti Kuu 2013 -2023”

Hotuba ya Papa kwa Curia Romana kutakiana heri ya Noeli 2023
21 December 2023, 17:38