Wakimbizi wanaookolewa  kutoka katika mitumbwi ya kiajabu baharini. Wakimbizi wanaookolewa kutoka katika mitumbwi ya kiajabu baharini.  (AFP or licensors)

Papa,Siku ya Kimataifa ya Haki za Wahamiaji:Uhamiaji ni ishara za nyakati

Papa Francisko katika ujumbe mfupi wa mitandao ya kijamii katika Siku ya kimataifa ya haki za Wahamiaji anasema:“Wahamiaji ni shara za nyakati.Kwetu sisi wakristo ni jukumu ambalo pia ni uaminifu kwa Yesu ambaye alisema:Nilikuwa mgeni na mkanikaribisha(Mt 25,35).”

Na Angella Rwezaula - Vatican

Katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa kwa Haki za wahamiaji, ifanyikayo kila tarehe 18 Desemba ya kila mwaka, Baba Mtakatifu  Francisko ametoa ujumbe wake mfupi katika mitandao ya kijamii kuwa:  “ Wahamiaji ni ishara za nyakati mahali ambapo ni wajibu wa kiraia. Kwetu sisi wakristo ni wajibu  ambao pia  ni uaminufu kwa Yesu, ambaye alisema: “ Nilikuwa mgeni na mkanikaribisha (Mt 25,35). Inahitajika upendo unaofanya ukaribu, wakipekee  na upendo mkuu kama ulivyo upendo wa Mungu kwetu sisi.”


Katika Muktadha huo wa Wahamiaji  hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 17 Desemba 2023 alitoa wito kwa ajili ya Wahamiaji kati ya Colombia na Panama. Papa alisema: “Leo ningependa kukumbuka maelfu ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka msitu wa Darién, kati ya Colombia na Panama. Mara nyingi hizo ni familia zilizo na watoto ambao huingia kwenye njia hatari, wakidanganywa na wale wanaowaahidi kwa uwongo njia fupi na salama, wakitendewa vibaya na kuibiwa. Wachache kabisa wanapoteza maisha katika msitu huo. Tunahitaji juhudi za pamoja za nchi zilizoathirika zaidi moja kwa moja na jumuiya ya kimataifa ili kuzuia ukweli huu wa kutisha usipitie chini chini bila kutambuliwa na kutoa kwa pamoja jibu la kibinadamu."

Katibu Mkuu wa UN,António Guterres:Uhamiaji ni kama nguvu chanya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres katika fursa ya  Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji inayoadhimishwa kila  tarehe 18 Disemba, amebainisha kwamba “Uhamiaji ni ukweli wa maisha na nguvu ya wema. Unakuza kubadilishana maarifa na mawazo na kuchangia ukuaji wa uchumi. Unawezesha mamilioni ya watu kutafuta fursa na kuboresha maisha yao. Wakati huo huo, uhamiaji usio na udhibiti mzuri husababisha mateso makubwa. Huwalazimu watu kushikwa na mtego wa kikatili wa wasafirishaji haramu wa binadamu, ambapo wanakabiliwa na unyonyaji, unyanyasaji na hata kifo. Hudhoofisha imani kwa utawala na taasisi, huzusha mivutano ya kijamii na kuharibu ubinadamu wetu wote. Katika Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji, tunaakisi hitaji la dharura kwa ajili ya utawala salama wa uhamiaji, unaokita mizizi katika mshikamano, ushirikiano na kuheshimu haki za binadamu Miaka mitano iliyopita, jumuiya ya kimataifa ilipitisha Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji Salama, Unaopangwa na wa Kawaida.( Global Compact per una migrazione sicura, ordinata e regolare.).Hiyo imekuwa marejeo muhimu na nyenzo kwa Nchi Wanachama kutathmini hatua, kuimarisha ushirikiano na kupanua njia za uhamiaji zinazozingatia haki. Bado hatua kama hizo zinabaki kuwa za ubaguzi,  na sio kawaida. Leo hii na kila siku ni lazima tufanye kazi kwa ajili ya usimamizi wa kiutu na utaratibu wa uhamaji kwa manufaa ya wote, ikiwa ni pamoja na jumuiya za asili, usafiri na unakokwenda. Kwa pamoja, tunahakikisha mustakabali ulio salama na wenye mafanikio zaidi kwa wote.”

Siku ya Kimataifa ya Haki za Wahamiaji 18 Desemba
18 December 2023, 16:09