Tafuta

2024.01.17 Papa Francisko wakati wa Katekesi walikaribisha kikundi cha sarakasi 2024.01.17 Papa Francisko wakati wa Katekesi walikaribisha kikundi cha sarakasi  (Vatican Media)

Papa aonesha ukaribu na mshikamano kwa eneo la Erbil

Mara baada ya Katekesi yake, Baba Mtakatifu Francisko katika salamu mbali mbali kwa lugha mbali mbali ametoa wito wake kuwa:Ninaelezea ukaribu na mshikamano wangu na waathirika,raia wote, wa shambulio la kombora lililopiga eneo la mijini la Erbil,mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Kurdistan ya Iraq.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Mara baada ya katekesi yake, Jumatano tarehe 17 Januari 2024 hakukosa kuonesha  kilichotokea katika eneo linalojitawala la Kurdistan ya Iraq ambapo Walinzi wa Mapinduzi ya Iran walidai "kulenga na kuharibu moja ya makao makuu ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni (Mossad)," katika uvamizi huo kwa "kombora za balestiki" juu ya Erbil kaskazini mwa Iraq. Katika shambulio hilo, takriban raia watano waliuawa, akiwemo mtoto wa kike wa miezi kumi na moja, huku watoto wengine kadhaa wakijeruhiwa. Hii iliripotiwa na  Shirika moja lisiolo la kiselikali la  Hengaw haki za Binadamu. Kwa njia hiyo Papa ameonesha ukaribu na mshikamano na waathirika wa  raia wote, na kubai isha kuwa: “Ninaelezea ukaribu na mshikamano wangu na waathirika, raia wote, wa shambulio la kombora lililopiga eneo la mijini la Erbil, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Kurdistan ya Iraq. Uhusiano mzuri kati ya majirani haujengwi na vitendo hivyo bali kwa mazungumzo na ushirikiano. Ninaomba kila mtu aepuke hatua yoyote ambayo huongeza mvutano katika Mashariki ya Kati na matukio mengine ya vita.”

Watoto wakiwa na bendera ya Ukraine
Watoto wakiwa na bendera ya Ukraine

Wazo hilo liliongezewa mkazo na Papa Francisko mwishoni mwa salamu kwa mahujaji wanaozungumza lugha ya Kiitaliano kubadilisha sauti ambayo, kwa muda mchache katika ukumbi ambapo kikundi cha wanasarakasi wa Sarakasi ya kifalme(Royal Circus) walikuwa wamecheza. Wengi wao walivaa bendera ya Ukraine, pia ishara ya mshikamano na idadi ya watu wanaokabiliwa na mzozo ambao umedumu kwa karibu miaka miwili sasa. Papa alisema: “Vita daima huharibu, vita haipandi upendo, hupanda chuki. Vita ni kushindwa kweli kwa binadamu. Tunawaombea watu wanaoteseka katika vita.”

Kuomba msaada katika kushinda vita vya kiroho dhidi ya pepo

Kwa kutazama Mashariki ya Kati, maombi ya Papa ya kutaka amani yameoneshwa pia hata ndege yenye dawa, chakula na blanketi iliyokusudiwa  kuwapelekea mateka wa Israel mikononi mwa Hamasambayo  iliwasili katika uwanja wa ndege wa Al Arish wa Misri, kwa msingi wa makubaliano yaliyotiwa saini kati ya Israel na Hamas kwa njia ya upatanishi wa Qatar. Mara tu shughuli za upakuaji zitakapokamilika,msaada huo utakabidhiwa kwa chama cha Luna Rossa ambacho kitaisafirisha hadi kivuko cha Rafah na kutoka hapo hadi Ukanda wa Gaza. Akiwahutubia waamini wanaozungumza Kiarabu, Papa  Fransisko aliwabariki katika umati wa watu wote, akiwataka watembee “katika njia ya upendo ambayo Yesu alitembea hadi msalabani”.

Kikundi cha Sarakasi katika picha ya pamoja
Kikundi cha Sarakasi katika picha ya pamoja

“Upendo pekee huzima mioyo yetu, huponya majeraha yetu na kutupa furaha ya kweli”. Na, tukikumbuka sura ya Mtakatifu Anthoni Aabati ambaye kumbukumbu yake ya kiliturujia inaadhimishwa kila tarehe 17 Januari , Papa Francisko alizungumzia juu ya mapambano, lakini kwa maana ya kiroho katika neno hilo. Kwa hakika, alisisitiza juu ya "mapambano ya kiroho dhidi ya pepo na dhambi ambapo   ambao ni muhimu  kukua katika utakatiffu.” “Hakuna mtu aliye salama kutokana na vita hivi, alikuwa tayari amesisitiza katika siku za mwanzoni katika tafakari yake. Kwa hiyo ametuomba tuombe msaada wa Bwana tuendelee kushinda vita hivi. Na aliongeza, akimaanisha tena mtu ambaye alichukuliwa kuwa mmoja wa waanzilishi wa watawa kwamba “Mfano wake unatuhimiza kukaribisha Injili bila masharti

Wakristo wapate umoja kamili

Katika mkesha wa Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo, linaloanza tarehe 18 Januari -25 Januari Papa alieleza matumaini yake kwamba kila mgawanyiko utashindwa. Tayari katika salamu zake kwa mahujaji wanaozungumza Kireno, alisisitiza jinsi ambavyo Bwana, aliyetuumba, anatuita kufuata njia za umoja. Kubainisha: "Siku zote tunachota ubunifu wa kufanya hivi kutoka kwa Injili". Kwa hiyo amewaalika waamini wote kusali, ili Wakristo wapate umoja kamili na kutoa ushuhuda mmoja wa upendo kwa wote, hasa kwa wale walio dhaifu zaidi.”

Wito wa papa baada ya Katekesi
17 January 2024, 16:33