Mafuriko mabaya ya Valencia nchini Hispania ambayo hayajawahi kutokea. Mafuriko mabaya ya Valencia nchini Hispania ambayo hayajawahi kutokea. 

Huzuni ya Papa kwa mafuriko ya hispania:Ninawaombea

Papa Francisko alituma ujumbe wa kwa njia ya video kwa wenyeji wa Valencia, walioharibiwa na Kimbunga Dana ambacho hadi sasa kimesababisha vifo vya zaidi ya 150, idadi isiyojulikana ya watu waliopotea na zaidi ya watu 1200 waliokimbia makazi.Papa anaonesha ukaribu wake na sala.Askofu wa Valencia,Benavent Vidal:Wakristo washikamane na wale wanaoteseka zaidi.Miundo ya Kanisa iwe mahali pa mshikamano na makaribisho.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ukaribu na maombi kwa wakazi wote wa Valencia katika wakati huu wa janga. Papa Francisko ameelezea uchungu wake kwa WanaValencia nchini Hispania walioathiriwa na Kimbunga Dana kupitia ujumbe kwa njia ya video ulioelekezwa kwa Askofu Mkuu Luis Javier Argüello García, wa jiji kuu la  Valladolid na rais wa Baraza la Maaskofu wa nchi hiyo, ambapo anawahakikishia ukaribu wake na watu wa Valencia na kutuma baraka zake. Hata hivyo  hali ya anga iliharibu pwani ya mashariki ya Hispania na zaidi ya waathiriwa rasmi 150, wakati idadi isiyojulikana ya watu waliopotea na zaidi ya watu 1200 waliokimbia makazi yao. Hili ndilo tukio lenye nguvu zaidi ambalo nchi inaweza kukumbuka, ambalo hata wanasayansi wanahusisha na mabadiliko ya tabianchi na ambayo katika masaa 8 ilisababisha mvua zaidi kuliko miezi 20 iliyopita.

Wito kutoka kwa  Mfalme

Tahadhari mpya nyekundu ilitolewa pia na wakala wa hali ya hewa wa Hispania kwa  maeneo kadhaa za Castellón, mkoa wa kaskazini kabisa wa mkoa wa Valencia, moja ya eneo linalovuna  machungwa mengi sana, kusini mwa Tarragona, kaskazini-mashariki mwa Catalonia, na kwa pwani ya magharibi ya Cadiz, kusini-magharibi mwa nchi. Wahispania pia walipokea wito kutoka kwa Mfalme Felipe wa Sita, ambaye aliwataka “kubaki na umoja katika misaada ili tuweze kuondokana na kiwewe hiki. Dharura haijaisha, na kuna utabiri wa hatari,"alielezea, mfalme

Matukio ya uharibifu

Nchi iliamka na matukio ya uharibifu na vijiji vizima kusombwa na mafuriko. Msako wa kuwatafuta waliopotea unaendelea bila kukoma. Mito ya maji ilifurika orofa za chini za majengo, na kufagia kila kitu kwenye njia yao. Madaraja na barabara nyingi zimeharibiwa, njia za reli zimekatizwa. Karibu familia 80,000 bado hazina umeme, wakati idadi isiyojulikana ya watu hawana maji ya bomba. "Kipaumbele chetu ni kutafuta waathiriwa na waliopotea, ili tuweze kusaidia kumaliza mateso ya familia zao," Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sánchez alisema katika siku ya kwanza kati ya tatu za maombolezo rasmi nchini humo.

Askofu wa Valencia: karibu na wale wanaoteseka

"Lilikuwa tukio la kushangaza ambalo lilishangaza kila mtu, kwa kasi ya matukio na kwa kiwango cha janga ambalo hatukujua - alisema Askofu Mkuu  Enrique Benavent Vidal, askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Valencia – Jumatano asubuhi tarehe 29 Oktoba 2024 ndipo tulianza kutambua kilichotokea, kutoka katika picha za televisheni, kutoka katika idadi inayokua kwa kasi ya waathiriwa." Haraka iwezekanavyo, aliongeza, kwamba yeye mwenyewe atasafiri hadi maeneo yaliyoathirika kutembelea parokia na mapadre, "ambao ni sawa, lakini makanisa mengine yameharibiwa kabisa."Kwa hiyo Askofu Mkuu Benavent Vidal aliwaomba Wakristo kuwa "katika mshikamano na wale wanaoteseka zaidi." Miundo ya parokia ipatikane, "ili iweze kuwa mahali pa mshikamano na kukaribishwa" na Caritas inafanya kazi pamoja na wale ambao wamepoteza kila kitu. Kisha Askofu  Mkuu alizindua ujumbe wa matumaini: “hali hii inatusaidia kuwa ndugu zaidi na, licha ya yote, kuishi kwa matumaini na kumtumaini Mungu.”

Huzuni wa Papa kwa waliokumbwa kimbunga VALENCIA
31 October 2024, 18:05