Tafuta

2024.10.31 Mkutano Mkuu wa Papa Francisko na Baraza la Kipapa la Mawasiliano. 2024.10.31 Mkutano Mkuu wa Papa Francisko na Baraza la Kipapa la Mawasiliano.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko na ndoto kwa wawasilianaji:kuakisi walio wa mwisho na kutangaza Injili!

Papa akikutana na Baraza la Kipapa la Mawasiliano wakati wa kuhitimisha Mkutano Mkuu ameeleza ndoto yake kwa Mawasiliano:kuwasiliana kutoka moyoni,kuhusika na ubinadamu,kuumizwa na mikasa ya ndugu wengi;mawasiliano ya kwenda zaidi ya kauli mbiu,umakini kwa masikini,wahamiaji, waathiriwa wa vita;kushuhudia leo hii uzuri wa kukutana na mwanamke Msamaria,Nikodemu,mwanamke mzinzi na Bartimayo kipofu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 31 Oktoba 2024 amekutana karibia na washiriki 300 wa Mkutano Mkuu Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa kuongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini katika Ukumbi wa Clmentina katika Jumba la Kitume, mjini Vatican ambapo katika hotuba yake Papa alifafanua utambulisho wa mzungumzaji (mwana mawasiliano) mwema, mtu ambaye yuko thabiti katika ukweli na haki na yuko tayari kueneza Injili!

Hotuba ya Papa kwa wanahabari
Hotuba ya Papa kwa wanahabari

Papa Francisko akianza hotuba yake amewasalimia wote kuanzia na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano wasimamizi wengine; Makardinali na Maaskofu waliookuwapo na wote wanaonda jumuiya hii kubwa ya wafanyakazi. Baba Mtakatifu Francisko ameeleza kwamba katika liturujia ya leo tunasoma himizo hili kutoka kwa Mtakatifu Paulo: Basi simameni imara, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa ajili ya kunesea Injili ya mani”(Waef 6:14-15). Inaweza pia kuwa kitambulisho cha mwasilianaji mzuri, sivyo unafikiri? Inaweza kwenda…Papa amesisitiza "Hakika ninyi ni wito, na ni utume! Kwa kazi yenu na ubunifu wenu, kwa matumizi ya akili ya njia ambazo teknolojia hufanya kupatikana, lakini juu ya yote kwa moyo wenu: mnawasiliana na moyo.

Papa amendelea kusema kuwa "Mnaitwa kwa kazi kubwa na ya kusisimua: ile ya kujenga madaraja, wakati wengi wanajenga kuta, kuta za itikadi; ile ya kukuza ushirika, wakati watu wengi waanzisha migawanyiko; ile ya kujihusisha na mikasa ya wakati wetu, wakati wengi wanapenda kutojali. “Na utamaduni huu wa kutojali, utamaduni huu wa “kunawa mikono”:ya “siyo zamu yangu. Acha wafanye “... Hii inauma sana!” Katika siku hizi za Mkutano  wenu mmejiuliza jinsi gani ya kuhimiza mawasiliano ambayo ni kujenga kisinodi. Sinodi ya kisinodi ambayo tumehitimisha hivi karibuni inakuwa ni njia ya kawaida inayopaswa kuleta maendeleo; “njia inayotokana na wakati ambapo Mtakatifu Paulo VI aliunda Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu.”

Hotuba ya Papa kwa wanabari
Hotuba ya Papa kwa wanabari

Mtindo ambao tunaishi nao ushirika katika Kanisa, mtindo wa sinodi. Katika kila onesho la maisha ya jumuiya yetu, tunaitwa kurudisha upendo huo wa kimungu ambao katika Kristo ulituvutia na kutuvuta. Na hii ndiyo sifa ya kuwa mali ya kikanisa: ikiwa tungejadiliana na kutenda kulingana na makundi ya kisiasa au ya ushirika, hatungekuwa Kanisa. Hii si sawa! Ikiwa tungetumia vigezo vya kidunia au ikiwa tungepunguza miundo yetu kwa urasimu, tusingekuwa Kanisa. Kuwa Kanisa kunamaanisha kuishi katika ufahamu kwamba Bwana anatupenda sisi kwanza, anatuita kwanza, anatusamehe sisi kwanza (taz. Warumi 5:8). Na sisi ni mashuhuda wa huruma hii isiyo na kikomo, ambayo imemiminwa kwa uhuru juu yetu, kubadilisha maisha yetu.

Mkutano na   Papa
Mkutano na Papa

Baba Mtakatifu ameongeza na “Sasa mnaweza kuniuliza: lakini yote haya yana uhusiano gani na kazi yetu kama wawasilianaji, na kazi yetu kama waandishi wa habari? Ina kitu cha kufanya nayo, na mengi! Kwa hakika kama wawasilianaji, kiukweli, mmeitwa kusuka ushirika wa kikanisa na ukweli kiunoni mwenu, haki kama silaha, viatu na kuwa tayari kueneza Injili ya amani.” Katika kukazia hilo Baba Mtakatifu Francisko ameelezea ndoto yake kwa wanahabari kwamba : Acha niwambie ndoto yangu. Nina ndoto ya mawasiliano ambayo yanaweza kuunganisha watu na tamaduni. Ninaota ndoto ya mawasiliano yenye uwezo wa kusimulia na kuthibitisha historia na shuhuda zinazotokea kila kona ya dunia, zikiziwekwa katika mzunguko na kuzitoa kwa kila mtu.

Mkutano wa Papa na wanahabari
Mkutano wa Papa na wanahabari

Ndiyo maana ninafurahi kujua kwamba - licha ya ugumu wa kiuchumi na hitaji la kupunguza gharama, nitazungumza juu yake baadaye ... mmejitahidi kuongeza toleo la lugha zaidi ya hamsini ambazo vyombo vya habari vya Vatican vinawasiliana, na kuongeza lugha za Kilingala, Kimongolia na Kikannada. Ninaota ndoto ya kuwasiliana kutoka moyoni, tukijiruhusu kuhusika katika mambo ya kibinadamu, tukijiruhusu kuumizwa na mikasa inayowapata kaka na dada zetu wengi. Hii ndiyo sababu ninawaalika kwenda nje zaidi, kuthubutu zaidi, kujihatarisha zaidi, na sio kueneza mawazo yenu, lakini kusema ukweli kwa uaminifu na shauku. Ninaota ndoto ya mawasiliano ambayo inajua jinsi ya kwenda zaidi ya kauli mbiu na kuweka umakini zaidi kwa masikini, walio hatarini zaidi, wahamiaji, na waathiriwa wa vita. Mawasiliano ambayo yanakuza ushirikishwaji, mazungumzo na utafutaji wa amani.

Hotuba ya Papa kwa wanahabari
Hotuba ya Papa kwa wanahabari

Papa amesisitiza kwamba: “Ni uharaka ulioje kuwapa nafasi wapatanishi! Msichoke kueleza shuhuda zao, katika kila sehemu ya dunia. Ninaota ndoto ya mawasiliano ambayo ynatufundisha kuacha kidogo juu yetu wenyewe ili kutoa nafasi kwa wengine; mawasiliano ya shauku, ya kudadisi na yenye uwezo, ambayo yanajua jinsi ya kuzama katika hali halisi ili kuitangaza. Inatufaa kusikiliza historia zenye ladha ya kiinjili ambayo leo, kama miaka elfu mbili iliyopita, inatuambia kuhusu Mungu kama vile Yesu, Mwana wake, alivyomfunua kwa ulimwengu.

Papa Francisko ametuomba kwamba Tusiogope kujihusisha, kubadilika, kujifunza lugha mpya, kusafiri njia mpya, kukaa katika mazingira ya kidijitali. Daima kufanya hivyo bila kujiruhusu kuvutiwa na zana tunazotumia, bila kufanya chombo kuwa ujumbe, bila kupuuza, bila kuidhinisha uhusiano wa kweli, thabiti, wa mtu na mtu katika mkutano wa mtandaoni. Injili ni historia ya kukutana, ya ishara, ya kutazama, mazungumzo mitaani na mezani.” Papa bado aliendelea kueleza kwamba “ Ninaota ndoto ya mawasiliano ambayo yanaweza kushuhudia leo hii uzuri wa kukutana na mwanamke Msamaria, na Nikodemu, na mwanamke mzinzi na Bartimayo kipofu ...

Mkutano wa Papa na Baraz ala kipapa la Mawasiliano
Mkutano wa Papa na Baraz ala kipapa la Mawasiliano

“Yesu, kama nilivyoandika katika Waraka Mpya wa  Dilexit nos, “anapatia uangalifu wake wote kwa watu, kwa wasiwasi wao,  na kwa mateso yao” (n. 40). Kwa hiyo “Sisi wawasilianaji tumeitwa kufanya vivyo hivyo, kwa sababu kwa kukutana na upendo, upendo wa Yesu, "tunakuwa na uwezo wa kusuka vifungo vya kidugu, kutambua utu wa kila mwanadamu na kutunza nyumba yetu ya kawaida pamoja.” Kwa  hiyo papa ameongeza “ Nisaidie, tafadhali, kuufanya Moyo wa Yesu ujulikane kwa ulimwengu, kwa njia ya huruma kwa dunia hii iliyojeruhiwa. Nisaidie, kwa mawasiliano, kuhakikisha kwamba ulimwengu,” ambao unasalia kati ya vita, kukosekana kwa usawa wa kijamii na kiuchumi, kutumia sana na matumizi ya teknolojia dhidi ya binadamu, mnaweza kurejesha kile ambacho ni muhimu zaidi yaani : moyo ( Dilexit nos, 31). Nisaidie kwa mawasiliano ambayo ni chombo cha ushirika.

Papa pia ameakisi usahihi wa taaluma ambayo lazima pia zishughulikie shida za kiuchumi na hitaji la kupunguza gharama ambapo amebainisha kwamba " Ingawa ulimwengu umetikiswa na jeuri ya kutisha, sisi Wakristo tunajua jinsi ya kutazama miali mingi ya matumaini, katika historia nyingi ndogo na kubwa za mema. Pia ningependa kumtaja Bi. Gloria Fontana. Ni siku yako ya mwisho kazini: Ninatumaini watakufanyia sikukuu! Vema baada ya miaka 48 ya huduma: aliingia siku ya Komunyo yake ya Kwanza, nadhani... alitania Papa. "Alifanya huduma nzuri mafichoni, akijitolea kunakili hotuba za Papa na  kuhamasisha kwa wote."

Bi Gloria anayekwenda pensheni baada ya kufanya kazi miaka 48
Bi Gloria anayekwenda pensheni baada ya kufanya kazi miaka 48

Kishauovu hautashinda, kwa sababu ni Mungu ambaye anaongoza historia na kuokoa maisha yetu. "Na ningependa kukuambia jambo moja: bado tutalazimika kufanya nidhamu zaidi na pesa. Ni lazima mtafute njia ya kuokoa zaidi na kutafuta fedha nyingine, kwa sababu Vatican haiwezi kuendelea kusaidia kama ilivyo sasa. Ninajua ni habari mbaya, lakini habari njema kwa sababu inasongesha kuwa  na ubunifu wenu nyote.”

Jubilei

Jubilie, ambayo tutaanza baada ya  majuma machache, ni fursa nzuri ya kutoa ushuhuda wa imani yetu na matumaini yetu kwa ulimwengu. Ninawashukuru mapema kwa yote mnayoyafanya, kwa dhamira ya Baraza la Kipapa  kusaidia mahujaji wote watakaofika Roma na wale ambao hawataweza kusafiri, lakini shukrani kwa vyombo vya habari vya Vatican vitaweza kufuatilia maadhimisho ya Jubilei wakiwa na umoja pamoja nasi.  Asante! Asante, sana! Ninawabariki kwa moyo wote ninyi na kazi zenu. Na tafadhali msisahau kuniombea. Asante!

Hotuba ya Papa kwa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Oktoba 31
31 October 2024, 12:45