Nia za Papa Francisko kwa mwezi Novemba 2024:kwa waliofiwa mtoto,wazazi wasaidiwe

Katika ujumbe kwa njia video wa Papa Francisko wenye nia ya maombi kwa mwezi wa Novemba 2024,mawazo yake yanageukia wale wanaoomboleza kifo cha mtoto wa kiume au wa kike:Ni maumivu makali sana kiasi kwamba hakuna hata maneno ya kueleza.Familia zisikilize vidonda hivyo na jamii iwatunze,"Papa anasema.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa upande wa Baba Mtakatifu Francisko, kufiwa na mtoto ni jambo la kusikitisha sana na halina maelezo kiasi kwamba sentensi za kiutamaduni ambazo haziambatani na ukaribu wenye upendo, nyeti na wa maombi hazina maana.” Ni mada ambayo tayari Papa alipata fursa ya kujieleza mara kadhaa na sasa imerudia katika ujumbe wake kwa njia ya  video kama kawaida iliyoundwa na Mtandao wa wa Kimataifa wa nia za Maombi ya Papa kwa Mwezi Novemba 2024 uliochapishwa tarehe 31 Oktoba 2024. Baba Mtakatifu anauliza kuwa : “Unaweza kusema nini kwa wazazi ambao wamepoteza mtoto? Jinsi gani ya kuwafariji?”

Hakuna maneno mbele ya kufiwa mtoto

Papa amesema "Kutoweza kuita jina, baada ya kufiwa na mtoto ni jambo ambalo haliwezi kupuuzwa na kuzidisha maumivu haya. “Fikiria: mmoja wa wanandoa anapofiwa na mwenzake ni mjane au mgane, mtoto aliyefiwa na mzazi ni yatima, kuna neno. Lakini kwa mzazi anayefiwa na mtoto, hakuna neno na jina.” Papa anaongeza kuwa "si kawaida kwa mzazi kuishi muda mrefu zaidi ya mtoto wake. Maneno ya kustarehesha wakati mwingine hayana maana au ya hisia na hayafai kitu. Hata kama yanasemwa kwa nia nzuri zaidi, yanaweza kuishia kuongeza maumivu."

Nia za sala Novemba 2024
31 October 2024, 16:35