2024.10.28 Papa Francisko akutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Kimisionari la  Mtakatifu Carlo(Wascalabrini.) 2024.10.28 Papa Francisko akutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Kimisionari la Mtakatifu Carlo(Wascalabrini.)  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa wamisionari wa Mtakatifu Carlo:kutunza wahamiaji na waathirika wa dhuluma za kibinadamu!

Papa Francisko akikutana na Wamisionari wa Mtakatifu Carlo wajulikanao Wascalabrini amejikita na mada ya Jubilei:“Mahujaji wa Matumaini” iliyoongoza Mkutano wao Mkuu wa XVI wa Shirika na kusisitiza mambo matatu katika huduma:wahamiaji,huduma ya uchungaji wa dharura na upendo unaomrudishia haki na kitovu cha utu wa mwanadamu

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 28 Oktoba 2024,Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu XVI wa Shirika la  Kimisionari ya Mtakatifu Carlo, wajulikanao Wascalabrini. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu amesema: “Mnaadhimisha katika mkesha wa Mwaka Mtakatifu na ni jambo la kupendeza kwamba, katika kupanga umisionari na uchungaji wenu wa siku za usoni kwa ajili ya wahamiaji, mmechagua kupata msukumo kutoka katika mada ya Jubilei: “Mahujaji wa Matumaini.” Kisha tunaweza kutafakari pamoja juu ya wema huu, tukirejea vipengele vitatu vya huduma yenu:wahamiaji, huduma ya kichungaji na upendo." Akianza kudadavua vipengele hivyo ameanza na wahamiaji. Papa amesema: "Ni walimu wa matumaini. 'Mimi ni mtoto wa wahamiaji. Na nyumbani siku zote tumeishi ile ya kwenda huko kuifanya Amerika, kusonga mbele, kwenda mbali zaidi.' Hawa wanaondoka wakiwa na matumaini ya kupata mkate wao wa kila siku mahali pengine,  kama Mtakatifu Yohana Mbatizaji Scalabrini alivyosema na hawakati tamaa, hata wakati kila kitu kinaonekana kwenda kinyume na wao, hata wanapopata kufungwa na kukataliwa.”

Papa amekutana na wascalabrini
Papa amekutana na wascalabrini

Uimara wao, ambao mara nyingi unaungwa mkono na upendo kwa familia zilizoachwa katika nchi zao, unatufundisha mengi, hasa kwao ambao ni  wahamiaji kati ya wahamiaji,  kama mwanzilishi wao alivyotaka ushiriki safari yao. Kwa hiyo, kwa njia ya mienendo ya kukutana, ya mazungumzo, ya kumkaribisha Kristo aliyepo ndani ya mgeni, wao wanakua pamoja nao, katika mshikamano na kila mmoja, ahachwi katika Mungu na katika Mungu peke yake.” Papa amesisitiza kwamba: “Msisahau Agano la Kale: mjane, yatima na mgeni. Wao ni mapendeleo ya Mungu.” Utafutaji wa wakati ujao unaohuisha mhamiaji, zaidi ya hayo, unaonesha hitaji la wokovu unaounganisha kila mtu, bila kujali rangi na hali.  Kwa hakika, mzunguko, unaoeleweka na kuishi kwa usahihi, unaweza kuwa, hata katika maumivu, shule ya thamani ya imani na ubinadamu kwa wale wanaosaidia na wale wanaosaidiwa (taz. Ujumbe kwa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani 27 Mei 2019).

“Tusisahau kwamba historia ya wokovu yenyewe ni historia ya wahamiaji, ya watu wanaohama. Na hii inatuleta kwenye jambo la pili: hitaji la uchungaji wa matumaini. Hakika, ikiwa kwa upande mmoja uhamiaji, kwa usaidizi unaofaa, unaweza kuwa wakati wa ukuaji kwa kila mtu, kwa upande mwingine, ikiwa uzoefu katika upweke na kuachwa, inaweza kudhoofika na kuwa janga la kung'olewa kwa uhalisia, migogoro ya maadili na mitazamo, hadi kusababisha upotevu wa imani na kukata tamaa. Ukosefu wa haki na jeuri ambalo kaka  na dada zetu wengi hupitia, wakiwa wameng'olewa kutoka katika nyumba zao, mara nyingi ni wa kikatili sana hivi kwamba wanaweza kuwavuta hata walio na nguvu zaidi kwenye giza la kukata tamaa au giza la kujiuzulu. “Tusisahau kwamba wahamiaji lazima wapokelewe, wasindikizwe, wahamasishwe  na washirikishwe. (Kukaribishwa, kusindikizwa, kuhamasishwa na kuunganishwa”)Papa Francisko alirudia kukazia vipengele hivi.

Wamisionari wascalabrini
Wamisionari wascalabrini

Iwapo tunawataka wasikose nguvu na uthabiti unaohitajika ili kuendelea na safari zinazofanywa, tunahitaji mtu anayeinama chini ya  majeraha yao, kutunza udhaifu wao mkubwa wa kimwili, pia udhaifu (wao) wa kiroho na kisaikolojia. Maingiliano madhubuti ya kichungaji ya ukaribu yanahitajika, kwa kiwango cha nyenzo, kidini na kibinadamu, ili kudumisha tumaini ndani yao, pamoja na njia za ndani zinazoongoza kwa Mungu, msafiri mwaminifu, anayekuwepo kila wakati pamoja na wale wanaoteseka (rej. Ujumbe wa Papa Benedikto XVI kwa ajili ya Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani Oktoba 2013 na 12 Oktoba 2012). "Na pia, leo nchi nyingi zinahitaji wahamiaji. Italia haina watoto, haina watoto. Umri wa wastani ni miaka 46. Italia inahitaji wahamiaji na lazima ipokee, isindikizane nao, iwaendeleze na kuwaunganisha. Lazima tuseme ukweli huu,” Papa amesisitiza 

Na hii inatuleta kwenye kipengele cha tatu Upendo. Katika kukaribia Jubilei  ya 1900, Mtakatifu Yohane Mbatizaji Scalabrini alisema: “Dunia inaugua chini ya uzito wa maafa makubwa.” Haya ni maneno mazito, lakini kwa bahati mbaya bado yanasikika sana. Hata leo, kiukweli, wale wanaoondoka mara nyingi hufanya hivyo kwa sababu ya tofauti zenye kuhuzunisha na zisizo za haki katika fursa, demokrasia, wakati ujao, au matukio ya vita yenye uharibifu ambayo yanaikumba sayari. Kinachoongezwa na hayo ni kufungwa na uhasama wa nchi tajiri, ambazo huona yeyote anayebisha hodi kwenye mlango wao kuwa tishio kwa ustawi wao. “Pia tunaliona hii: kuna kashfa kwamba kwa mavuno ya apple, Kaskazini, wanaleta wahamiaji kutoka Ulaya ya Kati, lakini kisha kuwawafukuza. Wanawatumia kuchuma maeple kisha wanaondoka. Hii ndiyo leo.”

Kwa hivyo, katika mzozo wa kushangaza kati ya masilahi ya wale wanaolinda ustawi wao na mapambano ya wale wanaojaribu kuishi, wakikimbia njaa na mateso, maisha mengi ya wanadamu yanapotea chini ya mitazamo ya sintofahamu  ya wale wanaotazama tu onesho, au mbaya zaidi kubashiri kwenye ngozi ya wale wanaoteseka. Katika Biblia, mojawapo ya sheria za Jubilei ilikuwa ni kurudisha ardhi kwa wale walioipoteza (taz. Law 25:10-28). Leo hii tendo hili la haki linaweza kudhihirika katika muktadha mwingine katika upendo unaomrudisha mtu, haki zake, utu wake katikati (taz Mtakatifu Yohane Paulo II, Hotuba kwa washiriki wa Kongamano la IV la Dunia linaloandaliwa  na Baraza la Kipapa. Baraza la Utunzaji wa Kichungaji kwa Wahamiaji na Watu Wasafiri, 9 Oktoba 1998, 2), kushinda ubaguzi wa kibaguzi, kutambua wengine, wao ni nani na popote wanatoka, zawadi kutoka kwa Mungu, ya kipekee, takatifu, isiyoweza kuepukika, yenye thamani kwa manufaa ya wote.

Papa akimbariki mscalabrini
Papa akimbariki mscalabrini

Papa Francisko ameshukuru karama ya Wascalabrini hai ndani ya Kanisa: hili linashuhudiwa na vijana wengi ambao kutoka nchi mbali mbali za dunia wanaendelea kuungana nao. Papa amesema wamshukuru Bwana kwa wito uliopokelewa. Hakika, ikiwa wanataka Sura hii iwe fursa ya kukuza na kufanya upya maisha na utume wao, awali ya yote, wafanye iwe wakati wa shukrani ya unyenyekevu na furaha, mbele ya Ekaristi, Yesu aliyesulubiwa na Maria, Mama wa wahamiaji, kama Mtakatifu Yohane Mbatizaji Scalabrini alivyowafundisha. Ni kutoka hapo tu ndipo tunaanza kutembea pamoja, kwa matumaini, katika upendo (taz. Efe 5:2). Na kwa kufikiria wao Papa amesema jinsi ambavyo alitaka kumfanya kardinali, ambaye alitaka kufika hapo awali lakini hakutaka. Sasa, kwa utii, nilifanya hivyo. Na pia kuna makadinali wa wawili hapa Roma. Kwa njia hiyo amewaleza kwamba “ waichukulie hiyo kama ishara ya heshima, na  kubwa. "Tayari ninawafahamu kutoka katika majimbo mengine  na kujua jinsi mnavyofanya kazi sana.” Asante kwa kazi kubwa mnayoifanya. Ninawabariki na kuwaombea, na ninapendekeza tafadhali msisahau kuniombea. Asante.” Amehitimisha Papa.

Hotuba ya Papa kwa wascalabrini wamisionari
28 October 2024, 12:23