Papa:ikiwa ubatizo ni sakramenti ya kuzaliwa,kipaimara ni sakramenti ya ukuaji

Papa Francisko katika Katekesi,Jumatano 30 Oktoba 2024 amejikita na mada sakramenti ya kipaimara na kutoa mwaliko wa kugundua matunda ya kwanza ya Roho Mtakatifu.Kipaimara sio kupakwa kwa juu,bali ni mwanzo wa maisha hai katika Kanisa.Katika Jubilei,lazima tuondoe majivu ya kutoshiriki na kuwa kama washika mienge kwenye Michezo ya Olimpiki,wabebaji wa cheche za Roho.

Na Angella Rwezaula – vatican.

Jumatano tarehe 30 Oktoba 2024 Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Akianza tafakari yake amesema: “Leo tunaendelea na tafakari ya uwepo na matendo ya Roho Mtakatifu katika maisha ya Kanisa kwa njia ya Sakramenti. Tendo la utakaso la Roho Mtakatifu hutufikia kwanza kabisa kupitia njia mbili: Neno la Mungu na Sakramenti. Na kati ya Sakramenti zote, kuna moja ambayo ni, bora kamili, ya Sakramenti ya Roho Mtakatifu, na ni juu yake ambayo ningependa kusisisitiza leo hii. Hii ni Sakramenti ya Kipaimara.” Baba Mtakatifu amendelea “Katika Agano Jipya, pamoja na ubatizo wa maji, ibada nyingine imetajwa, ile ya kuwekea mikono, ambayo ina lengo la kuwasiliana na Roho Mtakatifu kwa kuonekana na kwa njia ya kuomba karama za roho (charismatic), na matokeo sawa na zile zilizotolewa kwa Mitume wakati wa  Pentekoste.

Katekesi ya papa 30 Oktoba
Katekesi ya papa 30 Oktoba

Matendo ya Mitume yanaripoti tukio muhimu katika suala hili. ‘Walipojua kwamba baadhi ya watu katika Samaria walikuwa wamepokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohane kutoka Yerusalemu.’ Andiko hilo linabainisha: “Walishuka na kuwaombea ili wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana alikuwa bado hajashuka juu ya hata mmoja wao, bali walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.” Zaidi ya hayo ni yale ambayo Mtakatifu Paulo anaandika katika Waraka wa Pili kwa Wakorintho: “Mungu mwenyewe ndiye atuthibitishaye sisi pamoja nanyi katika Kristo, aliyetupatia sisi upako, ameweka muhuri juu yetu na ametupatia dhamana ya Roho ndani ya mioyo yetu” (1:21-22).

Akiba ya Roho. Papa Francisko ameendelea: “Mada ya Roho Mtakatifu kama "muhuri wa kifalme" ambayo Kristo huwatia alama kondoo wake iko kwenye msingi wa fundisho la "tabia isiyoweza kufutika" inayotolewa na ibada hii. Kadiri muda ulivyopita, ibada ya upako ilichukua sura ya Sakramenti yenyewe, ikichukua sura na yaliyomo tofauti katika zama mbalimbali na katika taratibu mbalimbali za Kanisa. Hapa si mahali pa kurejea historia hii tata sana.” Papa Francisko ameeleza “Lakini maana ya Sakramenti ya Kipaimara katika ufahamu wa Kanisa inaonekana kwangu kuelezewa, kwa urahisi na kwa uwazi, na Katekisimu ya Watu Wazima ya Baraza la Maaskofu wa Italia, inasema hivi: “Kipaimara ni kwa kila mwamini kwa jinsi Pentekoste ilivyokuwa kwa Kanisa zima. […]”

Papa akisalimia mtoto
Papa akisalimia mtoto

Yenyewe inaimarisha kuingizwa kwa ubatizo katika Kristo na Kanisa na kuwekwa wakfu kwa utume wa kinabii, kifalme na kikuhani. Inashirikisha  wingi wa karama za Roho [...]. Kwa hiyo, ikiwa ubatizo ni sakramenti ya kuzaliwa, kipamaira  ni sakramenti ya ukuaji. Kwa sababu hiyo pia ni sakramenti ya ushuhuda, kwa sababu hii inahusishwa kwa karibu na ukomavu wa uwepo wa Kikristo." Hadi wakati huu Katekisimu. Shida ni jinsi gani ya kuhakikisha kwamba Sakramenti ya Kipaimara haipunguzwi, kimatendo, kuwa “mpako uliokithiri”, yaani, sakramenti ya “kuondoka” kutoka katika Kanisa. Papa Francisko ameongeza kusema: “Inasemekana ni sakramenti ya kuaga, kwa sababu mara baada ya vijana wanapopokea sakramenti ya kipaimara, wanaaga na kuondoka kisha watarudi kwa ajili ya harusi. Hivi ndivyo watu husema... Lakini lazima tuifanye kuwa sadaka” ya kushiriki kikamilifu katika maisha ya Kanisa. Ni lengo ambalo linaweza kuonekana kuwa lisilowezekana kwetu kutokana na hali ya sasa katika Kanisa lote, lakini hii haimaanishi kwamba lazima tuache kulifuatilia.

Papa akizunguka kusalimia mahujaji
Papa akizunguka kusalimia mahujaji

Baba Mtakatifu amekazia kusema: “Haitakuwa hivi kwa vipaimara vyote, kwa watoto au watu wazima, lakini ni muhimu iwe hivyo kwa angalau baadhi ambao watakuwa viongozi wa jumuiya. Kwa kusudi hili, inawezekana kusaidia kupata usaidizi katika kutayarisha Sakramenti kutoka kwa waamini walei ambao wamekutana kibinafsi na Kristo na kuwa na uzoefu wa kweli wa Roho. Baadhi ya watu wanasema waliipitia kama kuchanua kwao ndani ya Sakramenti ya Kipaimara waliyopokea wakiwa watoto. Lakini hii haihusu tu watahiniwa wa kipaimara wa siku zijazo; inatutazama sisi sote kila wakati. Mtume alituhakikishia, kuwa “ Pamoja na kipaimara na upako, tumepokea, pia akiba ya Roho ambayo mahali pengine anaiita "malimbuko ya Roho" (Rm 8:23).

Papa akisalimia wana ndoa wapya
Papa akisalimia wana ndoa wapya

Ni lazima "tutumie" amana hii, tufurahie matunda haya ya kwanza, sio kuzika karama na talanta zilizopokelewa chini ya ardhi. Mtakatifu Paulo alimsihi mfuasi wake Timotheo “kuwasha upya karama ya Mungu, iliyopokelewa kwa kuwekewa mikono” (2 Tim 1:6), na kitenzi kilichotumiwa kinadokeza taswira ya mtu anayepuliza moto ili kuwasha tena mwali wake. Hapa kuna hatua nzuri kwa mwaka wa Jubilei! Kuondoa majivu ya mazoea na kutojihusisha, kuwa, kama washika mienge kwenye Michezo ya Olimpiki, wabebaji mwali wa Roho. Na Roho atusaidie kuchukua hatua chache katika mwelekeo huu!Amehitimisha.

Katekesi ya Papa 30 Oktoba 2024
30 October 2024, 10:44