Papa:tuombe kwa ajili ya amani.Je watoto wanahusiano gani na vita?
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya tafakari ya Katekesi yake, Jumatano tarehe 30 Oktoba 2024 ametoa salamu na kuwakaribisha “kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano: Hasa, parokia ya Mtakatifu Leo wa Saraceno na Caritas Teramo-Atri pamoja na Askofu Leuzzi, ambapo amewahimiza "kuendelea kwenye njia ya ushuhuda wa kiinjili." Kisha amewapa salamu "Chama cha Wanasheria Wanawake wa Italia na Shirikisho la Faita-Federcamping", kwao: "Ninahimiza kila mtu katika ahadi zao za kila siku za kutumikia jamii.” Papa Francisko mawazo yake pia yamewaendea vijana, wagonjwa, wazee na wenye ndoa wapya."
Papa amekumbusha siku kuu ya watakatifu wote
“Sasa tunakaribia maadhimisho ya Watakatifu Wote: Ninawaalika mjionee kumbukumbu ya mwaka huu wa kiliturujia, ambapo Kanisa linataka kutukumbusha kipengele cha ukweli wake: utukufu wa mbingu wa ndugu waliotutangulia katika safari ya uzima na ambao sasa, katika maono ya Baba, wanataka kuwa katika ushirika nasi ili kutusaidia kufikia lengo linalotungoja.”
Papa Francisko ametoa wito wa kuomba amani
“Na tuombe amani. Vita inakua! Hebu tufikirie nchi zinazoteseka sana: Ukraine inayoteswa, Palestina, Israel, Myanmar, Kivu Kaskazini. Na nchi nyingi ambazo ziko kwenye vita. Tuombe amani! Amani ni zawadi ya Roho na vita daima - daima, daima, daima! - ni kushindwa. Katika vita hakuna anayeshinda; kila mtu hupoteza. Tuombe amani ndugu. Jana niliona watu 150 wasio na hatia wamepigwa risasi na mashine…Je! watoto wanauhusiano gani na vita? Familia? Wao ni waathirika wa kwanza. Tuombe amani.”