Tafuta

2024.11.09 Papa akutana na Patriaki wa Kanisa la Ashuru ya Mashairiki. 2024.11.09 Papa akutana na Patriaki wa Kanisa la Ashuru ya Mashairiki.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa akutana na Patriaki Mar Awa III wa Ashuru:tuombe tufikie umoja kamili

Papa akutana na Patriaki Mar Awa III wa Kanisa la Wakatoliki wa Ashuru ya Mashariki,mjini Vatican kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 30 ya hati ya kiekumene na miaka 40 ya mkutano kati ya Patriaki Mar Dinkha IV na Papa Yohane Paulo II.Na wakati wa Mkutano huo,Papa alitangaza kumjumuisha Mtakatifu Isaka wa Ninawi,Askofu wa Ashuru wa karne ya 7 katika kitabu cha Mashahidi wa Roma.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kama ilivyokuwa tayari imetolewa taarifa , Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 9 Novemba 2024 amekutana na Patriaki wa Kanisa la Wakatoliki wa Ashuru ya Mashariki Mar Awa III, mjini Vatican kwa ajili ya kumbukumbu ya hati ya kiekumene na kumbukizi ya miaka 40 ya ziara ya kwanza ya Roma ya Patriaki wa Ashuru kumtembelea Mtakatifu Yohane Paulo II. Baba Mtakatifu Francisko akianza hotuba yake amebainisha kwamba: “Bwana wa nyakati […] katika siku za hivi karibuni ameanza kumimina toba ya ndani na hamu ya muungano kwa wingi zaidi katika Wakristo waliojitenga” (Hati ya Unitatis redintegratio, 1). Papa aliongeza: “Ninakumbusha yale maneno mashuhuri  ya Zizioulas, mtu wa Mungu, alivyosema: "Ninajua tarehe ya muungano, ninaijua," Ni ipi? “Siku moja baada ya hukumu ya mwisho. Kabla ya hapo hakutakuwa na muungano, lakini kwa sasa ni lazima tutembee pamoja, tusali pamoja na kufanya kazi pamoja. Hicho ndicho tunachofanya sasa,” Papa alisema. Akiendelea “Mtakatifu Yohane Paulo II alimkaribisha Patriaki  Mar Dinkha IV, katika tukio la mkutano wa kwanza rasmi kati ya Askofu wa Roma na Patriaki wa Kikatoliki wa Kanisa la Ashuru la Mashariki, miaka arobaini iliyopita, kama ulivyokumbuka hivi punde.”

Papa akiwa na Kundi lilimsindikiza Patriaki wa Kanisa la Ashuru
Papa akiwa na Kundi lilimsindikiza Patriaki wa Kanisa la Ashuru

Papa amesem, “Maneno hayo yalichukuliwa kutoka katika Hati ya Uekumene ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican  ya “ Unitatis redintegratio, ambapo Kanisa Katoliki linaadhimisha miaka sitini mwezi huu. Hatua kwa hatua,na  polepole. Ilikuwa ni "shauku ya umoja", ambayo Hati inarejea mara kadhaa (taz UR, 7), ambayo ilisukuma watangulizi wetu kukutana.” Hii "desiderium unitatis" yaani ni “shauku ya Umoja”, kulingana na usemi mzuri wa Mtakatifu Yohane Cassian (Collationes, 23, 5), ni neema ambayo imehamasisha harakati za kiekumene tangu asili yake na kwamba ni lazima daima kukuza. Kwa kuamshwa na Roho Mtakatifu, si kitu kingine isipokuwa shauku ya Kristo mwenyewe, iliyooneshwa katika Karamu ya mkesha wa Mateso yake, "ili wote wawe kitu kimoja" (Yh 17:21).

Patriaki MAR AWA III akisoma hotuba yake
Patriaki MAR AWA III akisoma hotuba yake

Baba Mtakatifu amemgeukia Patriaki huyo: " Ndugu mpendwa, ndiyo hasa “shauku  hiyohiyo ya umoja” ndiyo inayotuhuisha leo hii, tunapoadhimisha kumbukumbu ya miaka thelathini ya Makataba wa  pamoja wa Kikristo kati ya Makanisa yetu, ambao ulikomesha miaka 1500 ya mabishano ya kimafundisho kuhusu Mtaguso wa Efeso. Tamko hili la kihistoria lilitambua uhalali na usahihi wa matamshi mbalimbali ya imani yetu ya pamoja ya Kikristo, kama ilivyotungwa na Mababa katika Sala ya Kanuni ya  Imani ya Nikea. Mtazamo huo wa "hermeneutic" uliwezekana kwa kanuni ya kimsingi iliyothibitishwa na hati  ya upatanisho, yaani, kwamba imani ile ile, iliyokabidhiwa na Mitume, ilioneshwa na kukubalika kwa njia na mitindo tofauti kulingana na hali tofauti za maisha (taz. Unitatis redintegratio, 14). "Na hiyo ilikuwa kanuni muhimu." Ilikuwa ni Azimio la Pamoja la Kikristo lililotangaza kuanzishwa kwa Tume mchanganyiko ya majadiliano ya kitaalimungu kati ya Makanisa yetu, ambayo yameleta matokeo mashuhuri, pia katika ngazi ya kichungaji.”

Papa na mgeni wake Patriaki wa Ashuru
Papa na mgeni wake Patriaki wa Ashuru

Papa Francisko aidha amependa kukumbuka hasa mkataba wa 2001 juu ya ‘Anaphora ya mitume Addai na Mari, ambayo iliruhusu waamini husika, kuwa na mawasiliano fulani katika andiko la communicatio in sacris kwenye hali fulani; na kunako mwaka 2017 Tamko la Pamoja kuhusu "maisha ya kisakramenti." Hivi majuzi zaidi, miaka miwili iliyopita, hati ya  'Le immagini della Chiesa nelle tradizioni siriaca e latina' yaani 'Picha za Kanisa katika Mapokeo ya Kisiria na Kilatini' liliweka msingi wa kuelewa kwa pamoja katiba ya Kanisa. “Leo hii-  Papa ameongeza, kwa hiyo, nina fursa ya kuwashukuru ninyi nyote, wataalimungu wajumbe  wa Tume Mchanganyiko, kwa kujitolea kwenu. Hakika, bila kazi yenu, makubaliano haya ya mafundisho na ya kichungaji yasingewezekana.” Baba Mtakatifu Francisko pia amefurahishwa kuchapishwa kwa kitabu cha ukumbusho, chenye nyaraka mbalimbali zinazoashiria hatua za safari yetu kuelekea umoja kamili,” chenye utangulizi wa pamoja wa Patriaki huyo pamoja na Papa mwenyewe.

Kwa hakika, mazungumzo ya kitaalimungu ni ya lazima katika safari yetu kuelekea umoja, kwani umoja tunaotamani ni umoja katika imani, mradi tu mazungumzo ya ukweli hayatenganishwi na mazungumzo ya upendo na mazungumzo ya maisha: mazungumzo kamili ya binadamu. Umoja huo katika imani tayari umefikiwa na watakatifu wa Makanisa yetu. Wao ndio waelekezi wetu bora zaidi kwenye njia ya umoja kamili. Kwa sababu hiyo, kwa makubaliano ya Patriaki  huyo na Patriaki wa  Kanisa la Wakaldayo, na pia kutiwa moyo na Sinodi ya hivi karibuni ya Kanisa Katoliki juu ya sinodi, ambayo ilikumbusha kwamba mfano wa watakatifu wa Makanisa mengine ni “zawadi tunayoweza kupokea, tukiingiza kumbukumbu lao katika kalenda yetu ya kiliturujia” (Hati ya Mwisho, n. 122),Papa Francisko ameongeza “nina furaha kutangaza kwamba Isaka mkuu wa Ninawi, mmoja wa Mababa wanaoheshimika zaidi wa tamaduni ya  Siria-Mashariki, anayetambuliwa kama Baba  na mtakatifu kwa tamaduni zote, atajumuishwa katika kitabu cha Mashahidi wa Roma.”

Papa na mgeni wake wa Kanisa la Ashuru la Mashariki
Papa na mgeni wake wa Kanisa la Ashuru la Mashariki

Kwa maombezi ya Mtakatifu Isaka wa Ninawi, akiunganishwa na ya Bikira Maria, Mama wa Kristo Mwokozi wetu, Wakristo wa Mashariki ya Kati daima wamshuhudie Kristo Mfufuka katika nchi zinazoteswa na vita. Na urafiki kati ya Makanisa yetu uendelee kushamiri hadi siku yenye baraka tutakapoweza kusherehekea pamoja kwenye madhabahu moja na kupokea ushirika wa Mwili uleule na Damu ya Mwokozi, “ili ulimwengu upate kuamini” (Yh 17:21). Papa Francisko amemshukuru Patriaki huyo na kuombe kuendelea kutembea pamoja, kuomba pamoja na kufanya kazi pamoja, na tusonge mbele kwenye njia hii kuelekea umoja kamili." Papa amewashukuru tena kwa ziara hiyo. Ameomba wabaki pamoja katika kusali pamoja:  “Na sasa ninawaalika muombe pamoja sala ambayo Bwana Yesu alitufundisha, ya Baba Yetu. Kila mtu anapaswa kuomba kulingana na mapokeo yake na kwa lugha yake, kwa sauti ya chini," Papa alisema.

Papa na Patriaki AWA III
09 November 2024, 11:34