Papa akutana na Wanachama wa Shirikisho Vyama vya Kutoa damu lItalia:Furaha,ushuhuda na mshikamano!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 9 Novemba 2024 alikutana katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican na Wanachama wa Shirikisho la Vyama vya kutoa damu Itakia(FIDAS)katika fursa ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo. Papa Francisko katika hotuba yake alibainisha kwamba wamehuishwa na kujitolea kimya kwa maelfu ya wafadhili kote nchini. Papa Francisko amependa kutafakari nao kwa muda vipengele vitatu vya shughuli zao, kwanza furaha - kwa sababu amesema anavyojua kwamba wao ni mwenye furaha, ushuhuda na mshikamano. Furaha na chanya ni sifa za mara kwa mara katika mazingira ya kujitolea na kwa ujumla zaidi kati ya watu wanaojitolea kwa manufaa ya wengine. Wanaweza kuhisi hapo pia, kati yao, na sio kwa bahati mbaya,” Papa alisema.
Kutoa kwa upendo, kiukweli, huleta furaha. Yesu mwenyewe alisema hivi: “Ni heri kutoa kuliko kupokea” (taz Mndo 20:35). Sababu ni kwamba “tulifanywa […] kutoa upendo, kufanya mapenzi kuwa msukumo wa shughuli zetu zote” (Salamu za Papa Benedikto kwa vijana katika Kanisa Kuu la Westminster, 18 Septemba 2010). Zawadi hiyo inatoa furaha, kwa sababu ndani yake maisha yetu yote yanabadilika na kustawi, tukiingia katika msukumo wa Injili, ambamo kila kitu kinapata maana yake na utimilifu wake katika upendo. "Zawadi inatoa furaha, ishara hii ya ‘kutoa’ ambayo inakufanya uwe na furaha zaidi kuliko ishara hii ya 'kuchukua'. Ishara hii ya 'kutoa' hutufurahisha, Papa amekazia. Hii ni kuwapatia wengine kwa hiari sehemu muhimu yako mwenyewe, damu yako na hakika unakuwa unajua furaha inayotokana na kushiriki," Papa alisisitiza.
Pili Papa Francisko amesema ushuhuda. Kwa kufafanua amesema “Katika ulimwengu, tunajua, uliochafuliwa na ubinafsi, ambao mara nyingi huwaona wengine kama adui zaidi wa kupigana kuliko ndugu wa kukutana, kwa hiyo ishara yao isiyo na nia kinyume na isiyojulikana ni ishara inayoshinda kutojali na upweke, ya kushinda mipaka na kuvunja vikwazoa.” Mtoaji hajui damu yake itamwendea nani, wala mtu anayetiwa damu mishipani hajui kwa ujumla mfadhili wake ni nani. Na damu yenyewe, katika kazi zake muhimu, ni ishara fasaha: haiangalii rangi ya ngozi, wala uhusiano wa kikabila au wa kidini wa mtu anayeipokea, lakini huingia kwa unyenyekevu pale inapoweza, ikijaribu kufikia, na kukimbia, kupitia mishipa, kila sehemu ya kiumbe, na kuleta nguvu kwa yule aliyeipokea. Baba Mtakatifu ameongeza: “Hivi ndivyo upendo unavyofanya kazi. Na katika suala hili, ishara ya kupanua mikono, ambayo inafanywa wakati wa kutoa damu na ni muhimu. Ni sawa na vile Yesu alivyofanya katika Mateso yake, alipounyosha mwili wake msalabani kwa hiari. Ni ishara inayozungumza juu ya Mungu, na inatukumbusha kwamba "utume wa uinjilishaji wa Kanisa unapitia upendo" (tazam Mahburu ya Mtakatu Yohane Paulo II wakati wa kutangazwa Mwenyeheri mama Teresa wa Calcutta, 19 Oktoba 2003).
Hatimaye, Papa ameeleza mshikamano. “Wale wanaopokea damu hufika moyoni, kimwili, lakini pia kiroho: yaani, inafika kwenye "kituo cha kuunganisha cha mtu" (Waraka wa Kitume wa Dilexit nos, 55), ambapo "kujitukuza nafsi yako na kujithamini," uwazi kwa wengine" (ibid. 18), mahali pa ubora wa upatanisho na umoja.” Na katika suala hilo Papa amependa kuwaalika waishi tendo hilo la uchangiaji wa damu, pamoja na tendo la ukarimu wa kibinadamu, pia njia ya ukuaji wa kiroho katika njia ya mshikamano unaoungana katika Kristo, kama zawadi kwa Bwana wa Huruma anayejitambulisha na wale wanaoteseka.” Kufuatilia damu ili kufikia moyo Papa ameomba wasisahau hilo yaani, kuzidi kukumbatia kila mwanamume na mwanamke wanayekutana naye, kila mtu, katika upendo mmoja. Papa amewashukuru sana kwa kile wanachotenda na amewabariki wao na familia zao zote na wale wote wanaoshirikiana na Shirikisho lao. Amewahakikishia kuwakumbuka katika sala zake na pia ikiwapendeza wasisahahu kumuombea.