Papa Francisko:kuna utakatifu mwingi uliofichika ndani ya Kanisa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican kwa kuwageukia waamini na mahujaji waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, kushehereka siku kuu ya Watakatifu wote, tarehe Mosi Novemba 2024, alisema: “Leo, ni Maadhimisho ya Watakatifu Wote, ambapo katika Injili (taz Mt 5:1-12), Yesu anatangaza kitambulisho cha Mkristo na kitambulisho cha Mkristo ni kipi? Heri. Ni kitambulisho chetu na pia njia ya utakatifu (taz Waraka wa Kitume wa Gaudete et exsultate, 63).” Papa amesema kuwa “Yesu anatuonesha njia, ile ya upendo, ambayo Yeye mwenyewe alitembea kwanza kwa kuwa mwanadamu na ambayo kwetu sisi wakati huo huo ni zawadi kutoka kwa Mungu na yeye pia ni mwitikio wetu.
Papa Francisko amependa kuelezea mambo mabwili "Zawadi na majibu." Kwanza ni zawadi kutoka kwa Mungu, kwa sababu, kama Mtakatifu Paulo asemavyo, ni Yeye atakasaye (taz 1Kor 6:11). Na kwa sababu hiyo, kwanza kabisa, tunamwomba Bwana atufanye watakatifu, aifanye mioyo yetu iwe kama yake(Waraka wa kitume wa Dilexit nos, 168). Kwa neema yake hutuponya na kutuweka huru kutokana na kila kitu kinachotuzuia kupenda kama anavyotupenda (Taz Yh 13:34), ili ndani yetu, kama Mwenyeheri Carlo Acutis alivyosema, kuwa "siku zote nisijifikirie kwanza mimi, ili kuachia nafasi Mungu.”
Na hii inatupeleka kwenye sehemu ya pili ya majibu yetu. Papa alisema: “Baba wa mbinguni, kiukweli, hututolea utakatifu wake, lakini hatulazimishi. Anapanda ndani mwetu, hutufanya tuuonje na kuona uzuri wake, lakini basi unasubiri majibu yetu. Anatuachia uhuru wa kufuata maongozi yake mazuri, kujiruhusu kuhusika katika mipango yake, kufanya hisia zake kuwa zetu (taz Dilexit nos, 179), kujiweka wenyewe, na alitufundisha, kuwa katika huduma ya wengine, kwa upendo kama anavyoongezeka kwa wote, uwazi na kushughulikiwa kwa wote, uwazi na kushughulikiwa kwa ulimwengu mzima. Tunaona haya yote katika maisha ya watakatifu, hata katika wakati wetu.
Hebu tufikirie, kwa mfano, juu ya Mtakatifu Maximilian Kolbe, ambaye huko Auschwitz aliomba kuchukua nafasi ya mtu mwenye familia aliyehukumiwa kifo; au tumfikirie Mtakatifu Teresa wa Calcutta, ambaye alitumia maisha yake kuwahudumia maskini zaidi; au kwa Askofu Mtakatifu Oscar Romero, aliyeuawa altareni kwa kutetea haki za maskini dhidi ya unyanyasaji wa waonevu. Na kwa hivyo tunaweza kutengeneza orodha ya watakatifu wengi, sana wale tunawaheshimu kwenye madhabahu na wale wengine, ambao ninapenda kuwaita watakatifu wa mlango wa karibu”, hawa wa kila siku, waliofichwa ambao huendeleza maisha yao ya kila siku ya Kikristo.
Papa amesisitiza na kusema je ni kiasi gani cha utakatifu uliofichwa katika Kanisa!” Tunatambua kaka na dada wengi walioundwa na Heri za mlimani:maskini, wapole, wenye rehema, wenye njaa na kiu ya haki, wapatanishi. Hawa ni watu waliojaa Mungu, wasio na uwezo wa kubaki bila kujali mahitaji ya wengine; wao ni mashuhuda wa mapito angavu, yanayowezekana kwetu pia. Hebu tujiulize sasa: je, ninamwomba Mungu, katika sala, kwa ajili ya zawadi ya maisha matakatifu? Je, ninajiruhusu niongozwe na misukumo mizuri ambayo Roho wake anaivuvia ndani yangu? Na je, mimi binafsi hujitolea kutenda Heri za Injili, katika mazingira ninayoishi? Maria, Malkia wa Watakatifu Wote, atusaidie kuyafanya maisha yetu kuwa njia ya utakatifu.