2024.11.07 Papa akutana na Waseminari a Jimbo la Kikanisa la Toledo nchini Hispania. 2024.11.07 Papa akutana na Waseminari a Jimbo la Kikanisa la Toledo nchini Hispania.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa na waseminari wa Toledo:hamasisheni ukaribu na watu wa Mungu!

Baba Mtakatifu Fransisko akikutana na waseminari ambao watakuwa mapadre wa siku zijazo Novemba 7,amefafanua mlinganisho kati ya maisha ya kuwekwa wakfu na Sikukuu ya'Reservado'ambapo mnamo mwezi Novemba inaadhimishwa kumbukuzi la Sakramenti Takatifu iliyohifadhiwa katika hema la Kikanisa cha Seminari ya Toledo nchini Hispania.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 7 Novemba 2024 amekutana na Jumuiya ya Seminari ya Toledo, ambapo katika hotuba yake amefurahi kukutana nao ikiwa ni kundi jipya la waseminari, kama jumuiya ya Nchi ya Hispania, waliofika kwa maandamano hadi katika Kanisa Mama ili kufanya kituo cha Toba. “Toba au utalii? Lilikuwa ni swali la Papa na kubainisha alivyojiwa akilini mwake neno hilo, awali ya yote kwa sababu daima ni muhimu kutunza Watu watakatifu wa Mungu katika roho yake iliyo rahisi. Wao wanajua kuwa mapadre wanapaswa kuwa karibu, wanapaswa kuhamasisha ukaribu. Awali ya yote ukaribu wa Mungu kwa namna ya kwamba uwezo huu wa kukutana na Bwana unakuwa karibu na Bwana. Ukaribu wa pili ni wa maaskofu na maaskofu kuwa na ukaribu na Mapadre. Kuhani ambaye hayupo karibu na Askofu wake ni “kiwete” anakosa kitu. Tatu, ukaribu kati yao  mapadre, ambao wanaanza kujitayarisha katika seminari na nne, ukaribu na watakatifu, Watu  waaminifu wa Mungu.

Papa amekutana na waseminari wa Toledo
Papa amekutana na waseminari wa Toledo

Papa Francisko alisema anavyojua kwamba maandamano ya"Reservado" ambayo yanatayarishwa siku hizi ni Uamaduni wa zamani ambao unakumbusha kwa mara ya kwanza Sakramenti Takatifu ilipohifadhiwa, katika Hema la  kikanisa kidogo. Kwa njia hiyo "Tazameni mnavyo fanya wakati mnapiga magoti mkenda kuabudu." Maadhimisho haya ya kuvutia yanajumuisha nyakati tatu: adhimisho la Ekaristi, ufafanuzi wa Sakramenti Takatifu kwa siku nzima na hatimaye maandamano. Hatua hizi zinaweza kutumika kutukumbusha mambo msingi ya ukuhani ambayo wanatayarisha papa amesema.

Waseminari na Papa Francisko
Waseminari na Papa Francisko

Akianza kudadavua Papa amesema "Kwanza, adhimisho la Ekaristi." Ni Yesu anayekuja katika maisha yetu ili kutupatia uthibitisho wa upendo mkuu zaidi. Linatualika, kama Kanisa, uwepo katika ukuhani na katika watu, katika sakramenti na katika Neno. Kuwa naye duniani na kumwilisha maisha yao na moyo wao. Kisha, Bwana anabaki wazi katika monstrance siku nzima. Ni wakati wa kuwa pekee pamoja naye, kusikia sauti yake katika ukimya, katika kusikiliza Neno, katika ushuhuda wa imani ya wale wanasali  karibu nao.  Ni katika kukutana tu mtu na mtu, kukutana kwa upendo na Yesu kunaweza kuakisi na, kudumisha mwendo wa siku yetu ya kidunia. Mkutano huo na uwe msukumo madhubuti unaobadilisha uwepo wao.

Hatimaye, kuna hatua ya kubeba Bwana kwa maandamano, kwa sababu" tunampokea ili kumbeba, huduma yetu ni kuandamana na Kristo kuelekea kwa watu wake,na watu kuelekea Kristo." Na wao bila kuondoa mitazamo yao kutoka kwa Yeye anayetuongoza, tujifunze kutembea pamoja kwa matumaini ya kukutana ambapo tayari tunatazamia hapa kwa njia ya sakramenti." Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha.

Papa alikutana na waseminari wa Toledo, Hispania
07 November 2024, 16:22