Papa,marehemu makardinali na maaskofu:Walikuwa wachungaji na vielelezo vya kundi la Bwana!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu ameongoza Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 4 Novemba 2024 akisaidiwa na makardinali wengine kuanzia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, makardinali na maaskofu na waalimini wengi, kwa ajili ya kuombea marehemu Makardinali na Maaskofu waliofariki ndani ya mwaka 2024. Baba Mtakatifu Francisko ameanza mahubiri yake na kifungu cha Injili ya Luka iliyosomwa, kinachojikita na kusulibiwa kwa Yesu Msalabani na majambazi wawili ambapo ilisikika sauti ya ikisema: “Yesu, unikumbuke utakapoinga katika Ufalme wako”(Lk 23,42). Haya ni maneno ya mwisho yaliyoelekezwa kwa Bwana, kutoka kwa mmoja wa wawili waliosulibiwa naye. Siyo mfuasi aliyeyatamka, yaani mmoja wa wale ambao walimfuata Yesu kwenye njia za Galilaya na kushirikishana naye mkate wa Karamu Kuu. Siyo. Kinyume chake aliyemwelekea Bwana alikuwa ni jambazi. Mmoja wa aliyekutana naye tu, katika mwisho wa maisha; mmoja wa wale ambao wala hatujuhi jina. Pumzi za mwisho za mgeni huyo, lakini katika Injili yanageukua kuwa mazungumzo yaliyojaa ukweli. Wakati Yesu anahesabiwa miongoni mwa waovu(Is 53,12) kama alivyokuwa ametabiri Isaya, inasikia sauti isiyotarajiwa ambayo inasema: “ Tunapokea kile tunachostaili kwa sababu ya matendo yetu; yeye kinyume hake hakufanya ubaya wowote(Lk 23,41).
Na ndivyo ilivyo. Na mhukumiwa huyo anawakilisha sisi sote, tunaweza kumwambia jina letu. Hasa, tunaweza kufanya maombu yetu kama yake: “Unikumbuke Yesu.” Nifanye niwe katika kumbu kumbu yako.” Usinisahau.” Baba Mtakatifu amesema tutafakari tendo hilo la “kumbuka, na kukumbuka. Kukumbuka maana yake ni “kupeleka tena katika moyo”, kuweka katika moyo. Mtu huyo, aliyesulibiwa na Yesu, anabainisha uchungu mkali katika sala: “ Nipokee katika moyo wako, Yesu.”Na hamwombi kwa sauti ya kuhuzunisha, kama yule aliyeshindwa, badala yeke kwa sauti kamili ya tumaini. Na ndicho hicho ambacho anatamani huyo jambazi ambaye anakufa kama mtume wa saa ya mwisho: anatafuta moyo wa kukaribishwa. Na hilo ndilo jambo kuu kwake, kwa kuwa sasa yuko uchi kabla ya kifo. Na Bwana husikiliza maombi ya mwenye dhambi, hadi mwisho, kama kawaida. Akiwa umetobolewa na maumivu, moyo wa Kristo unafunguka, na unafunguka kuokoa ulimwengu - moyo wazi, usiofungwa: unakaribisha, anayekaribia kufa, na sauti ya wale wanaokufa. Yesu anakufa pamoja nasi, kwa sababu anakufa kwa ajili yetu. “Anakufa pamoja nasi, kwa sababu anakufa kwa ajili yetu,” Papa amekazia mara mbili kusema.
Msalabani asiye na hatia anajibu wito wa msulubiwa hatiani kwamba: “Amin, nakuambia, leo utakuwa pamoja nami mbinguni” (Lk 23:43). Kumbukumbu ya Yesu ni ya ufanisi, kwa sababu ni tajiri katika huruma, na kwa sababu hii ni ya ufanisi. Ingawa maisha ya mwanadamu yanashindwa, upendo wa Mungu huachilia huru kutoka katika kifo. Kisha aliyehukumiwa amekombolewa; mgeni anakuwa mwenzi; kukutana kwa muda mfupi msalabani kutadumu milele kwa amani. "Hii inatufanya tufikirie kidogo.” Papa amesisitiza. Je, ninakutanaje na Yesu? Au bora zaidi, ni jinsi gani ninamruhusu Yesu akutane nami? Je, ninajiruhusu kukutana au ninajifungia katika ubinafsi wangu, katika maumivu yangu, katika utoshelevu wangu? Ninahisi kama mwenye dhambi kwa kujiruhusu kukutana na Bwana au ninahisi kuwa mwenye haki na kusema: “Hunitumikii. Endelea? Yesu anatukumbusha wale waliosulubishwa karibu naye, mpaka pumzi yake ya mwisho, inatufanya tutafakari: kiukweli kuna njia ya kukumbuka watu na vitu. Unaweza kukumbuka makosa, kumbuka biashara ambayo haijakamilika, kumbuka marafiki na wapinzani.
Papa amesisitiza kuwa: “hebu tujiulize leo hii mbele ya tukio hili kutoka kwa Injili: je, watu wako mioyoni mwetu? Je, tunawakumbukaje wale wanaopita karibu nasi katika matukio yote ya maisha? Je, ninahukumu? Je, ninagawanya? Au ninawakaribisha? Baba Mtakatifu amesema kwa kugeukia moyo wa Mungu, watu wa siku hizi na pia watu wa nyakati zote wanaweza kutumaini wokovu, hata kama “ilionekana machoni pa wapumbavu kuwa wanakufa” ( Hekima 3:2 ). Kwa hakika kumbukumbu ya Bwana huhifadhi historia nzima. Kumbukumbu imetunzwa. Yeye ndiye hakimu mwenye huruma na rehema. “Bwana yu karibu nasi ahukumu; yuko karibu, mwenye huruma na mwenye upole. Hii ndiyo mitazamo mitatu ya Bwana. Je, niko karibu na watu? Je, nina moyo wa huruma? Je! nina upole?”
Kwa imani hii, tuwaombee Makardinali na Maaskofu waliofariki katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita. Leo kumbukumbu yetu inakuwa kwa hawa ndugu zetu. Washiriki waliochaguliwa wa watu wa Mungu, walibatizwa katika kifo cha Kristo (rej. Rm 6:3), kufufuka tena pamoja naye. Walikuwa wachungaji na vielelezo vya kundi la Bwana (rej. 1 Pt 5:3): sasa wakae mezani pake, baada ya kuumega chini Mkate wa uzima. Papa amesema kwamba “Wao “Walipenda Kanisa, kila mmoja kwa njia yake, lakini wote walipenda Kanisa: tuombe ili wafurahie ushirika wa watakatifu milele. Na tungojee, kwa tumaini thabiti, kufurahi pamoja nao Mbinguni. Kwa kuongezea: “Na niwaalika mseme pamoja nami mara tatu: “Yesu, utukumbuke!” Kila mtu. “Yesu utukumbuke, Yesu tukumbuke, Yesu Utukumbuke Yalikuwa ni maneno yake ya mwisho ya Baba Mtakatifu Francisko.