Tafuta

Watu kadhaa waliuawa baada ya mwavuli wa zege kuporomoka katika kituo cha Reli cha Novi Sad nchini Seribai Ijumaa Mosi Novemba 2024. Watu kadhaa waliuawa baada ya mwavuli wa zege kuporomoka katika kituo cha Reli cha Novi Sad nchini Seribai Ijumaa Mosi Novemba 2024.  (ANSA)

Uchungu wa Papa Francisko waathirika wa ajali ya Novi Sad

Papa ametuma telegramu kwa Rais wa Serbia Aleksandar Vučić akielezea mshikamano na sala kwa waathirika wa kuangukia na kibanda katika kituo cha Treni.Ni ajali iliyotokea Ijumaa tarehe 1 Novemba 2024.

Vatican News

Walikuwa ni wasafiri wanaosubiri au wafanyakazi  wa kila siku katika usafiri, wameketi kwenye majukwaa yenye watu wengi, na wengine ndani wakinunua tiketi za treni. Karibu na adhuhuri, ghafla na ya kutisha, paa la zege juu ya mlango wa kuingilia lilianguka! Hivi ndivyo mkasa wa Novi Sad, nchini Serbia, ulivyotokea siku ya Ijumaa tarehe Mosi Novemba 2024, ambapo watu 14 waliangamia katika ajali hiyo pamoja na wengine watatu kujeruhiwa vibaya.

mmoja akiwasha mshumaa kuwaomba marehemu
mmoja akiwasha mshumaa kuwaomba marehemu

Ukaribu wa Papa kwa taifa la Serbia

Baba Mtakatifu Francisko baada ya kupata taarifa hizo  alitaka kuwa karibu na watu wa Serbia kwa kumwandikia telegramu Rais Aleksandar Vučić wa Jamhuri ya nchi hiyo ambapo anabainisha  kwamba yuko karibu na taifa katika "wakati huu mgumu" na kwamba anaombea "hasa marehemu, familia zao zinazoomboleza na kwa  wote waliojeruhiwa ”, huku akihakikisha ukaribu wake wa kiroho.

Maandamano na kukamatwa

Baadhi ya sehemu za kituo hicho zilikuwa zimefanyiwa ukarabati hivi karibuni kwa njia ya mwendo kasi, lakini paa hilo halikuathiriwa na kazi hizo. Siku chache baada ya mkasa huo, maelfu ya watu waliandamana huko Novi Sad na pia kulikuwa na maandamano na ghasia karibu na kituo hicho, jambo ambalo lilichochea hisia za polisi kufyatua  mabomu ya machozi na kukamatwa kwa wengine. Kuanguka kwa paa hilo kulisababisha kujiuzulu kwa Waziri wa Miundombinu na Uchukuzi Goran Vesic.

watu walifanya maandamano
watu walifanya maandamano
Salamu za rambi rambi za Papa kwa ajili ya waathirika wa Serbia
06 November 2024, 17:56