Ukimya wa Papa katika kumbukizi ya marehemu wote na sala kwa watoto Malaika

Papa Francisko ameadhimisha liturujia tarehe 2 Novemba 2024 kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu wote katika makaburi ya Laurentina,eneo la Castel di Decima. Kabla ya sherehe,alisimama kwenye "Bustani ya Malaika",eneo lililotengwa kwa ajili ya mazishi ya watoto ambao hawajawahi kuona nuru ya dunia ambapo alisali mbele ya makaburi yaliyozungukwa na michezo ya watoto na kumsalimia baba aliyefiwa na binti yake.Katika Misa hakuna homilia,lakini kutafakari na sala kimya.

Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.

Mama mmoja alikuwa akiandika kwa kutumia rangi, alama ya maandishi kwenye jiwe la kaburi la binti yake, ambaye alifariki akiwa na umri wa chini ya mwaka mmoja; Mwingine akiwa anabadilisha maji ya maua yaliyowekwa kwenye vyungu laini na kokoto zilizonakishiwa. Baba mmoja, Stefano, kinyume chake alioneakana akisafisha jiwe  lenye nyota na kuandikwa jina la msichana wake mdogo Sara, ambaye ujauzito wake ulikatizwa akiwa na majuma kumi na moja mnamo Julai 2021. Haya ni matukio yasiyo ya asili, kwa sababu yanaeleza hasa wazazi ambao wanomboleza vifo vya watoto wao wachanga, na ambao licha ya uchungu wao waliweza kumkaribishwa kuwasili kwa Baba Mtakatifu katika Makaburi ya Laurentino, eneo la Castel di Decima, Roma mahali ambapo Papa  kwa mara ya pili baada ya 2018,  amechagua tena kuadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu wote, tarehe 2 Novemba 2024.

Kusimama kwenye Bustani ya Malaika

Kituo cha kwanza, kama tayari ilivyokuwa miaka sita iliyopita, kilikuwa ni “Bustani ya Malaika, yaani eneo la takriban 600 m2 lililowekwa kwa ajili ya mazishi ya watoto ambao hawakuwahi kuzaliwa wakiwa hai, au kuzaliwa na baadaye kufariki mara kwa sababu ya upotezaji wa ujauzito au shida zingine wakati wa ujauzito. Kwa mfano Thomas, Mattia, Maria, Giuseppe, Andrea, Ariana: majina yao yamechongwa kwa mawe au kwenye jiwe la mbao, na wakati huo kuchonga au kuandikwa kwa rangi ya dhahabu. Wengi wana neno fetus(ikiwa na maana ya umbu) kabla ya majina yao, karibu safu nzima ya mbele ilikuwa imemilikiwa na watoto wa mwaka huu 2024. Karibu ya makaburi hayo kuna midoli laini vya wahusika wa utengenezaji wa Katuni za (Disney au katuni zingine, puto, pinwheels,)na vitu vingine vyote ambavyo hata hivyo vimechafuliwa na matope ya mvua. Hivi ni vitu ambavyo vinataka kurudisha tabasamu mahali pa machozi. Kwa njia hiyo Papa aliwasili karibu saa 3.45 asubuhi masaa ya Ulaya  kwa gari, akitembea kando kando ya ukanda mrefu ambapo, kwa upande mmoja, kulikuwa na kuta za makaburi ya  ya manispaa, ya tatu kwa ukubwa Jijini Roma; kwa upande mwingine, uwanja huo wenye watu mamia elfu walikusanyika tangu asubuhi na mapema chini ya jukwaa ndogo nyeupe ambapo Baba Mtakatifu aliadhimisha Misa.

Mbele ya makaburi ya watoto

Baada ya kuwasili kwenye “Bustani ya Malaika,” Papa akiwa katika kiti cha magurudumu alitembea kwenye ukanda mzima wa ardhi akiangalia mawe ya kaburi moja baada ya nyingine. Alisimama katikati na kubaki peke yake kwa dakika chache katika sala ya ukimya. Zaidi ya hayo, ni maneno gani ya kueleza? Aliyasema hayo mwenyewe katika ujumbe wa hivi karibuni kwa njia ya  video wa nia ya maombi ya mwezi wa Novemba 2024, ambayo ni maalumu kwa akina mama na akina baba wanaopitia mateso makali ya kufiwa na mtoto wa kiume au wa kike.“Maneno ya faraja, wakati mwingine, yanapingana au ya hisia na hayana faida. Hata kama yanasemwa kwa nia njema kabisa, yanaweza kuishia kuongeza jeraha,” Papa alisema kwenye video hiyo.

Mkutano na Stefano

Wakati wa kutafakari ulikatizwa na mazungumzo mafupi na Stefano ambaye amekuwa akimngoja Papa kila wakati kando ya bustani. Alipiga magoti alipofika na kumpa mkono, alimwambia kwa ufupi historia yake na kuonesha kaburi la mwanawe. Papa Francisko alitikisa kichwa na kuminya mkono wake, kisha alichukua barua ambayo mtu huyo alimkabidhi. Mara baada ya hapo Papa alihamia eneo la mbele, ambalo pia limetengwa kwa ajili ya mazishi ya watoto walioaga dunia mapema mno. Baadhi ya jamaa ilikuwa ni vikwazo, lakini hata salamu kwa busara, kulikuwa na kushikilia vyungu na maua katika mikono yao. Papa aliweka fungu la Maua ya  waridi nyeupe chini ya kaburi lenye kuandikwa: “Bustani ya Malaika,” kuzungukwa na midoli nyingine laini, na  sanamu za Malaika, nyingine za uso wa Kristo, Cinderella ya mto nk.

Salamu kwa Meya Gualtieri

Kwa gari la Papa Francisko alielekea jukwaani, akimulikwa na jua la Kiroma la tarehe 2 Novemba 2024.  Kivuli kilikuwa na ukuta mkubwa wa matofali meupe na uandishi wa Neno la Vita mutatur non tollitur. Watu walimkaribisha Baba Mtakatifu  kwa kelele za chinichini za “Papa oyee” zikiongozwa na upendo lakini wakifahamu mahali na tukio. Baba Mtakatifu Francisko alisalimiana kwa ufupi waamini, akiwalenga hasa wagonjwa katika viti vya magurudumu, vilivyowekwa mstari wa mbele. Alipofika alikaribishwa na meya wa Roma, Roberto Gualtieri, ambaye alimpatia mkono na kubadilishana maneno machache.

Muda wa kutafakari wakati wa Misa

Ujio wa wanafamilia wanaokwenda kuwatembelea na kuwasalimia wapendwa wao waliofariki uliendelea kwa muda mrefu zaidi na baadaye kila kitu kilisimama na kuanza kwa maadhimisho ya Misa. Wakati wa homilia Papa alikaa kimya, akiwa ameinamisha kichwa chake, katika kutafakari na sala. Baadaye kulifutika maombi ya liturujia ya siku: “Bwana, uwepo wetu wa duniani ni pumzi tu, utufundishe kuhesabu siku zetu, utupe hekima ya moyo ambayo inatambua wakati wa kifo sio mwisho bali mapito ya maisha.” Kisha aliwabariki wote waliokuwapo na kuinua sala ya haki na baraka kwa wale ambao wameondoka duniani na kumwomba Mungu kwa ajili ya faraja kwa wale wanaopata mateso ya kuondokewa wapendwa wao. Sala ya 'Raha ya Milele Uwape Ee Bwana' pia na kusindikizwa na makofi kutoka kwa umati katika kuhitimisha sherehe hiyo. Kabla ya kuingia kwenye gari kurudi Vatican  Papa alisimama haraka na waamini waliokuwapo. Vile vile tena salamu nyingine kwa Meya Gualtieri na baraka kwa tumbo la  mama  mjamzito zinahitimisha wakati huo.


Salamu kwa “Cheche za Matumaini”

Wakati huo huo, katika uwanja kulikuwa na "Scintille di Speranza" yaani “cheche za matumaini”  waliokusanyika hawa ni  kikundi cha akina mama wote wameunganishwa kwa sababu ya kupoteza mwana au binti mdogo sana kwa sababu tofauti. Hao waliungana tena baada ya Jubilei ya Huruma kwa shukrani kwa Yesu Mfufuka, parokia ya makaburi, ambayo - walisema - “ilitupatia tumaini la ufufuko na kukubalika, jambo pekee tunalohitajika, pamoja na kushiriki uchungu. Wacha tuone maumivu yetu pamoja." Kuna mayatima, wajane, kwa wazazi kama sisi, wanawake wanaeleza, "hakuna neno linalotutambulisha". Wanajitambulisha kwa kuchanganya jina lao na la mtoto wao: Francesca, mratibu, mama wa Giorgia ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 15, Caterina mama wa Marina, Maria Teresa wa Daniele, Shanti wa Marco, na kisha Roberta aliyepoteza Claudio, mama mwingine wa Roberta wa Chiara, Nazarena mama wa Chiara na Angela wa Cinzia. Wote  hawa walimpatia Papa kitambaa cheupe: "Ni kumbatio la joto kwa ajili yake, kukumbatiwa kwa ishara pia kutoka kwa watoto wetu", walieleza, wakimshukuru Papa kwa ukimya wake "mzito na wenye heshima” wakati wa Misa na kwa uwepo wake kwenye Makaburi ya Laurentino: “Ushuhuda wa upendo. Njia kuu ya kuwa karibu na watoto wetu."

Misa ya 2 Novemba katika makaburi

 

02 November 2024, 11:45