Ujumbe wa Papa kwa wafungwa wa Sollicciano:Ninawakumbatia nyote
Vatican News
Katika Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko aliowatumia wafungwa wote wa gereza la Florentine la Sollicciano, ambao ulizomwa mara baada ya Ibada ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa tarehe 19 Desemba 2024 alasiri na Askofu Mkuu Gherardo Gambelli wa Firenze, Italia Papa anabainisha kuwa: “Napenda kuwakumbatia wafungwa wote ninaowahakikishia ukaribu wangu wa kibinadamu na wa kiroho. Ninawaalika daima kumtumaini Mungu, Baba mwema na mwenye huruma.” Liturujia hiyo iliadhimishwa na Kardinali Ernest Simoni, wa Albania mwathirika wa mateso na utawala wa kikomunisti, aliyealikwa na Askofu mkuu kuungana naye katika ziara ya Noeli katika jela.
Kwa njia hiyo alipoarifiwa kuwepo kwa Simoni, Papa Francisko alimtumia ujumbe ili awafikishie wafungwa. “Sote tunamkaribisha Yesu aliyezaliwa na anaijaza mioyo yetu tumaini na matumaini. Ninawatakia Noeli Takatifu na mwaka mpya wenye amani, kwa moyo mkunjufu ninatoa baraka zangu za baba kwenu, kwa ndugu walio gerezani, kwa familia zao na kwa wafanyakazi wa magereza. Ninawakumbatia kila mtu na ninawaomba, tafadhali, mniombee."
Mahubiri ya Askofu mkuu
Katika mahubiri yake, Askofu mkuu kuhusu Injili ya siku aliwapatia wafungwa tangazo la matumaini, ujumbe mkuu wa Jubilei ya 2025, na kurejea uzoefu wa maisha ya Kardinali Simoni, aliyekamatwa usiku wa Noeli ya 1963 na kupelekwa jela ya Scutari huku Albania ambako alipata mateso mengi: "Kadinali Simoni aliteseka kwa miaka 28 ya kifungo na kazi ya kulazimishwa, mwathirika wa mateso ya utawala wa kikomunisti nchini Albania. Uwepo wake kati yenu leo unaibua mateso ya pamoja, unaonesha kuwa utu wa mtu lazima uheshimiwe kila wakati katika haki, lakini zaidi ya yote. inashuhudia kwamba nguvu ya imani hututegemeza hata katika nyakati za huzuni na kuweza kuushinda uovu," alisisitiza.
"Kuzaliwa kwake Yesu tutakaosherehekea siku chache kulifanyika katika hali ngumu, ya dhuluma, ya umaskini, lakini Mungu aliyefanyika mwili alileta nuru kwa historia yetu sote", alisema Askofu Mkuu huyo ambaye alikuwa Padre wa Sollicciano kabla ya kuteuliwa kuwa askofu mkuu wa Firenze. "Tumaini letu liko katika uhakika kwamba Bwana kamwe hatutupi katika taabu na makosa yetu, ikiwa tuko tayari kuongoka na kumkaribisha. Kwa kumwamini Yeye, jela inaweza kuwa mahali ambapo tunaweza kupata amani mioyoni mwetu."