Papa Francisko:Matufe ni mchezo mzuri wa urafiki wa kijamii
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akikutana Ijumaa tarehe 20 Desemba 2024, alifurahi kukutana na, wawakilishi wa Shirikisho la mchezo wa Matufe wa Italia, pamoja na Rais wa kimataifa na baadhi ya mamlaka za kiraia, ambao amewashukuru kwa uwepo wao. Papa Francisko alibainisha anavyopenda sana mchezo wa Matufe. Kwa sababu mbili: ya kwanza, kwa sababu ni mchezo maskini, ukilinganishwa na wale wa nyota wenye mikataba ya mabilioni ya dola, ambao daima hujaza vyombo vya habari.
Nadhani mabingwa wa mchezo wa matufe ni watu ambao ni wafanyakazi, au walimu, au mafundi bomba. Kwa kifupi, watu wa kawaida ambao wana shauku ya mchezo huu, labda nje ya mtindo, lakini ni matajiri katika ubinadamu. Papa ameonesha sababu ya Pili ya kuondolea kwake mchezo wa matufe kuwa ni mchezo ambao ninashirikishana na aina fulani ya urafiki, ya urafiki wa kijamii. Hapo zamani ilikuwa umeenea sana katika vijiji, katika ulimwengu wa vijijini, kila mahali kulikuwa uwanja wa matufe hata katika maparokia.
Ilikuwa ni njia ya kuwa pamoja, ya kutumia muda katika ushirikai, furaha ya afya na amani. Kwa bahati mbaya, jamii imebadilika, na hivyo pia mchezo wa boce: wanawake na vijana pia hucheza; Watu wengi wenye ulemavu wanafanya mazoezi, na ninawapongeza kwa haya yote. Papa Francisko amewapongeza kwa matokeo waliyoyapata kama Shirikisho kwa kiwango cha ushindani; na zaidi ya yote kwa sababu wanaendeleza mchezo huu mbadala ikilinganishwa na mashine kubwa ya biashara ya michezo, mchezo unaojumuisha, ambao bado una ladha ya "mchezo" na kampuni nzuri. Papa amewabariki kwa moyo wote na shughuli zao. Na tafadhali wasisahau kumuombea.