Papa:Jubilei ya Wagonjwa:hata katika udhaifu,Mungu hatuachi peke yetu

Katika mahubiri ya Papa yalisomwa na Askofu Mkuu Fischella,Mwenyekiti mwenza wa Baraza la Kipapa la Unjilishaji katika fursa ya Jubilei ya Wagonjwa na Ulimwengu wa kiafya,tarehe 6 Aprili 2025 ambapo Papa ameomba tusiwaweke pembeni walio dhaifu na maumivu yao mbali na maisha yetu.Ni matarajio ya Papa kushiriki na wagonjwa wakati huu uzoefu wa udhaifu,wa kujisikia dhaifu na wa kutegemea msaada wa wengine.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Dominika ya V ya Kwaresima  ikiwa ni fursa ya Jubilei  ya Wagonjwa na ya Ulimwengu wa Kiafya, Dominika tarehe 6 Aprili 2025, majira ya saa 4.30 asubuhi masaa ya Ulaya, ikiwa ni saa 5.30 mchana masaa ya Afrika Mashariki na Kati, katika Uwanja wa Basilika ya Mtakatifu Petro mjini Vatican, imeadhimisha Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu Mkuu Salvatore Fisichella, Mwenyekiti Mwenza katika Kitengo cha Masuala msingi ya Uinjilishai  Ulimwenguni wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na Mwakilishi wa Baba Mtakatifu Francisko katika tukio hilo. Baada ya Somo la Kwanza kutoka Nabii Isaya 43, 16-21: tazama mimi nafanya mapya na kuwapatia watu wangu wenye kiu, Somo la Pili, kutoka kwa Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi, 3, 8-14 na Injili kutoka Yohane 8, 1-11: Asiye na thambi kati yenu awe wa kwanza kutupa jiwe, kuhusiana na Mwanamke mzinzi,  Askofu Mkuu Fisichella kabla ya kusoma Mahubiri ya Papa alisema kuwa: “ Kaka na dada, mlioko mita chache kutoka kwetu, Papa Francisko, kutokea chumba chake huko Mtakatifu Marta, yuko karibu sana nasi na anashiriki kama wagonjwa wengi, watu wengi dhaifu, katika Ekaristi Takatifu kwa njia ya televisheni. Nina furaha na heshima kubwa sana kutoa sauti yangu kusoma mahubiri ambayo ametayarisha kwa ajili ya tukio hili.”

Jubilei ya wagonjwa na wahudumu wa kiafya
Jubilei ya wagonjwa na wahudumu wa kiafya   (Vatican Media)

Aliendelea kusoma, mahubiri yalioandaliwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili yao, kutokana na yeye kuendelea kupata nafuu katika makazi yame Mtakatifu Marta mjini Vatican  kwamba “Tazama, nitatenda jambo jipya, sasa litachipuka, je hamtalijua sasa,”(Is 43,19). Ni maneno ambayo Mungu  kwa njia ya nabii Isaya anawaelekea watu wa Israeli walihamishwa huko Babilonia. Kwa waisraeli ni kipindi kigumu utafikiri kila kitu kimepotea. Yerusalemu ilichukuliwa na kuharibiwa na wanajeshi wa Mfalme Nebukadreza II na watu wakachukuliwa, hakikubakia chochote. Upeo unaonesha kufungwa, wakati ujao wenye giza, kila tumaini ni bure. Kila kitu kinaweza kupelekea waliohamishwa wajiachilie na kujikabidhi kwa uchungu na kuhisi hawakubarikiwa hata kidogo na Mungu. Licha ya hayo, ni katika mutadha huo, ambapo mwaliko wa Bwana ni kupokea jambo jipya ambalo linakaribia kuzaliwa.  Si jambo litakalokuja wakati ujao. Bali ni lile ambalo tayari linatokea, ambalo liko linachanua kama chipukizi. Je hiki ni kitu gani? Ni kitu gani kinaweza kuzaliwa, na zaidi kinaweza kuwa tayari kimechipua katika uwanda uliopweke na mahangaika kama hayo?

Ni maswali, ya  Baba Mtakatifu ambaye ameendelea kubainisha  kuwa “kile ambacho kinazaliwa ni Watu wapya, Watu ambao waliangukia na uhakika wa uongo wa wakati uliopita. Wakagundua kile ambacho ni muhimu cha “Kubaki wamoja na kutembea pamoja katika nuru ya Bwana(Is 2,5). Watu ambao wanaweza kujenga upya Yerusalemu kwa sababu, walikuwa mbali na Mji Mtakatifu, na Hekalu ambalo lilikuwa limeharibika sasa. Bila kuwa na uwezo wa kuadhimisha liturujia kuu, walijufunza kukutana na Bwana kwa namna nyingine, ile ya “uongofu wa Moyo(Yer 4,4), katika kutekeleza sheria na haki, katika kuwajali maskini na wahitaji( Yee 22,3) na katika matendo ya huruma.

Jubilei ya wagonjwa
Jubilei ya wagonjwa   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Ni ujumbe huo huo ambapo kwa namna tofauti, tunaweza kuupokea hata katika sehemu hii ya Injili (Yh 8,1-11).  Hata hapa kuna mtu, mwanamke mmoja, ambaye maisha yake yameharibika: si kwa ajili ya umbali wa kijiografia, lakini aliyehukumiwa kimaadili. Ni mdhambi, na kwa hiyo yuko mbali na sheria na amehukumiwa na taasisi ya sheria na kwa kifo. Hata yeye utafakiri kwake hakuna tena tumaini. Lakini Mungu hakumuacha. Badala yake ni wakati ambao washitaki wake walipokuwa wameshikiria mawe mikononi mwao, ndipo pale Yesu aliingia katika maisha yake,  alimtetea na kumwondoa ndani ya vurugu zao, kwa kumpatia uwezekano wa kuanza tena maisha mapya akimwambia  “nenda, zako huko huru, umeokolewa(Yh 8,11). Katika simulizi hii kubwa na ya kusisimua, liturujia inatualika leo hii kupyaisha, imani katika Mungu  safari ya Kwaresima, ambaye daima yuko karibu  nasi ili kutukomboa. Hakuna utumwa, wala vurugu, wala dhambi, na wala aina yoyote ya maisha ambayo inaweza kumzuia kukaa karibu na mlango wetu na kubisha hodi, tayari aweze kungia pale tu tunapomruhusu (Ap 3,20). Na zaidi, hasa wakati majaribu yanapokuwa magumu zaidi, neema yake na upendo wake unatulazimisha tena kuwa wenye nguvu zaidi kutuinua.

Jubilei ya wadhaifu

Baba Mtakatifu Francisko kwa njia hiyo anakazia kwamba: “sisi tunasoma maandiko haya wakati tunaadhimisha Jubilei ya Wagonjwa na ya Ulimwengu wa kiafya, na kwa hakika ugonjwa ndiyo moja ya majaribu magumu zaidi, na magumu ya maisha, ambayo tunagusa kwa mkono kwa wale ambao ni wadahifu. Hayo yanaweza kutufanya kufikia kuhisi kama watu waliohamishwa, au kama mwanamke katika Injili: ambaye hakuwa na tumaini la wakati ujao. Lakini si hivyo. Hata katika wakati huo, Mungu hatuachi peke yetu, na ikiwa tunajikabidhi kwake, na hasa pale ambapo nguvu zetu zinakosa, tunaweza kufanya uzoefu wa faraja ya uwepo wake. Yeye mwenyewe, aliyefanyika binadamu alipenda kushirikisha yote katika udhaifu wetu (Fil 2,6-8) na anajua vizuri ni nini maana ya mateso(Is 53, 3). Kwa hiyo kwake Yeye tunaweza kusema na kumkabidhi uchungu wetu, kwa hakika ya kupata huruma, ukaribu na upole. Na si hiyo tu. Katika upendo wake aminifu, kiukweli, Yeye anatuhusisha ili tuweze kugeuka kwa mara nyingine tena, “malaika”, kwa mmoja na mwingine,  wapeleka habari za uwepo wake, kiasi kwamba, mara nyingi awe anayeteseka na awe anayehudumia, kitanda cha mgonjwa kinaweza kubadilika kuwa “mahali patakatifu,” pa wokovu na ukombozi.

Jubilei ya wagonjwa na ulimwengu wa kiafya
Jubilei ya wagonjwa na ulimwengu wa kiafya   (Vatican Media)

Baba Mtakatifu katika muktadha huo  amewageukia wahudumu wa kiafya kwamba “wapendwa  manesi, na wahudumu wote wa kiafya, wakati mnawahudumia wagonjwa wenu, hasa wadhaifu zaidi, Bwana anawapatia fursa ya kujipyaisha kila siku maisha yenu, kwa kumwilishwa na shukrani, ya huruma  na ya matumaini ( rej. Spes non confundit, 11). Anawaita kutia nuru kwa unyenyekevu kwa utambuzi kuwa hakuna cha bahati mbaya na kila kitu ni zawadi ya Mungu; kwa kumwilishwa na ubinadamu ule ambao mnafanya uzoefu, mnapoacha tabia za kijuu juu, na kubaki na  kilicho cha muhimu yaani ishara kubwa au ndogo za upendo. Mruhusu kwamba uwepo wa wagonjwa waingie kama zawadi katika maisha yenu, ili kuponesha moyo wenu, kuutakasa kwa yote ambayo si upendo na kuwashwa kwa moto unaowaka na huruma  tamu. Baba Mtakatifu hakukosa kuelezea hali yake kwamba: niko nanyi pia wapendwa kaka na dada, wagonjwa, katika wakati huu wa maisha yangu ninashirikishana nanyi sana: uzoefu wa ugonjwa, kujihisi mdhaifu, kutegemea wengine kwa mambo mengi, na kuwa muhitaji wa msaada. Siyo rahisi daima, lakini ni shule ambayo tunajifunza kila siku kupenda na kuacha kupendwa bila majivuno na bila kukataa, bila majuto na bila kuhangaika, kwa shukrani kwa Mungu na kwa ndugu kwa ajili ya wema tunaoupokea, kwa kujikabidhi na imani kwa kile ambacho bado kinaweza kutokea.

Askofu Mkuu Fisichella
Askofu Mkuu Fisichella   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Chumba cha hospitali na chumba cha kuugulia vinaweza kuwa mahali ambamo unahisi sauti ya Bwana anayesema hata sisi “Tazama, nitatenda jambo jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa?(Is 43,19). Na ndivyo hivyo kujipyaisha na kukuza imani. Papa Benedikto XVI ambaye alitupatia ushuhuda mkubwa wa utulivu katika kipindi cha ugonjwa wake, aliandika kuwa: “kipimo cha ubinadamu kimsingi huamuliwa katika uhusiano na mateso” na kwamba “jamii ambayo haiwezi kukubali wale wanaoteseka [...] ni jamii katili na isiyo ya kibinadamu,”(Soma Barua ya kitume ya Spe salvi, 38). Ni kweli: kukabiliana pamoja mateso kunatufanya kuwa binadamu zaidi na kushirikishana uchungu ni hatua muhimu ya kila safari ya utakatifu. Papa Francisko anasisitiza kwamba tusimfungie aliye mdhaifu mbali na maisha yetu, kama ilivyo kwa bahati mbaya leo hii,  wakati mwingine kuna aina fulani na mawazo, kutaka kuzuia maumivu kutoka katika  mazingira yetu. Zaidi ya hayo tufanye kuwa fursa ya kukua pamoja, ili kukuza matumaini, shukrani kwa upendo ambao yeye  alikuwa  wa kwanza Mungu kujitoa  kwa ajili yetu (Rm 5,5) na ambaye zaidi ya yote, ndicho kile kinachobaki daima ( 1Kor 13,8-10.13).

Maombi ya Ulimwengu kwa lugha mbali mbali

Baada ya mahubiri, ukimya, sala ya nasadiki, na maombi. Wakati wa maombi yalisomwa kwa lugha mbali mbali: Lugha ya “Tagalog inayozungumzwa nchini Ufilippino: “Baba wa huruma , uongoze Kanisa lako la kihija, katika ulimwengu, ili uhuhudia kwa ujasiri Kristo, msulibiwa na mfufuka kwa ajili ya wokovu wetu.” Kwa kislovakia: “Baba Mtakatifu, uangaze kwa neema yako watawala wa mataifa ili wahamasisha kila hali ya hadhi ya mtu binadamu;” Kwa Kireno: “Baba wa huruma nyingi, watie nguvu wale ambao wanateseka katika mwili na katika roho, ili wachote kutoka katika mateso ya Kristo nguvu ya faraja.” Kwa lugha ya Kiromania” Baba mwema, uwasaidie wahudumu wa kiafya, ili waweze kuwapatia faraja wale ambao wanaisha katika mateso na katika uchungu;” Kichina: “Baba Mwenyezi, ongoza familia yako iliyoungana katika upendo wako ili katika maadhimisho ya Ekaristi iweze kuwa sadaka hai inayokupendeza wewe.”

Mahubiri ya Papa katika fursa ya Jubilei ya wagonjwa
06 Aprili 2025, 15:25