Ask.Grech:Sinodi ni kona ya umisionari kwa ajili ya Kanisa lote duniani!
Na Sr. Angela Rwezaula, - Vatican.
Mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu mwambata wa Sinodi ya Maaskofu kunako tarehe 2 Oktoba 2019 alinzia mara moja uzoefu wa Sinodi ya Amazonia Askofu Mario Grech kuwa karibu na Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu. Kufuatia na hiyo Aksofu anasimulia uzoefu wake na kushirikisha tafakari juu ya kiini na ukuu wa mkuranoi unaojikita ndai ya hduma na matendo ya Kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko. Katika uzoefu huo yeye anathitisha ukweli wa kile ambacho Baba Mtakatifu anapenda kusema kwamba hali halisi ya maisha inaonekana vema pembezoni kuliko watu wanaoishi katikati! Na hii ina maana ya hali halisi ya kijamaii na kiutamaduni kwa ajili ya uzoefu wa kikanisa anasisitiza Askofu Grech. Anakumbuka ni kwa jinsi gani maaskofu wa Brazil na kama wao pia walivyojifunza sana kutokana na kusiliza wenzao. Na kwamba japokuwa walikuwa wanatoka katika kanda moja, lakini kulikuwa na mambo mengi ambayo yalikuwa hayajulikani kati yao ya uzoefu na ulazima wa kusikiliza wengine. Na kwa maana hiyo uzoefu wa Sinodi ulikuwa muhimu kwa wale wanaotoka katika eneo hilp pamoja na wale ambao wanahisi kuwa wako katikati! Iwapo mmoja anasikiliza baadhi ya uzoefu uliojitokeza na si tu kutambua namna ya kupanda mbegu za watu wote na wingi wa Kanisa uliopo katika utumaduni, bali hata kiini cha makosa makubwa ambayo wengi wanafikiria kuwa juu ya watu hao.
Aidha kijibu kuhusu hisia alizopata mara baada ya kuteuliwa siku chache kabla ya Sinodi hiyo ya Amazonia anasema kuwa yeye anatoka katika jimbo dogo ambalo lakini lina nguvu sana ya kimisionari. Katika miaka yake ya mafunzo kwenye seminari, walikuwa wanawambia kwamba “«the world is my parish». "Yaani dunia ni parokia yangu". Na bila kujua tangu hawali ya kwamba Bwana alikuwa anamwandalia huduma mpya ambayo katika maoni yake inahusu ukuu wa kimisionari. Akiendelea kufafanua anasema hata kama Vatican siyo ardhi ya umisionari, lakini anafikiri kwamba kutumwa na Baba Mtakatofu kama utume kimisionari katika mantiki ya kuwa Katibu mwambata wa Sinodi ina maana ni kona ya njia inayopelekea katika njia nyingine kati ya Mabaraza ya Maaskofu duniani kote; na vile vile Sinodi ya Maaskofu ni zana ya uinjilishaji. Na kama Baba Mtakatifu anavyoandika kuwa: “katika kipindi ambacho Kanisa linajifafanua kwenye hatua ya uinjilishaji na ambao inataka kuunganisha kanda zote za ulimwengu kwenye utume mkubwa wa kimisionaro, Sinodi ya Maaskofu inaalikwa kama ilivyo kila taasisi ya Kanisa kuwa daima mkondo mwafaka kwa ajili ya uinjilishaji wa dunia ya sasa (Ec, 1).
Sinodi kwa hakika ndiyo ufunguo wa neno la huduma ya Kipapa na kwa maoni yake ni kwa nini ukuu wa sinodi ni muhimu wa Baba Mtakatifu? Askofu kwamba, maoni na mawazo ya Baba Mtakatifu kuhusu sinodi una mizizi yake katika aina za Watu wa Mungu. Hii ina maana ya uthibitisho katika kwenye sanduku la Baba Mtakatifu ambalo linabeba: Taalimungu ya watu, tunda la utambuzi unaobubujika katika Mtanguso wa II wa Vatican na hata juu ya uzoefu wake kama Askofu wa watu wa Buenos Aires. Watu ndiyo moyo wa uzoefu wa kichungaji na taalimungu yake, pia talimungu ya Kanisa ndiyo tunda la uzoefu wa kuwa katikati ya Watu wa Mungu. Katika mwanga wa hivyo Kanisa halijitambushi kama hirakia, bali katika Watu wa Mungu wakiwa na wajumbe wake maaskofu, watu waliowekwa wakfu na walei , ambao pamoja na karama zao tofauti wanapewa hadhi sawa kutokana na Ubatizo huo huo (LG12). Mungu huwawekea waamini wote maumbile ya imani (sensu fidei) ambayo huwasaidia kutambua kile kinachotoka kwa Mungu. Kuwepo kwa Roho anaye huwapatia Wakristo umoja fulani na hali halisi ya Kimungu na hekima inayo waruhusu kuvielewa kwa asili, ingawa hawana zana zinazofaa kuelezea wazi. (Eg, 119). Kwa kufikiria kuwa maandiko yake kuhusiana na ushauri wa waamini, Mtakatifu John Henry Newman alikuwa ameboresha tafakari, tena juu ya maana ya waamini (sensu fidei ambayo baadaye ilishawishi hata Mtaguso wa II wa Vatican (DV 8, LG 129: hata suala la kutangazwa kwake mtakatifu wakati wa Sinodi kuhusu Amazonia, ilikuwa inawakilisha fursa ya dhahabu kwa ajili ya tafakari ya kina juu ya maana ya waamini na ambayo kwa maono yake ilikuwa imeachwa pembeni.
Ni namna gani ya kutafakari kwa kina kuhusu mambo mawili ya taasisi ya sinodi iliyonzishwa na Papa Paulo VI kutokana na zana ya kisikiliza watu wa Mungu na Muungano wa Maaskofu? Katika katiba ya kitume Baba Mtakatifu anatoa mantiki kwa ajili ya kuimarisha mchakato wa majadiliano kati ya maaskofu na Watu wa Mungu na ili hiyo ya mwisho kuhakikisha nafasi pana ya ushiriki katika Kanisa, ule mchakato kwa ngazi kuu ya ushirikishwaji kati ya muungano wa waamini (communio fidelium), muungano wa maaskofu (communio episcoporum, na muungano wa kanisa (communio ecclesiarum). Kwa hakika anathibitisha Askofu Grech kwamba wakati anakubali kwamba Sinodi ya Maaskofu kimsingi ni mkutano wa maaskofu wa kukuza mazungumzo na ushirikiano kati ya maaskofu na kati ya maaskofu na Askofu wa Roma, lakini hiyo haipaswi kutengisha na watu wa Mungu, kwa sababu “maisha ya Kanisa na maisha ndani ya Kanisani ni hali ya utume na mazoezi ya kila Askofu kufundisha. Sinodi ya maaskofu lazima iwe zana mwafaka wa kusikiliza Watu wa Mungu. Maaskofu anayeishi katikati ya waamni wale ana maskio yaliyfunguka kwa ajili ya kisikiliza kile ambacho Roho anasema kwa Kanisa ( Mdo (Ap, 27) ni sauti ya konoddo na haya kwa njia ya viungo vya kijmbia ambavyo vina shughuli ya kushuri Askofu, kuhamasisna mazungumzo halisi na kujenga (Ec 5).
Na Baba Mtakatifu Francisko alisema katika hotuba yake ya jubilei ya miaka 50 tangu kuanzisha kwa Sinodi ya Maaskofu kuwa mkutano wa maaskofu unawapatia mfumo mzuri zaidi wa kutafsiri kwa ajili ya kuelewa huduma hiyo hiyo ya kihierarkia. Na ikiwa tunaelewa hiyo, kama alivyosema Mtakatifu John Chrysostom, “Kanisa na Sinodi vinafanana, kwa sababu Kanisa syio kitu chochote zadi ya kutembea pamoja , kama zizi la Mungu kwenye njia za historia, ili kukutana na Kristo Bwana, aidha tunaelewa pia kuwa ndani yake hakuna mtu anayeweza kuinuliwa juu ya wengine. Kinyume chake, katika Kanisa ni lazima kwamba mtu ajiishushe kwa ajili ya kujikita mwenyewe katika hatua za huduma ya ndugu.