Jumamosi 29 Okotba alitangaza Sr Maria Berenice Duque Hencker kuwa Mwenyeheri nchini Colombia. Jumamosi 29 Okotba alitangaza Sr Maria Berenice Duque Hencker kuwa Mwenyeheri nchini Colombia. 

Mwenyeheri Maria Berenice Duque Hencer na sifa ya unyenyekevu

Jumamosi 29 Oktoba huko Medellín,Colombia,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu aliongoza misa takatifu kwa ajili ya kumtangaza mwenyeheri mpya,mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa kike wa Kupashwa Habari.Katika mahubiri yake alibainisha wasifu wake ambao ulimfanya kufanana na Mama wa Yesu,kwa namna ya kuishi kwa imani kati ya wasiwasi na matatizo na upendo wake kwa ajili ya maskini na watoto.

Na Angella Rwezaula; Vatican.

Unyenyekevu ndio ilikuwa fadhila kuu zaidi iliyotia alama ya maisha ya Sr. Maria Berenice Duque Hencker, Mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa Kupashwa Habari habari aliyeishi kati ya karne ya XIX na XX, na ambaye alitangazwa kuwa mwenye heri katika Kanisa Kuu la Bikira Maria msafi wa Moyo huko Medellín, nchini Colombia, Jumamosi tarehe 29 Oktoba 2022. Kardinali  Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu, akiwakilisha Baba Mtakatifu katika Misa ya kumtangaza mwenyeheri huyo katika  mahubiri alieleza kuwa katika mchakato wake uliopelekea sifa ya kumfikisha altareni, ambaye zamani alikuwa anaitwa Anna Giulia, wataalimungu washauri  walikubaliana kwa kumfafanua kuwa ‘mnyenyekevu’. Hii ni muhimu sana kwa sababu msingi wa fadhila zote za kikristo ni unyenyekevu. Mtakatifu Agostino alikuwa anasema: Je unataka kuwa juu? Anza kujinyenyekeza kwa kuanzia chini. Ikiwa unafikiri kujenga nyumba juu ya utakatifu, andaa kwanza msingi wa unyenyekevu.

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu alimtangaza Sr Maria Berenice Duque kuwa Mwenyeheri
Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu alimtangaza Sr Maria Berenice Duque kuwa Mwenyeheri

Akiwa na wasiwasi mkubwa Sr. Mdomenikani, ambaye alikuwa na asili ya Salamini na ambaye mnamo 1943 alianzisha familia mpya ya kitawa, alikuwa  ni yule wa kusaidia waliobaguliwa na jamii na kujibu mahitaji ya dhati ya watu.  Alikuwa na upendo wa kupeleka ujumbe wa Yesu hadi miisho ya dunia na kwa  kusukumwa na mwamko wa kimisionari alitaka izaliwe jumuiya hata nchi nyingine. Kardinali Semeraro alikumbusha kuwa Sr. Maria Berenice daima alikuwa na mfano wake Bikira Maria Mpashwa habari na ambaye aliweza kujikita naye kwa kuanzisha shirika la kwanza la watawa wanaoitwa watawa wa Mpashwa Habari. Yeye mwenyewe aliishi kila siku kwa yaliyo ya lazima tu kwa kujifikiria mdogo, takataka, na wa bure. Katika mahubiri yake, Kardinali Semeraro alijikita kutazama masomo ya liturujia ambapo yaliweza kwenda sambamba na sura ya Bikira Maria na ile ya Sr. Maria Berenice.

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu alimtangaza Sr Maria Berenice Duque kuwa Mwenyeheri
Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu alimtangaza Sr Maria Berenice Duque kuwa Mwenyeheri

Bikira Maria ni mfano katika kuhisi daima mdogo mbele ya ukuu wa utume ambao uhahisiwa kukabiliana nao na ambao alitangaziwa na Malaika Gabriel, alibaki mnyenyekevu na kujieleza Mtumishi wa Bwana, alijibu kwa maneno ya unyenyekevu na kubaki daima mnyenyekevu. Kufuatia na hilo, Kardinali Sermararo alitaja kifungu cha maneno ya Papa Francisko aliyosema wakati wa sala ya Malaika wa Bwana mnamo tarehe 24 Septemba 2017 kwamba: “Maria hakujikweza mbele ya matarajio ya kuwa Mama wa Masiha, lakini alibaki kawaida na kijielezea kujitoa kwake katika mpango wa Bwana. Maria hakujidai. Ni mnyenyekevu na wa kawaida. Na wakati Malaika alipoondoka kutoka kwake, Maria alibaki peke yake na fumbo la umama”, alisisitiza Kardinali.

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu alimtangaza Sr Maria Berenice Duque kuwa Mwenyeheri
Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu alimtangaza Sr Maria Berenice Duque kuwa Mwenyeheri

Na kumbe inahitaji kuishi imani, ambayo kama alivyoicha kwa ajili yetu na kwa ajili ya ubunifu wetu. Mungu kiukweli anatuacha daima huru, alisema Kardinali na kuongeza kwamba, kuishi imani haina maana ya kuwa lisiti ya shida, lakini ni kutafuta kila mara  jibu moja kibinafsi, kwa kufikiria mitindo wa Mungu na kupokea wito wake katika historia. Huo ndio utakatifu. Sr Maria Berenice alisema kwamba alitafuta siku hadi siku, iwe shida, mateso, na kushinda majaribu, jinsi ya kujibu Mungu, kati ya mapingamizi na kutoeleweka. Lakini alikuwa na mfano mzuri wa Bikira Maria, ambaye alimwiga hata kwa upendo kuelekea kwa maskini ambapo ilikuwa ni kitovu cha maisha yake na hata ili wao waweze kuinjilishwa alianzisha familia ya kitawa. Upendo kwa namna ya pekee ulikuwa ni kwa ajili ya watoto wenye shida ambao alikuwa akiwafikiria kama wapendwa Bwana. Alimini kabisa kwamba wao ndio ufalme wa mbingu, alihitimisha Kardinali kwamba Ufalme wa Mungu unaanzia hapa duniani kwa mambo madogo sana.

Mwenyeheri mpya Sr Maria Berenice huko nchini Colombia
30 October 2022, 15:05