Wakimbizi nchini Ukraine Wakimbizi nchini Ukraine 

Vatican:Wakimbizi wanahitaji kuwa na mpango wa amani wa kudumu!

Katika hotuba yake kwaUNHCR,mjini Geneva,Francesca Di Giovanni,katibu Msaidizi wa Kitengo cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ya Sekretarieti ya Vatican,alithibitisha kwamba,hasa katika mazingira ya vita kama hivi sasa,wahamiaji wengi mno hawawezi kuunganishwa pia kwa sababu ya sera ambazo hazipendekezi mapokezi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Vita nchini Ukraine vimefanya jambo la mapokezi kuwa la kuvunja moyo zaidi. Lakini katika hali halisi, idadi kubwa ya wakimbizi wanaendelea kupotea katika hali ya sintofahamu, na hawawezi kurejea nyumbani au kujumuika katika nchi zao za hifadhi. Pia kwa sababu, jumla ya migogoro, baadhi ya nchi zimeamua zaidi baadala ya kukaribisha, wanaonelea bora kuwakabidhi wengine kuwafanyia, kwa mujibu wa mkakati usio endelevu wa utumiaji wa kazi na kwa hivyo kuepuka kuwajibika moja kwa moja katika mtiririko mkubwa wa mchanganyiko kupitia makubaliano ambayo inazuia katika maeneo ya kimkakati ya njia yao.

Ndiyo picha halisi iliyojionesha katika Baraza la Kitaifa linavyoielekeza kwa upya wakati wa kikao cha 73 cha Kamati ya Utendaji la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kinachoendelea mjini Geneva kuanzia tarehe 10 hadi tarehe 14 Oktoba 2022. Na aliyewasilisha maono ya Vatican  ni Francesca Di Giovanni, katibu Msaidizi wa  sekta ya Kimataifa ya Kitengo cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ya Sekretarieti ya Vatican ambaye alisisitiza umuhimu mkubwa wa kutambua njia mbadala kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa wakati na kudumu kwa ajili ya kuwasaidia wale wanaohama kwa nguvu katika kutafuta hifadhi mpya.

Kwa maneno yake, yamekuwa mwangwi wa Papa katika mwito wa kukomesha mapigano barani  Ulaya Mashariki, na kwa hali inayofafanuliwa kuwa sio endelevu na bado ambayo haiwezi kuepukika. Katika kuwashukuru wale waliofanya kazi ya kuwapa wahamiaji ardhi mpya, Di Giovanni alibainisha kuwa Migogoro na hali ya muda mrefu ya wakimbizi haiwezi kuwa kawaida mpya' Wakimbizi na watu waliohamishwa  ni wanadamu na kwa hivyo ni chini ya haki na wajibu, sio vitu vya usaidizi. Ukosoaji pia unatolewa katika mbinu ya 'ichukue au iache' inayotumiwa na baadhi ya wajumbe, hata katika ofisi nyingine za Umoja wa Mataifa, kuhusu jinsi ya kudhibiti jambo hilo.

Mtazamo ambao, anasema mwakilishi wa Vatican unadhoofisha utashi wa kisiasa na umoja wa pande nyingi. Matumaini ni kurejea kwenye mazungumzo kwa nia njema na dhamira ya kuona mbali zaidi kuliko kuzingatia tu kutoa usaidizi huku tukipuuza 'dalili' za migogoro mbalimbali ambayo familia ya kibinadamu inapaswa kukabiliana nayo wakati huu. Jitihada hizo, ni kuhakikisha hali muhimu ili watu waweze kuishi kwa amani, usalama na heshima katika nchi zao za asili lakini pia kuhama kutoka kwa mikakati ya nguvu za kisiasa, kiuchumi na kijeshi hadi mpango wa kimataifa wa amani na kukuna kuwa na ulimwengu uliogawanyika kati ya mamlaka zinazogombana; na iwe ndio kwa ulimwengu ulioungana kati ya watu na ustaarabu unaoheshimiana, alihitimisha Di Giovanni.

 

11 October 2022, 13:05