Tafuta

 Papa Pio XII. Papa Pio XII. 

Mkutano:'Hati mpya za Upapa wa Pio XII na maana katika uhusiano wa Kiyahudi na Kikristo'

Katika Chuo Kikukuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma,Mkutano wa Kimataifautafanyika kuanzia tarehe 9-11 Oktoba 2023 ukiongozwa na mada: “Hati mpya za Upapa wa Pio XII na maana yake kwa ajili ya uhusiano wa Kiyahudi na Kikristo:mazungumzo kati ya Wanahistoria na Watalimungu.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika taarifa kutoka Ofisi ya Mawasiliano na habari ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana imebainisha kuwa kuanzia tarehe 9 hadi 11 Oktoba 2023 utafanyika mkutano wa Kimataifa katika Ukumbi mkuu wa Chuo Kikuu  hicho ukiongozwa na mada: “Hati mpya za Upapa wa Pio XII na maana yake kwa ajili ya uhusiano wa Kiyahudi na Kikristo:mazungumzo kati ya Wanahistoria na Watalimungu”.

Katika tarifa yao, inabainisha kwamba hii ni kutokana na kwamba mnamo mwezi Machi 2023, Baba Mtakatifu Francisko aliruhusu uwezekano wa kufikia hati milioni kadhaa  zinazohusiana na Upapa wa Pio XII (1939-1958), ambazo zote zina  uwezo wa kuchunguzwa kwa njia nyingi, muhimu zote mbili katika masuala ya kihistoria na kitaalimungu. Utafiti huu utachukua miongo kadhaa ya uchunguzi na uchanganuzi ili kubaini thamani halisi ya kumbukumbu hizi, inayokadiriwa kuwa angalau kurasa milioni 16. Hata hivyo, baadhi ya uvumbuzi muhimu uko tayari kushirikishwa na umma kwa ujumla.

Kutokana na hiyo, Mkutano wa Kimataifa  kuhusu  Hati Mpya za Upapa wa Pio XII na Maana Yake katika Mahusiano ya Kiyahudi na Wakristo: Mazungumzo Kati ya Wanahistoria na Wataalimungu” utajikita kumulika jinsi gani kumbukumbu hizi zinavyotoa mwanga juu ya mabishano ya kihistoria na kitaalimungu kuhusu Papa Pio XII na Vatican wakati wa kipindi cha mauaji ya kimbari na juu ya mahusiano ya Wayahudi na Wakristo katika ngazi mbalimbali kama vile kutoka kwa  wasio wataalamu hadi wale walio na nyadhifa za mamlaka katika duru za maamuzi na katika taasisi za Kiyahudi na Kikatoliki.

Katika mwaka wa 1965, kwa hakika, Kanisa Katoliki lilipyaisha mafundisho yake kwa kutumia Hati ya Mtaguso ya Nostra Aetate, ambamo kuna maelezo zaidi ya tangazo linaloshutumu chuki dhidi ya Wayahudi na kuwaonesha Wayahudi kuwa wamebarikiwa na Mungu. “Je nyaraka mpya zinaweza kutuambia nini kuhusu makabiliano ambayo yalisababisha wakati huo muhimu katika mafundisho mapya ya Kanisa? Litakuwa ni swali kubwa na hivyo Mkutano huo utawaleta pamoja wanahistoria na wataalimungu, Wakristo na Wayahudi, ambao wanajifunza pamoja ili kuongeza ujuzi wa kihistoria na mahusiano ya Kiyahudi-Kikristo.

Tukio hilo litakuwa wazi kwa umma na vyombo vya habari vilivyoidhinishwa. Taarifa zaidi, pamoja na taratibu za kujiandikisha kwa ajili ya mkutano huo, zitasambazwa mwezi Septemba. Kwa hitaji lolote wasiliana na Dk. Paolo Pegoraro (Ofisi ya Habari na Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana: press@unigre.it).

12 July 2023, 17:02