Vatican,Kard.Krajewski amehitimisha utume Nchi Takatifu
Konrad Krajewski
Akirejea kutoka katika utume wake katika Nchi Takatifu, kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, Kardinali Krajewski ameandika tafakari yake akiakisi juu ya uzoefu alioishi kwenye mipaka ya vita huko Gaza ambapo anasema katika Baba Yetu, Yesu anasema: “Mapenzi yako yatimizwe na Ufalme wako ufike,” wakati mwanadamu anafuata mapenzi yake na malengo yake tu mateso na migogoro mara nyingi hutokea." Ifuatayo ni tafakari ya uzoezo huo na ushuhuda wa Kardinali Krajewski kuwa: "Nilikwenda kwenye Nchi Takatifu kwa imani na sala, mahali ambapo vita vinaendelea, ambapo kuna chuki, kuna kulipiza kisasi, mahali ambapo mtu anaua mwingine, ambako kuna ukosefu wa maji, chakula, na ambapo hakuna umeme.
Hata wakati wa Noeli, siku takatifu zaidi kwetu, hawakuacha kupigana, kuua, huko Ukraine kama hata Ukanda wa Gaza. Nilifika katika nchi hii nikiwa na silaha za hali ya juu zaidi ulimwenguni, yaani, imani na sala, ambazo zinaweza kufanya isogee milima kila wakati na kwa hivyo kumaliza migogoro ... Lakini kwa nini sio hivvyo?
Nimekwenda sehemu zote ambapo Yesu aliishi. Nimekuwa Nazareti, Bethlehemu, nimefika mahali aliposulubishwa, akauawa kisha alipofufuliwa, ninajiuliza: “Bwana, mbona hakuna amani? Unataka amani.” Nimefikiria kila mara juu ya sala hii: “Utuokoe, Bwana, kutoka katika maovu yote, utupatie amani katika siku zetu” ... Basi kwa nini usitupatie amani katika siku zetu?
Sisi watu labda tumejiweka mahali pa Mungu na tunataka kuamuru, kulaani lakini tunafanya bila huruma, bila upendo. Labda hii ndiyo sababu hakuna amani, kwa sababu hatusujudu tena mbele za Mungu, mbele ya fumbo. Jana ilikuwa sikukuu ya Mtakatifu Yohane Mtume, alifika kwenye kaburi la Yesu na akainama ili aweze kuingia, aweze kuona kuwa mwili wake haupo, kwamba amefufuka. Lakini leo hatuinami tena, hata kama milango ya hapa katika Nchi Takatifu inatuambia kwamba tunapaswa kufanya hivyo ili kuelewa siri ya Mungu, kuelewa upendo wake, huruma yake, kuishi sawasawa na mantiki ya mafundisho ya Yesu, yaani kwa mantiki ya Injili.
Ninamshukuru Bwana kwa kuishi siku hizi katika Nchi Takatifu na kuanza kuelewa siri ya Mungu, sala ya Baba yetu, sala ambayo Yesu alitufundisha, inasema, “Mapenzi yako yatimizwe, Bwana”", sio yangu, kwa sababu tangu mapenzi yangu kuna vita, kuna vifo vingi.” Ufalme wako uje,” si wetu, ufalme wa uharibifu ni wetu. “Jina lako litukuzwe, sio langu, jina langu linapotakaswa mimi ni hatari kwa wengine. Baada ya Baba Yetu, kuhani anasema: |Ee Bwana, utuokoe na mabaya yote, utupatie amani siku zetu.” Matumaini yangu ni kwamba amani istawi kweli katika mioyo ya wanadamu.