Kardinali Parolin Katibu wa Vatican akiwa na Jumba la Giustiniani Roma  na Senet Ignazio La Russa. Kardinali Parolin Katibu wa Vatican akiwa na Jumba la Giustiniani Roma na Senet Ignazio La Russa.  (ANSA)

Kard.Parolin,Mashariki ya Kati:wasiwasi kwa mzozo unaowaka moto

Katibu wa Vatican, akiwa kando ya hafla katika Seneti juu ya Kadinali Achille Silvestrini,alitoa maoni juu ya mashambulio ya hivi karibuni katika Bahari Nyekundu na Erbil:ikiwa hatua za kukabiliana hazitachukuliwa,mzozo utaenea.Alizindua upya ombi la Papa kwa kazi iliyopo Davos ya uchumi jumuishi na wa kijamii.

Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula - Vatican

Katibu wa Vatican, Kardinali  Pietro Parolin alionekana kuwa na  wasiwasi mkubwa katika mashambulizi ya hivi karibuni katika Bahari Nyekundu yaliyofanywa na waasi wa Houthi, kuongezeka kwa ghasia huko Gaza na pia shambulio la makombora la Iran huko Erbil, huko Kurdistan ya Iraq. Hofu, yake ni kwamba ikiwa hatua kinyume na hayo hazitachukuliwa, ni kupanuka,  na kuongezeka kwa mzozo. Kwa kukumbuka yale ambayo Papa Francisko alielezea  uchungu wake wakati wa Katekesi kwamba ni moja ya mambo ya msingi na kwamba “mzozo huu haupaswi kuenea” alisema hayo Kadinali katika mazungumzo na baadhi ya waandishi wa habari tarehe 17 Januari 2024,  kando ya tukio moja kwenye Jumba la Giustiniani, katika Seneti, Roma lililokuwa linatazama sura ya  Kadinali Achille Silvestrini asiyesahaulika kwani alikuwa mkuu wa ujumbe wa Vatican kwa ajili ya marekebisho ya Mkataba wa Laterano na serikali ya Italia  mnamo tarehe 18 Februari 1984.

Kardinali Parolin akiwa na viongozi wa Seneti Italia
Kardinali Parolin akiwa na viongozi wa Seneti Italia

Kardinali Parolini alisema: “Hatari iko pale, roho zina shauku sana na hali ni tete... Ni lazima tuhakikishe kwamba kila mtu anajaribu kudhibiti hisia zake ili kusiwe na moto wa jumla.” Alisema hayo kwa uhakika hasa kwa kutazama mzozo kati ya Israel na Hamas, na  alithibitisha kile ambacho Vatican inakazia hasa kuhamasisha suluhisho la watu wawili, na mataifa mawili.  Na kuhusu dhana ya kihistoria ambayo Hamas, kupitia maneno ya kiongozi wake wa nje Khaled Meshal, ilisema inaikataa kabisa,  Kardinali Parolin alisema: “Kwa sisi, hata hivyo, watu wawili, nchi mbili zinaendelea  kuhamaishwa ili kuwa na  suluhisho. Ni muhimu pia kutafuta njia ya kufanya mazungumzo ili kweli itendeke.”

Kujitolea katika mwelekeo wa kibinadamu nchini Ukraine

Kwa  upande wa Ukraine, Kardinali Parolin alionesha pia wasiwasi wa hatima yake na kusisitiza tena kuhusika kwa Vatican  kwa ajili ya suluhisho la amani: “Hata kama tutajiwekea kikomo, angalau hadi sasa, kwa mwelekeo wa kibinadamu, ni mojawapo ya mambo  10 msingi ya kile kinachojulikana kama jukwaa la amani la Zelensky linahusika na misaada ya kibinadamu na hapo ndipo Vatican  inazingatia juhudi zake.” Alisema Kardinali Parolin. Kuhusu mkutano wa ngazi ya juu wa amani ulioombwa na Rais Zelensky mwenyewe huko Davos, ambapo alizungumza kwenye Jukwaa pia  la Uchumi la Dunia, lililoanza tarehe 16 Januari 2024, Kardinali Parolin alifafanua kuwa, “kama katika matoleo matatu yaliyopita (ya hivi karibuni zaidi nchini Saudi Arabia), Vatican itashiriki: “Sasa mwakilishi wa kudumu huko Geneva, Monsinyo Ettore Balestrero, aliyeteuliwa na Sekretarieti ya Vatican, anashiriki katika mkutano huo.”

Uchumi shirikishi na wa kijamii

Akiwa bado katika mawazo ya  Jukwaa la Davos, Katibu wa Vatican alizindua wito  kwa upya wa wyale yaliyokuwamo katika ujumbe uliotumwa kwa washiriki  hao na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Januari 2024 yaani wa kujitolea katika: "uchumi shirikishi na wa kijamii" ambao ingawa unadhibitiwa na vigezo vya kiuchumi, “ni muhimu kwamba mataifa na wafanyabiashara waungane katika kukuza mifano ya utandawazi yenye mtazamo wa mbali na yenye maadili mema, ambayo kwa asili yake lazima ihusishe kuweka chini katika kutafuta madaraka na faida ya mtu binafsi, na iwe hivyo kisiasa au kiuchumi, kwa manufaa ya wote ya familia yetu ya kibinadamu,tukitoa kipaumbele kwa maskini, wahitaji na wale walio katika mazingira magumu zaidi.”

Wakristo wanaoteswa: haki ya dini zote ziheshimiwe

Kadinali Parolin pia alitoa maoni yake kuhusu ripoti iliyowasilishwa siku hiyo 17 Januaru 2024 kwa Baraza la Manaibu na ‘Open Doors’ kuhusu mateso ya Wakristo duniani kote: takriban watu milioni 365 wanateseka kwa vurugu na mateso kwa sababu ya imani zao. Hilo pia ni “hangaiko kubwa” kwa Vatican, alisema Kardinali: “Wakristo katika sehemu nyingi za ulimwengu hawana uhuru wa kidini ambao ni haki yao na ambayo ni haki ya dini zote kuheshimiwa katika dini zao,  maonesho ya uaminifu. Kwa upande mwingine, Injili ilikuwa tayari imeshaona... Kwa hili hatutaki kuendeleza mambo haya lakini kwa kiasi fulani ni hali ya Wakristo katika ulimwengu wa kupata uadui, upinzani na mateso. Ni ushuhuda katika jina la Yesu unaohusisha haya.”

Majadiliano na siasa

Hatimaye, swali kwa Katibu wa Vatican  katika  kukumbuka sura ya Kardinali Silvestrini, mtu wa mazungumzo na siasa na taasisi, juu ya aina ya mazungumzo iwezekanavyo leo kati ya siasa na Vatican. Mazungumzo ni ya lazima, kulingana na Kardinali Parolini kwamba: “Lazima kuwe na, na nmazungumzo lakini ikiwa tunakumbuka alilezea Papa mwanzoni mwa papa wake alisema kuwa uhusiano na siasa za Italia ni jukumu la Baraza la Maaskofu Italia(CEI). Hata hivyo, ninaamini kwamba katika hali fulani tunayoishi hatuwezi kuepuka uhusiano na Vatican. Jambo muhimu ni kwamba kuna uratibu, ushirikiano, kati ya Vatican na CEI kwa njia ambayo mambo sawa yanaletwa mbele.”

Nafasi ya maadili ya Kikristo katika siasa

Kulikuwa pia na swali kwa Kadinali Parolin kuhusu maadhimisho ya miaka 30 ya kumalizika kwa Demokrasia ya Kikristo ambayo yanatarajuwa katika siku za hivi karibuni ambapo alisema: “labda tunahisi ukosefu wa chombo cha kisiasa cha kubeba matakwa ya Wakatoliki?” Yaliyopita hayawezi kurudiwa,” alijibu Kardinali Parolin. “Ulikuwa msimu ambao ulikuwa na ukubwa wake na udhaifu wake na pia mipaka yake, lakini umeisha na tunajua jinsi gani. Zaidi ya mitindo, jambo muhimu ni kwamba maadili ya Wakatoliki - ambayo ni maadili ya kibinadamu - yanaweza kupata nafasi katika siasa za leo na pia kutafsiriwa katika ukweli.” Maadili kama vile ‘mshikamano’, ‘ kushirikishana’  ambayo pia ni ‘kanuni za Katiba yetu’alibainisha Kardinali Parolin. Maadili na mwisho wa maisha, mada ambayo imekuwa muhimu katika siku za hivi karibuni na sheria haijaidhinishwa huko Veneto, hivyo Kardinali alisem: “Ni mada yetu. Maisha katika awamu zake zote, vipimo vyake, usemi wake, kutoka mwanzo wa asili hadi mwisho wa asili.”

Msaada kwa Afrika:mkutano wa mpango wa Mattei 28&29 Januari

Kwa kuhitimisha tunatumaini kwamba msaada unaweza kutolewa kwa Mpango wa Mattei kwa  ajili ya Afrika, ambapo mkutano wa kimataifa utafanyika katika Seneti mnamo  tarehe 28 na 29 Januari 2024, Kwa maoni ya Kardinali alisema kuwa: “Afrika inahitaji ushirikiano wa kimataifa. Afrika lazima isuluhishe matatizo yake yenyewe. Na haiwezi kufanya hivyo ikiwa hakuna ushirikiano na usaidizi usio na nia kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.”

18 January 2024, 17:02