Baba Mtakatifu tarehe 25 Julai 2024 amemteua Askofu Robert Cissé wa Jimbo Katoliki la Sikasso kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bamako, nchini Mali na kumpandisha hadhi na hivyo kuwa Askofu mkuu. Baba Mtakatifu tarehe 25 Julai 2024 amemteua Askofu Robert Cissé wa Jimbo Katoliki la Sikasso kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bamako, nchini Mali na kumpandisha hadhi na hivyo kuwa Askofu mkuu.   (AFP or licensors)

Askofu Mkuu Robert Cissé wa Jimbo Kuu la Bamako, Mali

Baba Mtakatifu tarehe 25 Julai 2024 amemteua Askofu Robert Cissé wa Jimbo Katoliki la Sikasso kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bamako, nchini Mali na kumpandisha hadhi na hivyo kuwa Askofu mkuu. Askofu Robert Cissé wa Jimbo Kuu la Bamako alizaliwa tarehe 7 Julai 1968 huko Bamako, Mali. Baada ya malezi na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 10 Julai akapewa Daraja Takatifu ya Upadre; Tarehe 11 Februari 2023 akawekwa wakfu kuwa Askofu wa Jimbo la Sikkasso.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Kardinali Jean Zerbo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bamako lililoko nchini Mali la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu tarehe 25 Julai 2024 amemteua Askofu Robert Cissé wa Jimbo Katoliki la Sikasso kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bamako, nchini Mali na kumpandisha hadhi na hivyo kuwa Askofu mkuu. Askofu mkuu Robert Cissé wa Jimbo Kuu la Bamako alizaliwa tarehe 7 Julai 1968 huko Bamako, Mali. Baada ya malezi na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 10 Julai akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki Sikasso, nchini Mali. Tarehe 14 Desemba 2022, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Sikasso, lililoko nchini Mali na kuwekwa wakfu tarehe 11 Februari 2023. Na Baba Mtakatifu Franchisko tarehe 25 Julai 2024 akamteuwa kuwa ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bamako lililoko nchini Mali.

Kardinali Pietro Parolin akiwa nchini Mali kikazi.
Kardinali Pietro Parolin akiwa nchini Mali kikazi.

Itakumbukwa kwamba, Kardinali Jean Zerbo, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Bamako amelitumikia Kanisa kama Padre kwa muda wa miaka 50.4, na kama Askofu kwa miaka 35.68 na kama Kardinali miaka 7.08. Kardinali Zerbo alizaliwa tarehe 27 Desemba 1943 huko Sègou, Mali. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi kunako tarehe 10 Julai 1971, kwa ajili ya Jimbo Katoliki Bamako, Mali. Tarehe 21 Juni 1988 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo la Mopti na kuwekwa wakfu kuwa Askofu wa Jimbo la Mopt. Tarehe 27 Juni 1998, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bamako. Tarehe 28 Juni 2017 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Kardinali. Na ilipogota tarehe 25 Julai 2024 akang’atuka kutoka madarakani.

Uteuzi Bamako
27 July 2024, 14:37