Msemaji wa UNICEF,kutoka hospitali ya Gaza:Kutochukua hatua ni mauaji ya watoto
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto, UNICEF, James Elder akitokea katika hospitali ya Gaza wakati akizungumza na kwa njia ya video na waandishi wa habari tarehe Mosi Desemba 2023 wakiwa katika Jumba la Umoja wa Mataifa huko Geneva kuhusu hali halisi ya vita alisema: “Leo walio mamlakani waliamua kwamba mauaji ya watoto yaanze tena Gaza. Ikiwa mtanipa dakika, ninaweza kuwaambia kile nilichokuwa nimetayarisha kabla ya mashambulizi kuanza. Hali ya kibinaadamu huko Gaza ni ya hatari kiasi kwamba kitu chochote isipokuwa amani ya kudumu na misaada mikubwa ya dharura ambayo ikikosa itasababisha maafa kwa watoto wa Gaza. Kisha nizungumze kuhusu hali mbaya ya afya, lishe, maji na usafi wa mazingira, na jinsi hii inavyotishia janga la idadi isiyo na kifani kwa watoto wa Gaza. Huo ndio ukubwa wa mahitaji, vile vile kumekuwa na kukwama kwa misaada kwa muda mrefu, kwamba licha ya juhudi kubwa za majuma yaliyopita, hali ya afya, lishe na usafi inazidi kuwa mbaya siku hadi siku Na Ningehitimisha kwa kusema: Kwa hiyo ni muhimu kutekeleza usitishaji vita wa kudumu. Njia mbadala haifikirii kwa wale ambao tayari wanaishi katika ndoto. Kutochukua hatua, hatimaye, ni idhini ya mauaji ya watoto. Lakini hapa tupo. Mlipuko huo ulianza sekunde chache baada ya kumalizika kwa usitishaji mapigano.
Akiendelea Mwakilishi wa UNICEF amesema, mara moja nilikwenda Hospitali ya Nasser. Tulipokaribia niliona kwamba kulikuwa na shambulio la umbali wa mita 50 hivi. Nasser ndio hospitali kubwa zaidi inayofanya kazi huko Gaza. Ni karibu kwa uwezo wa 200%. Mamia ya wanawake na watoto hulala katika vyumba vya kusubiri na kwenye korido. Watoto walio na majeraha ya vita wako kila mahali. Hospitali haziwezi kuchukua wagonjwa wengine waliojeruhiwa. Mfumo umeharibiwa. Nilitembelea hospitali iliyo kaskazini mwa nchi, ambayo kwa kawaida hutakiwa kutoa rufaa kwa wataalamu. Sasa ni hospitali kubwa zaidi inayofanya kazi kaskazini. Bandeji za damu zimefunika sakafu. Wahudumu wa afya wamechoka. Kanisa ndani ya hospitali sasa ni chumba cha dharura pia ilishambuliwa. Nilimuona mama akilia huku mwanae akitokwa na damu hadi kufa. Kifo kiko kila mahali.
Bwan Elder kwa kusisitiza ameeleza kuwa: Nilikwenda hospitali ya Nasser juma zima. Kuwasikiliza watoto, wahudumu wa afya wa Palestina wenye ujasiri na wasiochoka, na familia. Nilicheza na watoto, nikijaribu kuwakengeusha kwa upole kutoka kwenye ndoto zao mbaya. Na wakati mwingine, niliweza kuona mabadiliko kidogo katika nyuso zao. Muonekano wa kurudi utotoni. Sivyo tena. Hofu imerudi. Pamoja na waliojeruhiwa. Nikiwa pale, miili yenye damu ilikuwa ikifika. Ni kutojali kufikiri kwamba mashambulizi zaidi dhidi ya wakazi wa Gaza yanaweza kusababisha kitu chochote zaidi ya mauaji. Hata hivyo, kulikuwa na milipuko mikubwa mitatu au minne karibu nilipokuwa huko. Bila shaka, mazungumzo yoyote kuhusu Gaza lazima yaanze kwa huruma. Inasikitisha sana kusikia jinsi baadhi walivyoweza kupuuza vifo vya kusikitisha vya watoto hawa; na sasa, leo hii, wanaonekana kuwa vizuri na vitisho, na wakatik mashambulizi yanaanza tena. Kukubali kafara ya watoto wa Gaza ina maana kwamba ubinadamu unajisalimisha. Hii ni nafasi yetu ya mwisho kabla hatujajikuta tukielezea janga lingine linaloweza kuepukika." Amehimitimisha mwakilishi huyo wa UNICEF.
https://twitter.com/1james_elder/status/1730475560323678402?s=48&t=OZqoKB6fQg2nZUE7tLYAGw