Tunahitaji kuwekeza zaidi ili kuzindua upya mfumo wa Ekolojia wa nchi yetu kwa kuweka ubunifu,mabadiliko ya kidijitali na maendeleo endelevu katikati ya ajenda.” Tunahitaji kuwekeza zaidi ili kuzindua upya mfumo wa Ekolojia wa nchi yetu kwa kuweka ubunifu,mabadiliko ya kidijitali na maendeleo endelevu katikati ya ajenda.”  (ANSA)

Tuzo kwa ajili ya Uvumbuzi wa kidijitali:zaidi ya miradi 30 bora ilitolewa

Katika Chumba cha Wafanyabiashara cha Roma,toleo la 2023 la Tuzo la ANGI(Chama cha Kitaifa cha Vijana Wavumbuzi) ilitolewa.Miongoni mwa tuzo zaidi ya thelathini kwa ajili ya miradi bora katika ulimwengu wa biashara na wanaoanza,pia kuna ile ya Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya kusaidia vijana na kukuza ushirikishwaji kupitia uboreshaji wa teknolojia ya kidijitali.

Vatican News

Sherehe ya tuzo za toleo la VI la Innovation Oscar ambayo ni Tuzo ya ANGI 2023(Chama cha Kitaifa cha Vijana Wavumbuzi)lililohamasishwa  na Jumuiya ya Kitaifa ya Vijana Wavumbuzi na iliyoandaliwa katika mpangilio mzuri kwenye Ukumbi wa Hakalu la Vibia Sabina na Adriano ambacho ni  Chumba cha Biashara cha Roma, lilifanyika katika siku za hivi karibuni. Kwa hiyo zaidi ya tuzo 30 zilitolewa ili kutuza miradi bora katika ulimwengu wa biashara na wanaoanza na kutoa heshima kwa baadhi ya watetezi wakuu wa mashirika ya kiraia na tabaka tawala ambao wamejitofautisha kwa taaluma yao muhimu.

Sherehe ya tuzo ilikuwa mafanikio ya ajabu kwa umma na yaliyomo, ambayo iliona uwepo wa wawakilishi wa taasisi za Italia na Ulaya. Rais wa ANGI, Gabriele Ferrieri (zamani ForbesU30), alitoa heshima na kutoa maoni yake kuwa: "Kusaidia vizazi vichanga, katika kuimarisha ubora wa Italia na kukuza vipaji ni chaguo msingi la dhamira ya Chama cha Kitaifa cha  Vijana Wavumbuzi. Tunahitaji kuwekeza zaidi ili kuzindua upya mfumo wa Ekolojia wa nchi yetu kwa kuweka ubunifu, mabadiliko ya kidijitali na maendeleo endelevu katikati ya ajenda.” Miongoni mwa kumbukumbu maalum zilizotolewa, za umuhimu hasa ni zile alizoonesha Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambaye katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa kusaidia vijana na uendelevu kama kanuni za ustawi kwa uvumbuzi kama njia kuu na kipengele cha ushirikishwaji wa kusaidia jamii.

12 December 2023, 16:09