Siku ya Wanayamapori Duniani 4 Machi. Siku ya Wanayamapori Duniani 4 Machi. 

Siku ya Wanyamapori duniani 2024:Kuunganisha Watu na Sayari.Kuchunguza Ubunifu wa Kidijitali

Siku ya Umoja wa Mataifa ya Wanyamapori Duniani(WWD)huadhimishwa kila mwaka tarehe 3 Machi.Siku hii WWD 2024 ni jukwaa la kubadilishana vizazi na kuwawezesha vijana kupitia sanaa,mawasilisho na mazungumzo kuhusu fursa zilizopo kwa mustakabali wetu endelevu wa pamoja katika uhifadhi wa wanyamapori kidijitali.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Siku ya Wanyamapori Duniani kwa mwaka 2024 inaakisi umuhimu wa wanyamapori na mazingira asilia katika kudumisha uwiano wa sayari yetu. Siku hii uadhimishwa kila tarehe 3 Machi ambayo ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2013 katika kuadhimisha tarehe ambayo, mnamo mwaka 1973, ilitiwa saini Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Mimea na Wanyama walio Hatarini Kutoweka. Kaulimbiu ya Siku hii ya WWD2024 ni “Kuunganisha Watu na Sayari. Kuchunguza Ubunifu wa Kidijitali katika Uhifadhi wa Wanyamapori.” Siku hii huadhimishwa ili kuongeza ufahamu wa jukumu la msingi ambalo bioanuwai inatekeleza katika kudumisha mazingira yenye afya tunamoishi. Madhumuni ya maadhimisho haya ni kukuza ufahamu wa uharaka wa kuhifadhi na kutumia maliasili kwa njia endelevu, na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za kulinda aina tajiri za maisha Duniani. Maadhimisho ya siku hii yanatualika kutafakari matendo yetu na jinsi yanavyoathiri bayoanuwai, ikisisitiza haja ya kujitolea kwa pamoja ili kuhakikisha maisha endelevu ya vizazi vijavyo.

Wanyamapori lazima walindwe
Wanyamapori lazima walindwe

Kwa Mujibu wa waandaaji wa Siku ya Wanyamapori Ulimwenguni (WWD) 2024, wanabainisha jinsi ambavyo wanachunguza uvumbuzi wa kidijitali na kuakisi jinsi teknolojia na huduma za uhifadhi wa kidijitali zinavyoweza kuendesha uhifadhi wa wanyamapori, biashara endelevu na halali ya wanyamapori na kuishi pamoja kwa binadamu na wanyamapori, sasa na kwa vizazi vijavyo katika ulimwengu unaozidi kushikamana. “Tuko katikati ya mapinduzi ya kimataifa ya kidijitali ambayo yanabomoa vizuizi kwa utawala wa kidijitali unaozingatia watu na kupata fursa sawa kwa wote kuibua nguvu ya mabadiliko ya kidijitali. ‘Mgawanyiko wa kidijitali’ unapungua polepole, huku muunganisho bora na ufikiaji wa Intaneti ukifikia asilimia 66 ya watu wetu duniani. Hata hivyo, karibu watu bilioni 2.7 ya idadi yetu ya kimataifa bado hawako mtandaoni.” Vile vile wanabainisha kwamba “Kwa wastani, ni asilimia 36 tu ya watu katika nchi zilizoendelea kidogo na nchi zinazoendelea zisizo na jukwaa wako mtandaoni. Wanawake na vijana wana uwezekano mkubwa wa kupata mapengo katika ufikiaji wa mtandao na/au ujuzi wa kidijitali unaotayarisha kazi.

Lengo la Siku ya Kimataifa ya Wanyamapori 2024(WWD2024)

Ubunifu wa kiteknolojia umefanya utafiti, mawasiliano, ufuatiliaji, uchanganuzi wa Vinasaba(DNA) na mambo mengine mengi ya uhifadhi wa wanyamapori kuwa rahisi, ufanisi zaidi na sahihi. Hata hivyo, ufikiaji usio sawa wa zana hizi mpya, uchafuzi wa mazingira na matumizi yasiyo endelevu ya teknolojia fulani yanasalia kuwa masuala muhimu katika kufikia ujumuishaji wa kidijitali kwa jumla ifikapo 2030.” Kwa njia hiyo “Siku ya Wanyamapori Ulimwenguni WWD)2024 ni jukwaa la kubadilishana vizazi na kuwawezesha vijana kupitia sanaa, mawasilisho na mazungumzo kuhusu fursa zilizopo kwa mustakabali wetu endelevu wa pamoja katika uhifadhi wa wanyamapori wa kidijitali.” Siku hii ya WWD2024 inatoa hatua ya kuruka juu ya kugundua ni uvumbuzi gani wa kidijitali unaopatikana sasa, ni tofauti zipi za makutano tunazokabiliana nazo na jinsi tunavyotaka muunganisho wetu wa kidijitali uimarishwe kwa watu wote na sayari.”

Kutunza misitu ili wanyama wapate kuishi
Kutunza misitu ili wanyama wapate kuishi

Mwaka huu, Sekretarieti ya CITES imeungana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, WILDLABS, Jackson Wild (mwenyeji wa Maonesho ya Siku ya Wanyamapori Duniani) na Mfuko wa Kimataifa wa Ustawi wa Wanyama (IFAW) (mwenyeji wa Shindano la Sanaa la Vijana la Siku ya Wanyamapori Duniani). Ikiwa  maadhimisho ya WWD2024  yalikuwa ni tarehe 3 Machi 2024, lakini tukio la Umoja wa Mataifa (kwa kiwango cha juu) limefanyika tarehe 4 Machi 2024 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani na imeoneshwa moja kwa moja kwenye Televisheni (WebTV.)” ya Umoja wa Mataifa. Kwa njia hiyo Siku ya Wanyamapori Duniani ni kwa ajili ya kuwaunganisha watu na ulimwengu wa asili na kutia moyo kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa wanyama na mimea baada ya siku nzima.

Siku ya Kimataifa ya Wanyamapori 2024
04 March 2024, 13:02