Hawa na baadhi ya viongozi ambao tayari wameanza mkutano huko Apulia (Puglia) nchini Italia mkutano uitwao G7. Hawa na baadhi ya viongozi ambao tayari wameanza mkutano huko Apulia (Puglia) nchini Italia mkutano uitwao G7.  (ANSA)

G7:Amref,Afrika sio bara la kuchukua na kuliogopa!

Tukio kuu la Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa G7 unafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15 Juni 2024 huko Puglia,katika jimbo la Brindisi kwenye mandhari ya kifahari iitwayo Borgo Egnazia.Mkurugenzi wa Amref Italia,sehemu ya shirika kubwa la afya la Afrika anatoa uchambuzi kuhusu bara la Afrika uhusu mkutano huo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hatuwezi kujenga mustakabali wa pamoja ikiwa tutaendelea kuiona Afrika kama bara ambalo tunaweza kuchukua kutoka kwao na kuliogopa. Huu ni wito wa Guglielmo Micucci, mkurugenzi wa Amref Italia, sehemu ya shirika kubwa la afya la Afrika, kwa kuzingatia tukio la Mkutano wa Viongpzi wakuu wa Nchi na Serikali(G7,) ambao umefunguliwa  tarehe 13 hadi 15 Juni 2024 huko Puglia katika jimbo la Brindisi kwenye mandhari ya kifahari iitwayo Borgo Egnazia. Kwa njia hiyo migogoro ya kivitia, ya tabianchi, Mpango wa Mattei na tahadhari kuelekea Afrika changa na yenye nguvu, ndiyo  hasa ujumbe ulioelekezwa kwa Wakuu wa Nchi. Katika fursa hiyo Shirika la Amrefu pia  linatoa tafakari kuhusu Akili Mnemba (AI,) mojawapo ya  zinazohusu G7.

Hata rais wa Ukraine amekaribishwa katika G7
Hata rais wa Ukraine amekaribishwa katika G7

Ka maana hiyo Afrika inakuwa mojawapo ya mada kuu za G7, chini ya urais wa Italia. Tayari katika siku ya kwanza, mpango huo unajumuisha mipango yenye kichwa: “Afrika, Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo.” Mabadiliko ya tabianchi yanaathiri zaidi zile nchi ambazo hazijashiriki katika ongezeko la uchafuzi wa mazingira unaoathiri hali ya hewa, alisema Micucci akihojiwa na Shirika la Habari za Kanisa la Italia (SIR)

Kikao cha kwanza na viongozi hawa wa G7
Kikao cha kwanza na viongozi hawa wa G7

Bara, ambalo husababisha chini ya 2-3% ya uzalishaji wa gesi chafuzi duniani na ambalo, kutokana na uhaba wa rasilimali, lina uwezo mdogo wa kukabiliana na athari za ongezeko la joto duniani, kwa mara nyingine tena litalipa bei kubwa sana kwa ukosefu wa hatua za haraka kukabiliana na changamoto hii duniani kote. Ukumbusho fulani kutoka kwa mkurugenzi wa Amref Italia ulikwenda moja kwa moja katika  migogoro kwamba: “tunaomba tahadhari itolewe kwa vita vilivyosahaulika, ambavyo vinasukuma watu kukimbia, kwa sababu hawaoni tena siku zijazo. Wacha umakini wa G7 urejee katika maeneo hayo.”

Viongozi wa Afrika walifika katika mkutano Italia kuhusu mpango wa Mattei Januari 2024
Viongozi wa Afrika walifika katika mkutano Italia kuhusu mpango wa Mattei Januari 2024

Kuhusu Mpango wa Mattei, Bwana Micucci alisema: “tunaomba sana Afrika isikilizwe. Kwa sasa tumezungumza kuhusu nishati, uhamiaji, Afrika Kaskazini.” Hii inatoa wazo wazi kwamba mtazamo yunaelekezwa kwetu tena. Njia hiyo si sahihi. Kabla hatujaanguka, lazima tuhusishe waingiliaji wa Kiafrika kwa Mpango na Afrika. Kwa upande mwingine wa Mediterania kuna zaidi ya watu bilioni 1.4 ambao wanataka kushinda maisha yao ya baadaye, kubaki katika nchi zao wenyewe, ili kuhakikisha maendeleo ambayo ni huru lakini yanayounganishwa na yetu.

Wageni wa G7
Wageni wa G7

Hatutaweza kujenga mustakabali iwapo tutaendelea kuiona Afrika kama bara la kuchukua na kuliogopa.  Micucci alikumbuka kwamba Afrika ni bara changa, ambapo 60% ya watu ni chini ya miaka 25. Matumaini yake ni kwamba watu wenye nguvu duniani wakome kufikiria nini kinaweza kuwa kizuri kwa Afrika na kuanza kusikiliza bara.

Viongozi washiriki wa G7

Kwa hiyo kuanzia tarehe 13 hadi 15 Juni 2024, Borgo Egnazia, mjini Puglia, anakuwa mwenyeji wa Mkutano wa G7 wa Urais wa Italia. Siku tatu za vikao ambapo Viongozi watashughulikia masuala makuu ya kimataifa. Tukio hilo litawaleta pamoja Viongozi wa Nchi saba wanachama, pamoja na Rais wa Baraza la Ulaya na Rais wa Tume ya Ulaya anayewakilisha Umoja wa Ulaya. Sambamba na vikao vya awali vya G7, wawakilishi wa Mataifa kadhaa na Mashirika ya Kimataifa watashiriki katika vikao hivyo, vilivyoalikwa na Taifa linaloshikilia Urais.

Waziri Mkuu wa Italia akiwa katika eneo la Mkutano wa G7
Waziri Mkuu wa Italia akiwa katika eneo la Mkutano wa G7

Kwa hiyo wanaoshiriki mkutano huo ni pamoja na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Waziri Mkuu wa Vanada Jastin Trudeau, Rais wa Ufaransa, Emmanuale Macron, Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, Rais wa Marekani, Joe Biden, Waziri Mkuu wa Japan, Rish Sunak na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von de Leyen, vile vile Mataifa na mashirika ya Kimataifa orodha inaonesha kuwa:  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – Akinwumi Adesina, Rais wa Algeria – Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Argentina – Javier Milei, Rais wa  Brazili – Luis Ignacio Lula da Silva, Rais (Urais wa G20), Vatican, Baba Mtakatifu Francisko, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, Mkurugenzi mkuu wa  Shirika la Fedha la Kimataifa – Kristalina Georgieva, Mfalme wa Jordan – Abdallah II, Rais wa Kenya,  William Ruto, Rais wa Mauritania – Mohamed Ould Ghazouani,na (Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika), Katibu Mkuu wa OECD – Mathias Cormann, Rais wa Tunisia – Kaïs Saïed, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa – Antònio Guterres, Rais wa  Umoja wa Falme za Kiarabu – Mohammed bin Zayed, Rais wa  Benki ya Dunia – Ajay Banga, Rais.

 

13 June 2024, 15:14