Tafuta

2024.03.28  Udugu wa Yesu Mrazareti huko Sonsonate, El Salvador. 2024.03.28 Udugu wa Yesu Mrazareti huko Sonsonate, El Salvador.   (Hermana de Jesús Nazareno de Sonsonate)

Papa,El Salvador:Wakristo ni mashuhuda wa wema na udugu

Katika ujumbe aliouelekeza kwa Udugu wa Yesu Mnazareti wa Sonsonate,wakati wa kuadhimisha miaka 420 tangu kuanzishwa kwa udugu huo Baba Ntakatifu Francisko anawataka waamini kumtumikia Mungu kwa maisha yao na sio kutazama kutoka kwenye balkoni sadaka yake kwa ajili ya wanadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amewatumia ujumbe Udugu wa Yesu wa Nazareti wa Sansonate nchini El Slvador uliokezwa kwa Askofu Costantine Barrera Askofu wa Jimbo la Sonsonate  na wote wakiwa wanaadhimisha miaka 420 tangu kufika wa picha ya Mnazareti. Na kwa wote lazima wawe wa Yesu wa Nazaret. Katika ujumbe huo Papa amewashukuru kwa kumruhusu kushiriki katika ukumbusho wa kuwasili kwa sanamu ya Yesu wa Nazareti katika nchi hiyo, mwaka 1604 na kwa fursa ya kujiunga na sherehe yao katika siku hii kuu ya Ijumaa Kuu. Ni muhimu kuona jinsi Bwana anavyotumia lugha yetu duni kufikisha ujumbe wa kimungu kwetu. Hata leo hii tunangoja, kama wazee wetu walivyofanya zaidi ya miaka 400 iliyopita, kuona sura ya Yesu wa Nazareti ikitokea. Lakini, tunataka kuona nini? sanamu nzuri? Kazi ya sanaa ya thamani? Shamrashamra za watu?

Maadhimisho ya miaka 420 ua Picha ya Yesu Mnazareti huko El Salvador
Maadhimisho ya miaka 420 ua Picha ya Yesu Mnazareti huko El Salvador

Baba Mtakatifu amsema kwamba “Hakuna kati ya haya, kama ilivyo kwa  kila mwaka, tukitazama nje ya mlango wa nyumba zetu ni kumwona Yesu akija, tukikumbuka, kwa namna fulani, mtazamo wa watu wa Israeli, wakati, kila mmoja kwenye mlango wa hema lake, akifuata na macho ya Musa ambaye alikwenda kuelekea Utukufu wa Mungu (taz. Kut 33:8). Kama Musa, sisi pia tunaweza kupanda katika uwepo wa Bwana ili kuzungumza naye, “uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki” (taz 11). Tunaweza kufanya hivyo katika sala, ikiwa tunaiga imani yake. Katika sala hiyo Musa alimwomba Bwana kitu ambacho sisi pia tunatafuta, kwamba angemwonesha njia yake (taz Kut 33, 13). Mungu alimwahidi: “au nitakwenda pamoja nawe na kukupumzisha”na kwa uhakika huo nabii alivuka jangwa. Hata hivyo, kwa kuwa Mungu alikuwa mkuu sana, Musa hakuwa na fursa ya kuuona uso wake (rej. 20) na alipokabiliwa na majaribu ya maisha mara nyingi imani yake ilidhoofika. Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa “hata hivyo, tunaweza kuutafakari uso wa Mungu na kuhisi miguu yake ikitembea pamoja nasi. Hii ndiyo ahadi ambayo Mungu anatufanya wakati Mnazareti anapokengeuka hatua zake kuingia jirani yetu, kuvuka barabara yetu na kusimama kwenye mlango wa nyumba zetu. Mtazamo wake wa upendo uliovuliwa hutuchunguza na kutuuliza maswali, kama anavyofanya na Mtakatifu Petro, akituambia: “Je, unanipenda?”(Lk 22:61; Yh 21:15-17).

Maadhimisho ya miaka 420 tangu kufika kwa picha ya mnazareti
Maadhimisho ya miaka 420 tangu kufika kwa picha ya mnazareti

Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa “licha ya kutostahili kwetu, kutokuwa na shukrani kwetu mara kwa mara, hebu tumjibu kila wakati kwa ukarimu: “Bwana, unajua kwamba nakupenda.” Kwa sababu, kwa kujibu kwa njia hii, tunaiga katika maisha yetu mtazamo wa Waisraeli, ambao walibaki kusujudu, kila mmoja kwenye mlango wa hema lao, wakati Utukufu wa Mungu uliposhuka juu yao (taz. 10). Katika mtazamo huu wa kuabudu, hebu tujionyeshe kuwa wapole kwa mienendo ya Roho wake ambaye, kama wingu la moto, anaongoza hatua zetu katika jangwa hili (ona Kut 40, 37). Ingekuwa ya kuhuzunisha jinsi gani ikiwa kila Ijumaa Kuu mioyo yetu ingebaki tu kutazama kutoka kwenye balcokoni kwenye tukio la udadisi, bila kusujudu Yesu alipokuwa akipita, bila kusikia mwaliko wake wa kumfuata kama Petro (rej.Yh 21:19). Ni aibu iliyoje ikiwa hatukuelewa kwamba ni kwa kushikamana na Msalaba wake kwamba tunaweza kutembea pamoja naye, na hatukutambua kwamba ndiye anayebeba nira hii ili tupate pumziko letu. Baba Mtakatifu Francisko amekazia kusema kuwa “ leo Bwana, kama kila mwaka, kama kila dakika, huja kukutana nasi, na tumfuate, tukimbeba mabegani mwetu, tukimfariji katika jeraha la wazi la ndugu zetu wanaoteseka. Hebu tumwombe atuoneshe jinsi tunapaswa kumtukuza Mungukwa maisha yetu, kufanya huduma yetu kuwa sifa, katika kazi zetu za kila siku, katika familia zetu, katika kujitolea kwetu kuunda jamii ya kidugu zaidi, kimsingi, katika ushuhuda wa mema ambayo sote tunaweza kutoa, bila kujali wito ambao tumeitiwa(Yh 21:19). Yesu wa Nazareti kutoka Kalvari awabariki na Mama yake Mwenye Huzuni awalinde. Na tafadhali msisahahu  kuniombea.”

Ukumbe wa Papa kwa El Salvador
28 March 2024, 16:34