Tafuta

2023.06.05 Kardinali Parolini akiwahutubia wajumbe wa Mfuko wa Centesimus Annus Pro Pontifice. 2023.06.05 Kardinali Parolini akiwahutubia wajumbe wa Mfuko wa Centesimus Annus Pro Pontifice.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kard.Parolin:migogoro ya sasa yahitaji majibu ya kimataifa

Katibu wa Vatican amefunga mkutano wa siku mbili wa Mfuko wa Centesimus Annus Pro Pontifice,unaoadhimisha miaka 30.Urafiki kijamii na utamaduni wa kukutana ni thamani jumuishi ambazo zinahamasisha ukweli wa maendeleo ya kijamii na ishara muhimu ya ushirikiano.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ni hatari kwamba siasa pia zinaweza kuendeshwa, zikisukumwa kuzingatia maslahi binafsi yaliyoingiliwa badala ya juhudi zinazohusika katika maono ya manufaa mapana ya pamoja, ambayo ni pamoja na ulinzi hata kwa wale ambao kamwe hawaingii katika maamuzi, waliotengwa kwa kila aina. Na bado kuna mambo mawili ambayo yanaweza kusababisha mshikamano na ushirikiano zaidi, ambayo Papa anasisitiza sana yaani urafiki wa kijamii na utamaduni wa kukutana. Kardinali Pietro Parolin katibu wa Vatican, ameweka hayo wazo kuwa ni tunu  mbili msingi na pendwa za Papa Francisko katika hotuba aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Mfuko wa Centesimus Annus Pro Pontifice katika fursa ya kuadhimisha miaka 30 tangu kuundwa kwake.  Katibu wa Vatican  aliingilia kati katika Ukumbi wa Jumba la Kitume wa Clementina mjini Vatican mbele ya washiriki,  akizingatia neno  la Papa Francisko juu ya jumuiya, Neno lililomo kwenye kauli mbiu ya  mkutano  huo kuhusu “Kumbukumbu ya kujenga mustakabali: Kufikiria na kutenda kwa kuzingatia jumuiya”.

Katibu wa Vatican akihutumia wajumbe wa Centesimus Pro Pontefice
Katibu wa Vatican akihutumia wajumbe wa Centesimus Pro Pontefice

Kardinali alisema “Kufikia sasa ni wazi kwa kila mtu kwamba matatizo, utafutaji wa ufumbuzi na matarajio ya kaka zetu wengi na dada zetu yana mwelekeo wa kimataifa na yanahitaji majibu sawa ya kimataifa”. Na kwa hivyo, kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya jamii, miito ya kawaida ya amani au ukuaji wa uchumi au uzuri wa mazingira hayatoshi. Dhana ya manufaa ya wote lazima ieleweke, na labda ieleweke tena, alidokeza Kardinali Parolin, ili kuepuka zama au shughuli zinazokuza suluhisho maalum, kwa kuwa hizi zinaweza kusababisha kutengwa au kupotea fursa kwa kila mtu. Na hapo urafiki wa kijamii na utamaduni wa kukutana, alisema katibu wa Vatican hutoa maoni muhimu kwa ajili ya kufikia manufaa halisi ya kawaida, kwa sababu zote mbili ni sifa za jamii iliyo wazi na yenye mwelekeo wa siku zijazo. Urafiki wa kijamii kwa sababu, kwa asili yake ni mjumuisho na husaidia kupanga shughuli sio tu kwa jumuiya au nchi ya mtu binafsi. Utamaduni wa kukutana kwa sababu, mbali na kuchochea matendo ya mara kwa mara ya upendo ambayo hujidanganya katika kuondoa ubaguzi, badala yake ni mtindo wa maisha ambao unajua jinsi ya kuheshimu hadhi  na uhuru wa wote kwa njia halisi.

Ikiwa waraka  wa  Centesimus Annus wa Yohane Paulo II ulichapishwa mnmao mwaka 1991,majisterio  ilihusishwa katika wakati huo wa kihistoria umuhimu mkubwa wa maadili kama vile demokrasia na uhuru, ambayo leo hii kwa mujibu wa Kardinali Parolin alionesha hali ya sasa kwamba unapata mwangwi katika tafakari iliyohamaishwa na Papa Francisko katika Waraka wa Fratelli tutti, ambapo anasisitiza kwamba maneno kama vile demokrasia, uhuru, haki au umoja yamekunjwa na kutengenezwa ili kutumika kama vyombo vya kutawala, kama lebo zisizo na maana, na nzuri katika hatua yoyote. Kudhoofika kwa maadili tata ambayo wale wanaochukua maamuzi ya kisiasa au kiuchumi wanapaswa kuyapima leo kunahitaji, utambuzi makini wa kulinda maslahi ya jumla. Kimsingi, ni suala la wajibu unaoelekeza maamuzi, na rasilimali, kuelekea ufahamu kamili wa wanadamu wote, ukuaji wao na matarajio yao, kwa msingi wa hadhi na utambulisho wao, alihitimisha Kardinali Parolin.

Hotuba ya Kardinali Parolin kwa wajumbe wa Centesimus Pro Pontefice
05 June 2023, 18:30