Tafuta

Utambulisho wetu sisi ni akina nani?

Vatican News ni mfumo mpya wa mawasiliano kutoka Vatican. Hii ni safari iliyoanza kushika kasi kunako tarehe 27 Juni 2015 kwa Barua binafsi ya Baba Mtakatifu Francisko iliyoanzisha Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Vatican News, ni mfumo wa kidigitali unaotumaini kujibu ili kukidhi mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanyika kwa kuzingatia mahali na mfumo wa mawasiliano. Mfumo huu unajikita na kutenda zaidi katika mpango mkakati unaozingatia tamaduni, njia mbali mbali za mawasiliano na vitendea kazi vyake.

Vatican News inajipambanua zaidi katika Nyanja kuu nne za habari zake: Shughuli za Baba Mtakatifu, Vatican, Makanisa Mahalia pamoja na Habari za Dunia. Kwa mara ya kwanza Vatican News imeanza kutekelezwa na Wahariri kutoka karika Lugha kuu Nne (Kitaalia, Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kihispania na Kireno) baadaye lugha nyingine 33 zitajumuishwa, humu ndani, ikiwemo lugha ya Kiswahili. Vatican News inapenda si tu kuhabarisha, lakini zaidi inapenda kutoa ufunguo utakaowawezesha kutafsiri matukio haya kwa mwanga wa Injili.

Kumbe, changamoto kubwa ni kuweza kujibu “ kwa ufanisi mahitaji ya utume wa Kanisa” katika tamaduni mamboleo, kwa kuwa na lengo kuu la “kutangaza na kushuhudia Injili ya huruma ya Mungu kwa watu wote” kwa watu wa tamaduni, mila na desturi mbali mbali.

Vigezo msingi ni “Utume na Umisionari kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa hali ngumu ya maisha ya watu, umaskini na changamoto wanazokabiliana nazo “Hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko kwa Baraza la Kipapa la Mawasiliano 4 Mei 2017.

 

KURUGENZI YA UHARIRI

Andrea Tornielli (Mhariri mkuu), Sergio Centofanti na Alessandro Gisotti, Wahariri Wasaidizi

 

MRATIBU WA RADIO VATICAN- VATICAN NEWS

Massimiliano Menichetti (Mhariri Mkuu Msaidizi)