Msumbiji:wito wa Maaskofu kwa ajili ya amani ya Cabo Delgado
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Sala kwa ajili ya waathirika wote wa janga la covid-19 na wito kwa ajili ya amani ya Mkoa wa Cabo Delgado, ambao kwa kipindi umekuwa ni wa ghasia ambazo haziishi kutokana na makundi ya kisilaha ya kijitahadi, ndiyo mambo makuu yaliyozungumzwa na Baraza la Maaksofu nchini Msumbiji (Cem). Ni katika taarifa yao, mara baada ya Mkutano wao wa mwaka ulioanza tarehe 9 hadi 14 Novemba katika Seminari ya kikanda ya Mtakatifu Agostino huko Matola. Kwa kuongongozwa na sehemu ya Injili ya Yohane, nawapa amani, na ninaachien amani yangu”, hti ya maaskofu inafunguliwa na salama za udugu wa ukaribu wa Baraza hilo kwa ndugu wote kike na kiume wa Cabo Delgado”, wakiwakumbuka daima katika sala zao, na matumaini ya kuweza kupata njia za mazungumzo ambayo yanarahisha mwisho wa mgogoro huo wa hatari na athari mbaya ya kibinadamu ambayo inaendelea.
Kwa sasa katika eneo hilo wanahezabiwa zaidi ya vifo elfu mbili na watu 400,000 waliorundikana ndani kwa sababu ya ghasia, kutumia nguvu, kutekwa nyara, uharifu na ukiukwaji wa haki. Mbele ya majanga maaskofu wa Msumbiji wanaandika kuwa kuna ulazima wa kuongeza nguvu katika taasisi zote za upendo kwa ajili ya kukimbilia wahitaji,hasa katika hali halisi ambaya ya watu mahali wanapoishi. Katika muktadha huo, Maaskofu wanakumbusha hata mchango uliotumwa na Papa Francisko, ambao ulitolewa maalum kwa ajili ya watu wengi waliokusanyika ndani ukuwa na thamani ya euro mila moja elfu. Pamoja na msaada huo lakini wanasema ni uwajibikaji wa kila mmoja kufanya kazi ili kweli kuweza kuondokana na mgogoro huo wa sasa, na wakiwaalika waamini wafanya kazi kwa ajili ya upatanisho wa ktaifa , wa amani na ustawi wa wote. Wakiwa katika mkutano wao, wa Mwaka Maaskofu hao walitembelea na Balozi wa Kitume nchini humo, Askofu Mkuu Piergiorgio Bertoldi, ambaye amewatia moyo waendelea katika utume wao katika jamumuiy kwa matarajio ya kutoa huduma.
Katikati ya kutano wao, ulikuwa pia mada ya semianro ambazo wamezsema ni lazima kuanza huduma zao ikiwa na uwezekano, shughuli za mafunzo zilizosimama kutokana na janga la Covid-19. Maskofu wakitazama uzoefu wa virusi vya Corona ambalo hadi tarehe 17 Novemba 2020 vimesababisha kesi 14,500 na vifo 116 maaskofu wamependelea uwezekano wa kuanza kwa maadhimisho ya misa katika maparokia. Lakini hata hivyo uchumi mkubwa kwamba ni kuanza kwa shughuli hiyo hauwezi kuwa mwema katika jumuiya za vijiji, hasa wale ambao hawawezi kufuata kanuni zilizoombwa za kiprotokali kiafya kutokana na rasilimali za kiuchumi ambazo ni kikwazo. Kanisa Katoliki nchi Msumbiji kwa maana hiyo limewashauri wasikate tamaa katika kipindi hiki cha majaribu na badala yake cheche za matumaini na Imani katika Kristo ziwe hai. Ujumbe wao unahitimishakwa kwa kuwatakia baraka ya amani, furaha na matumaini ya siku kuu zijazo za Kuzaliwa kwa Bwana.