Tafuta

2021.03.08  Papa Francisko akiwa narudi kutoka Iraq anajibu maswali ya waandishi wa habari. 2021.03.08 Papa Francisko akiwa narudi kutoka Iraq anajibu maswali ya waandishi wa habari. 

Lebanon,Paroko wa Beirut:watu wote wanahitaji kukumbatiwa na Papa

Ahadi ya ziara ya kutembelea nchi ya mierezi iliyosemwa na Papa Francisko wakati akiwa kwenye ndege anarudi kutoka Iraq,imebua hisia nzuri na matumaini.Katika mahojiano na Padre Jad Chlouk,wa Kanisa Kuu la Mtakatifu George ambalo liliharibiwa Agosti iliyopita, wakati wa mlipuko wa bandari ya mji mkuu wa Lebanon amesema wanamsubiri kwa hamu ili waimarishe imani yao.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Upepo wa matumaini umerejea huko Lebanon. Wakati Baba Mtakatifu Francisko, anarudi  kutoka safari yake ya kihistoria ya  Iraq, alifungua dirisha la uwezekano wa kufanya ziara ya kitume katika Ardhi ya Mwerezi, ambapo mioyo ya Walebanon imejaa furaha kubwa kusikia hivyo. Maneno ya Papa  aliyejulisha kwamba alikuwa amemwandikia Kardinali Béchara Boutros Raï barua, Patiaki wa Antiokia ya Wamaronites, akiahidi safari ya kwenda kwenye ardhi hiyo ya mateso na migogoro ya maisha, imepata mwangwi usiokuwa wa kawaida kwenye mitandao ya kijamii na katika mjadala wa umma.

Kwa haraka mitandao ya kijamii imeandika juu ya kile ambacho Papa Francisko alisema kwa mujibu wa Padre Jad Chlouk, wa Kanisa la Kimaronites wa Mtakatifu Giorge huko  Beirut. Kuhani huyo, ambaye machoni pake bado anakumbuka vema  uharibifu wa eneo lake la ibada umbali wa mita mia sita tu kutoka katika mlipuko wenye nguvu ulioharibu bandari ya mji mkuu wa Lebanon mnamo Agosti iliyopita., ameeleza kuwa kungojea Papa sio tu kwa Kanisa la kidini lakini pia kwa watu wote.  Hii ni kwa sababu tunahitaji kuwa na uwezo wa kugusa tumaini, kuweza kujua kwamba kuna mtu anayetuunga mkono”, amesisitiza kuhani huyo. Aidha Padre Jad Chlouk anaongeza: “Wakati Baba Mtakatifu alipokwenda Iraq kuwaimarisha watu na kuwahimiza upatanisho wa kweli, analenga kufanya safari kama hiyo ili Lebanon iliyokata tamaa, kuchanganyikiwa, na kukosa tumaini iweze kupatanishwa tofauti zake”.

Hata hivyo mesema kuhani  Mmaroniti, wao  hawataki kuondoka nchini, licha ya shida za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Na Papa yuko sahihi kwani Lebanon iko katika  hatari za  maisha na ina hatari ya kupoteza jumuiya  nyingi za Kikristo kwa  mfano, Wasiria, Wagiriki-Wakatoliki, Wagiriki-Waorthodox, Walatini. Hii ndio sababu tunasubiri ziara yake ambayo itatupatia nguvu ya kutekeleza dhamira yetu tena ya kimisionari”,amesema. Padre Jad Chlouk amesimulia kuwa Lebanon inaendelea kuteseka kwa nguvu kutokana na vijana wakristo ambao wanaendelea kuacha nchi yao katika kufuta hali bora, yenye msimamo na amani. “Kila wiki, kila mmoja wetu huaga kwa marafiki wasiopungua wawili. Na hii ni ngumu kwetu. Lakini pia watu wenye  zaidi ya miaka  50 wanakimbia, wakiondoka ili kuanza maisha kwa upya. Ni hasara ambayo haisimami lakini, badala yake, inazidi kuongezeka zaidi.

13 March 2021, 16:53