Fiji,Ask.mkuu Suva:Pasaka ni zawadi ya amani ya Mungu
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Pasaka ni zawadi ya bure ya amani ya Mungu kwa mujibu wa Askofu Mkuu Peter Loy Chong, wajimbo kuu katoliki la Suva, katika visiwa vya Fiji, kwenye barua yake ya kichugaji katika fursa ya Siku Kuu ya Ufufuko wa Bwana, Dominika tarehe 4 Aprili 2021. Ni Siku kuu katika siku kuu, anafafanua Askofu Mkuu huku akikumbusha umuhimu wa ishara ambazo ni muhimu kuwasilisha kazi ya wokovu wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Sherehe za Juma Kuu Takatifu kwa maana hiyo zimejaa ishara nyingi na si tu katika kurudisha nyuma ya matukio yaliyopita, lakini hasa katika kuchangia wakati huu uliopo, amesisitiza. Kwa jinsi hiyo matukio ya wokovu wa maisha ya Yesu unageuka kuwa sasa na kumbu kumbu zinazosaidia kuweka kitovu cha wokovu, neema na uhuru, zawadi za bure za Mungu katika uzoefu wa wanaume na wanawake wa leo hii” amesisitiza Askofu Mkuu Loy Chong,
Kwa maana hiyo Askofu Mkuu Suva, ameongeza kusema kwamba kumbu kumbu ya wakati ule, maana yake ni kuifanya iwe ya wakati uliopo ili ufufuko wa Kristo isitazamwe kwa wakati uliopita, bali uwe hai kwa wakati uliopo sasa. “Ufufuko wa Kristo ni sasa na siku tatu za maandalizi zinasaidia wakati uliopo sasa kuwa na liturujia kubwa, ibada kubwa ya upendo wa wokovu wa Mungu kwa binadamu wote”.
Akitazama matatizo mengi ambao yanakumba karne hii, miongoni mwake likiwa janga la Covid-19 na hatari ya kuongezeka kwa kimo cha baharí ambacho kinaviunganisha visiwa vyote vya Pasifiki, Askofu Mkuu Suva amesisitiza kuwa Mungu ni upendo na kile ambacho Mungu afanyacho ni upendo tu. Lakini yeye pia alifanya zawadi ya ubinadamu wa uhuru. Kwa binadamu anaweza kukubali kwa utimilifu wa upendo wa Bwana na kufanya uzoefu wa ujazo wa misha au kuchagua kubaki katika giza. Juma Takatifu, linasaidie kutafakari upendo na amani ambavyo vimetolewa zawadi ya Mungu na kushirikishana mpango wake wa wokovu kwa binadamu na kazi yake yote ya uumbaji.